Skip to main content

Posts

Showing posts with the label afya

FANYA HIVI KAMA UNASUMBULIWA NA CHUNUSI

  FANYA HIVI KAMA UNASUMBULIWA NA CHUNUSI. Chunusi ni vimbe zinazosababishwa na kuzibika kwa folikoli za nywele na mafuta ya ngozi (sebum), seli za ngozi zilizokufa, na protini zilizokufa. Kuziba huku kunavuta bakteria wa ngozi ambao husababisha uvimbe na kuongezeka kwa vimbe hizi. Sebum ni dutu yenye mafuta inayozalishwa na tezi za mafuta kwenye ngozi yako. Sebum inalinda ngozi, lakini unapozalishwa kupita kiasi, inaweza kuziba njia za ngozi, kufunga seli za ngozi zilizokufa, na kuvuta bakteria wa ngozi, hivyo kusababisha uvimbe na chunusi.   Uzalishaji wa sebum kupita kiasi unatokana na homoni za ngono zinazosambaa sana kwenye damu. Hii ndiyo sababu chunusi ni kawaida kwa vijana na watu wazima vijana. Protini inayojulikana kama Sex Hormone Binding Globulin (SHBG) inapunguza homoni za ngono zisizo na mpangilio.   SHBG inashikilia homoni hizi za ngono ili zisilete athari zisizohitajika kwenye seli na viungo kama ngozi. Homoni hizi za ngono ni estrogeni na testos...

JINSI YA KUZUIA NA KUKABILIANA NA UGONJWA WA GOUT.

  KUHUSIANA NA UGONJWA WA GOUT. Kuna component moja hujulikana kama FRUCTOSE . Hii ni component hatari sana katika afya ya mwanadamu, lakini cha kushangaza ni kwamba wanadamu wengi wanaitumia kwa kuifurahia bila kujua ya kwamba hii ni sumu ambayo inawamaliza taratibu. Fructose hupatikana katika sukari, asali pamoja na matunda matamu. Fructose inapoingia katika mwili, mchakato wake hufanyika katika ini tu. Na hutambuliwa na enzyme ijulikanayo kwa jina la FRUCTOKINASE . Kazi ya Fructokinase ni kufanya metabolism ya Fructose ili iweze kua FRUCTOSE 1 PHOSPHATE . Mchakato huu hupelekea enzyme nyingine kuamshwa ijulikanayo kama ADENOSINE MONOPHOSPHATE DEAMINASE ambayo hupelekea kuzalishwa kwa taka mwili ijulikanayo kama URIC ACID. URIC ACID ndio chanzo kikuu cha GOUT. Wengi watakwambia ya kwamba Gout inasababishwa na ulaji wa nyama nyekundu. Mtu akikwambia hivi, mwambie ya kwamba Gout inasababishwa na kuwepo kwa kiwango cha Uric Acid katika damu ambacho husababishwa na FRUCT...

MBINU 3 ZA MAMA ANAYENYONYESHA KUPATA MAZIWA MENGI

  ILI MWANAMKE AZALISHE MAZIWA MENGI Kwa muda mrefu sana wanawake wanaonyonyesha wamekua wakiambiwa mambo kadhaa ili kuweza kuzalisha maziwa ya kutosha kwa ajili ya watoto wao. Mfano wa vitu wanavyoambiwa ni; ·        Kula mara kwa mara upate maziwa ·        Kunywa maziwa ili upate maziwa ·        Kunywa soda ya coca ili uzalishe maziwa ·        Kula matunda mengi ·        Kunywa juisi ya Ribena ·        Na mengine mengi. Maziwa ya mama huzalishwa katika FAT LOBULES . Na ndio sababu kwa nini matiti ya mama hua makubwa pale anapokua mjamzito. Hakuna bomba kwenye titi la mwanamke ambalo litazalisha maziwa eti kwa sababu amekula chakula flani. Chakula anachokula mama ni lazima kipitie mmeng`enyo na kuweza kufyonzwa katika mwili. Maziwa ya mama huhifadhiwa katika Fat Lobules kabla ya kus...

HALI YA KUKOSA CHOO AU KUPATA CHOO KIGUMU.

 HALI YA KUKOSA CHOO AU KUPATA CHOO KIGUMU. Kukosa choo ni hali ya kushindwa kupata choo baada ya saa 72 tangu upate choo mara ya mwisho. Kama muda haujafika saa 72 haitaitwa hali ya kukosa choo. Ni lazima saa 72 zitimie. Zipo sababu kadhaa zinazoweza kusababisha mtu kuchelewa kupata choo kama vile;-         I.             Unapokua umefunga kula       II.             Unapobadilisha mazingira uliyoyazoea kujisaidia.     III.             Unapovadilisha muda ambao umezoea kujisaidia. Endapo utazidisha Zaidi ya saa 72 bila kupata choo basi fanya yafuatayo;-         I.             Usizidishe kiwango cha nyuzi nyuzi, kwani ni sawa na kuongeza idadi y...

FUNGA KULA ILI KUEPUKANA NA MARADHI

  FUNGA KULA ILI UEPUKANE NA MARADHI. Mwili wa mwanadamu haukuumbwa ili uwe na maradhi au kuugua. Lakini ni kwa nini mwanadamu hua anasumbuliwa na maradhi? Jaribu kuangalia wanyama kama sokwe, papa au mbwa mwitu. Ni wanyama ambao ni nadra kuona wanaugua. Lakini umeshawahi kujiuliza ni kwa nini? Jarbu kuangalia mazingira ya ulaji unaokuzunguka. Karibia kila kitu unachokula hakifai katika mwili wako lakini bado unakula. Wanadamu wanakula PRODUCTS Zaidi kuliko wanavyokula CHAKULA. Products ni vitu ambavyo miili yetu haiwezi kumeng`enya vinapofika tumboni. Na ndio maana mwanadamu anazungukwa na maradhi katika maisha yake. Ipo mbinu moja ya kale sana ambayo mwanadamu yoyote yule akiwa anaitumia hatakua mtu anayepata maradhi au kuugua ugonjwa wa aina yoyote ule. Mbinu hiyo si nyingine bali KUFUNGA KULA (FASTING) Unapokua umezuia mwili wako kula chakula kwa walau muda wa masaa 16 na Zaidi, mwili wako utakua katika hali ijulikanayo kama AUTOPHAGY. Yaani mwili wako hautafuni chaku...

P TATU ZA KUA NA AFYA NZURI

  P TATU ZA KUZINGATIA ILI UWE NA AFYA NZURI. Tupo katiika dunia ambayo watu wengi hupenda sana njia za mkato katika kila kitu. Na katika afya, wengi hukimbilia vidonge na dawa badala ya kubadilisha mtindo wa maisha yao ili waweze kuishi pasipo kutumia dawa ambazo mwisho wa siku zina madhara katika mwili.  Moja ya adui wakubwa ni UNENE, ni kwa sababu unene unakuanika katika kupata athari nyingi za ki afya mfano saratani, kisukari pamoja na magonjwa mengine mengi. Ila wengi hawataki kufanya hivyo wakidhani kuna vidonge vya kila tatizo wanalopata.  Dawa haziwezi kamwe kukuponya ugonjwa sugu, zitaondoa tu dalili kwa wakati huo na kukufanya uitegemee dawa hiyo katika maisha yako yote bila kupona kabisa. Utakua tu ukipata nafuu ili na kesho utumie tena na tena.  Chukulia mfano wa watu wenye vidonda vya tumbo, presha na kisukari. Kila siku watameza vidonge vitakavyowapa nafuu kwa muda mfupi, ila baadae wanarudi palepale. Maana yake ni kwamba kila siku itawabidi kut...

MAUMIVU YA KICHWA MARA KWA MARA

  MAUMIVU YA KICHWA MARA KWA MARA. Yawezekana hua unasumbuliwa au umeshaona mtu ambae hua anasumbuliwa na maumivu ya kichwa ya mara kwa mara. Na mara nyingi maumivu haya hua hayaishi hata kama ukimeza paracetamol au dawa yoyote ya kutuliza maumivu. Wengine huenda hospitali, kila vipimo wanavyofanyiwa huonyesha ya kwamba hawana shida yoyote ile. Mpaka wengine hudhania ya kwamba kuna mtu anawaloga. NI KWA NINI MAUMIVU HAYA HUTOKEA? Kisababishi kikuu hua ni upungufu wa madini ya Sodium mwilini. Kua na upungufu wa sodium kitaalam huitwa HYPONATRAEMIA. Watu wenye upungufu wa Sodium hua na shida kwenye pampu ya umeme katika seli zao ijulikanayo kama Sodium-Potassium Channel Pump. Pampu hii hutoa chaj za umeme kwa ajili ya kupeleka nguvu katika misuli na mfumo wa fahamu ili iweze kufanya kazi vizuri. Kukiwa na shida katika pampu hiyo, hutoa potassium kwa wingi sana katika seli za ubongo na hivyo kusababisha hali ya excitation katika chaneli za fahamu na matokeo yake kupata...

UZITO HUPOTEA KIUNONI NA SIO KWENYE MZANI

  UZITO/UNENE HUPOTEA KIUNONI NA SIO KWENYE MZANI. Ukitaka kutambua mwenendo wako wa kupungua uzito au unene, basi tumia kiuno chako na wala usitumie mzani. Mzani hauwezi kukupa ufanisi wa kujua uzito au unene ambao umepungua. Mzani hua unakupa tu uhakika, lakini kiuhalisia haikuonyeshi maendeleo yako kwa ufasaha. Usitumie muda mwingi sana kuangalia mzani wako unasemaje, kwa sababu mizani tofauti hua na calibration ya tofauti na pia unapopima kwa nyakati tofauti hua unapata namba tofauti. NJIA BORA YA KUJUA UZITO AU UNENE ULIOPUNGUA NI IPI? Njia bora Zaidi ni WAIST-TO-HEIGHT RATIO (WSR). Lakini pia, kuna mambo kadhaa ambayo unaweza kuangalia na kujua ya kwamba unapata matokeo mazuri. Mfano wa njia hizo ni; - ·          Kupata usingizi mzuri ambao mwanzoni hukua unaupata. ·          Kutokupata njaa mara kwa mara na kushiba mapema hata kama umekula chakula kidogo au mara moja kwa siku (impro...

FAIDA 10 UTAKAZOZIPATA UKIACHANA NA MLO WA ASUBUHI.

 FAIDA 10 UTAKAZOZIPATA UKIACHANA NA MLO WA ASUBUHI. FAIDA 10 ZA KUTOKULA ASUBUHI. 1. UTIMAMU WA AKILI/ KUMBUKUMBU NZURI Unapokula chakula cha asubuhi, unafanya domapine zako zimwagike bila sababu za msingi na hivyo kufanya uzito katika ufanyaji kazi wa ubongo wako. Watu ambao hula mlo wa asubuhi hua wanapata uvivu na ufanisi wa kazi zao kwa siku husika hua mdogo kwa sababu ubongo unakua bize kutengeneza dopamine ambayo imemwagika (dysregulated dopamine) pamoja na kusimamia umeng`enywaji wa chakula. 2. ARI YENYE NGUVU (ENERGETIC SOUL) Kila alfajiri kuanzia mida ya saa 10, mwili wako huachilia homoni zijulikanazo kama counter-regulatory hormones ambazo hukusaidia kukupa nguvu ya kuweza kupambana na siku husika. Hata kama una kazi ngumu kwa asubuhi hiyo, mwili wako unaweza kukupatia nguvu inayojitosheleza wewe kufanya shuhuli zako pasipo shida yoyote. Watu ambao hula asubuhi hupata kitu kijulikanacho kama sugar crash ambapo miili yao hua dhaifu kwa sababu inakua bize ku...

JE, MLO WA ASUBUHI (BREAKFAST) UNA FAIDA YOYOTE?

  JE, MLO WA ASUBUHI UNA FAIDA YOYOTE? MLO WA ASUBUHI HAUNA FAIDA YOYOTE KWAKO. Bila shaka umeshawahi kusikia au kuambiwa ya kwamba mlo wa asubuhi ni mlo wa muhimu kuliko mlo wowote ule. Tena ukaambiwa maneno kama vile ‘Kula mlo wa asubuhi kama mfalme, mlo wa mchana kama mtoto wa mfalme na mlo wa jioni kama ombaomba/maskini’ Je, kuna ukweli wowote kuhusiana na hili? Jibu ni HAPANA. Mlo wa asubuhi ni mlo usio na maana au faida yoyote kwako kuliko mlo wowote ule. NI KWA NINI MLO WA ASUBUHI HAUNA MAANA AU FAIDA YOYOTE KWAKO? Inapofika saa kumi alfajiri, mwili wako huachilia kiwango cha juu cha homoni aina nne.         I.             Glucagon       II.             Adrenaline     III.             Cortisol     IV.  ...

MADHARA YA PAMPERS (DIAPERS) KWA MTOTO

  MADHARA YA PAMPERS (DIAPERS) KWA WATOTO. Kwa wale ambao ni wakongwe kidogo, yaani waliozaliwa miaka ya 90 kurudi nyuma, wengi hawakuvalishwa pampers na wazazi wao, bali walivalishwa nepi au vinginevyo. Lakini miaka ya hivi karibuni na tunapoelekea, kila mtoto anavalishwa pampers kulingana na utandawazi unavyozidi. Kadiri siku zinavyozidi kwenda, ndivyo ambavyo mwanadamu anazidi kua mbali na asili yake na kuingia kwenye usasa ambao hauna chochote cha asili. Kadiri mwanadamu anavyoacha asili yake, ndivyo ambavyo matatizo ya ki afya huzidi Zaidi na Zaidi. Pampers za watoto zimetengenezwa na kemikali hatarishi ambazo huathiri afya ya mtoto ambae anakua. Kemikali hizo hufanya mambo yafuatayo; - ·          Huharibu ngozi ya mtoto na kusababisha mzio wa ngozi maeneo ya sehemu zake za siri. ·          Kemikali hizi hufyonzwa katika tishu za mwili na kusababisha shida katika kinga ya mwili wa mtoto...

MADHARA YA SODA KATIKA MWILI WAKO

  MADHARA YA SODA KATIKA MWILI WAKO. Moja ni moja kati ya vinywaji vinavyopendwa na kutumiwa sana na watu wengi. Na mbaya Zaidi, hata watoto ambao hawana hatia hupewa soda na wazazi wao kwa madai ya kuwaonyesha upendo kwa kuwaburudisha. Lakini kitu ambacho hatukifahamu ni kwamba tunajichimbia makaburi wenyewe na kujiwekea nafasi ya kuumwa magonjwa ambayo yanatesa sana baadae na kuyatibu ni gharama kubwa sana. Soda imetengenezwa na vitu vingi vyenye sumu ambavyo havina faida yoyote katika mwili wa mwanadamu, lakini mbaya Zaidi ni kwamba vina madhara makubwa ambayo hua hayatokei kwa haraka bali huja taratibu katika maisha ya mwanadamu. KEMIKALI ZILIZOPO KATIKA CHUPA YA SODA NI; - ·          Carbonated water ·          High fructose corn syrup ·          Caramel ·          Phosphoric acid ·    ...