MADHARA YA SODA KATIKA MWILI WAKO.
Moja ni moja kati ya vinywaji vinavyopendwa na kutumiwa sana
na watu wengi. Na mbaya Zaidi, hata watoto ambao hawana hatia hupewa soda na
wazazi wao kwa madai ya kuwaonyesha upendo kwa kuwaburudisha.
Lakini kitu ambacho hatukifahamu ni kwamba tunajichimbia
makaburi wenyewe na kujiwekea nafasi ya kuumwa magonjwa ambayo yanatesa sana
baadae na kuyatibu ni gharama kubwa sana.
Soda imetengenezwa na vitu vingi vyenye sumu ambavyo havina
faida yoyote katika mwili wa mwanadamu, lakini mbaya Zaidi ni kwamba vina
madhara makubwa ambayo hua hayatokei kwa haraka bali huja taratibu katika
maisha ya mwanadamu.
KEMIKALI ZILIZOPO KATIKA CHUPA YA SODA NI; -
·
Carbonated
water
·
High
fructose corn syrup
·
Caramel
·
Phosphoric
acid
·
Artificial
flavouring
·
Caffeine.
Hivyo wakati wowote ule unapokunywa chupa ya coca cola,
fikiria unaingiza vitu vyote hivyo katika mwili wako ndani ya dakika chache.
MADHARA YAKE; -
·
Kupata
ini lenye mafuta (fatty liver)
·
Kuharibika
kwa mazingira ya seli za mwili na matokeo yake kupelekea saratani.
·
Unene
na uzito uliopitiliza.
·
Magonjwa
ya tumbo (inflamed gut)
·
Madhara
makubwa ya kimetaboliki kama vile kisukari, presha na matatizo ya mifupa.
·
Ukungu
katika uwezo wa kufikiri. (unakua mzito kufanya maamuzi na kujiona mchovu
mchovu)
·
Uraibu
na kuharibika kwa dopamine katika ubongo wako.
Ukishajua madhara yote hayo, sitegemei kuona tena unafurahia
kunywa soda. Unauwzo wa kusema NAOMBA MAJI kila mara unapoulizwa UTAKUNYWA SODA
GANI? Kwani itakua ni bora Zaidi.
Na kama wewe umeshindwa kuacha soda kutokana na kudharau
kwako, basi walau usiwape watoto wako ili waweze kua na maisha marefu bila
kuteseka na magonjwa yasioambukiza.
FIT BY WAYNE.
Comments
Post a Comment