Skip to main content

Posts

Showing posts with the label kinga ya mwili

Mbinu za Kukusaidia Kua Mwanaume Rijali na Kuondokana na Upungufu wa Nguvu za Kiume

  Mbinu Zinazosaidia Kua Mwanaume Rijali na Kuondoa Upungufu Wa Nguvu Za Kiume. Upungufu wa nguvu za kiume (Erectile Dysfunction) ni hali ya kukosa uwezo wa kudumisha kusimama kwa uume wakati wa kufanya ngono. Hali hii huleta fedheha ambayo huteteresha mahusiano yaliyo mengi, husababishwa na matukio au hali ambazo huvuruga utimamu wa misuli, vhichochezi (hormones), mishipa ya fahamu pamoja na mishipa ya damu katika uume. Visababishi Vya Upungufu Wa Nguvu Za Kiume. Sababu za Kisaikolojia Sababu za kimetaboliki Sababu za mfumo wa neva za fahamu pamoja na mifupa ya misuli. 1. Sababu za Kisaikolojia Sonona/ msongo wa mawazo Unywaji wa pombe na sigara: (hudhoofisha mfumo wa neva, ubongo pamoja na mishipa ya damu kadiri mtumiaji anavyotumia) Wasiwasi Hali ya hatia Kujiona huna thamani (low self esteem) Picha ama video za ngono na punyeto: Hizi ndio mbaya zaidi kwani huleta ganzi katika sehemu zihusikazo na ladha za kimahaba katika ubongo. 2. Sababu Za Kimetaboliki Ugonjwa wa kisukari Shi...

Faida 8 Za Kutumia Majani Ya Nanaa (Mint Leaves)

  Faida Za Kutumia Majani ya Nanaa (Mint leaves). Majani ya nanaa hutumika kwa sababu mbali mbali duniani, wengi wakiwa wanatumia kama kiungo katika mapishi, dawa za meno hutumia majani haya kwa ajili ya kuleta harufu nzuri kwenye kinywa na kuzuia ukuaji wa bakteria kwenye meno na sababu nyingine nyingi. Zifuatazo ni faida zinazopatikana kwa kutumia majani ya Nanaa (mint) ki afya. Faida za Kutumia Majani ya Nanaa (Mint) 1. Hutibu Matatizo ya Tumbo Mint husaidia kutibu matatizo mbalimbali ya tumbo pamoja na kusaidia mmeng`enyo wa chakula na hivyo kuondokana na shida ya kukosa choo au kupata choo kigumu. 2. Hupandisha Kinga ya Mwili Kutokana na kua na wingi wa madini ya Phosphorus, calcium pamoja na Vitamin A,C,D na E ambazo huongeza kinga ya mwili kwa kulinda seli za mwili kutoka kwenye uharibifu. 3. Huondoa Chunusi Kwenye Ngozi Kutokana na tabia yake ya kua anti-inflammatory pamoja na anti-bacterial, majani ya nanaa husaidia kulainisha ngozi na kuondoa chunusi. Pia yana salicylic a...

Madhara 7 Yanayowapata Wanawake Wanene

  Madhara 7 Yanayowapata Wanawake Wanene. Unene au uzito uliopitiliza una madhara kwa jinsia zote mbili, wanaume na wanawake, Ingawa kwa wanawake hupata madhara makubwa zaidi ukilinganisha na wanaume. Madhara Yanayowapata Wanawake Wanene. 1. Kushindwa Kubeba Ujauzito Wanawake wanene hupata changamoto nyingi zinazoathiri kizazi kama vile Polycistic Ovarian Syndrom ijulikanayo kama PCOS, Mji wa mimba kuzungungwa na mafuta au kuvurugika kwa hedhi inayosababishwa na kuvurugika kwa homoni. 2. Kupata Shida Wakati Wa Kujifungua Wengi hupata tabu katika kusukuma mtoto au mtoto kua mkubwa (macrosomia). Hii husababishwa na uchochezi wa insulini kwa kiumbe kinachokua tumboni mwa mama kutokana na ulaji mbovu wa mama kwa muda mrefu. 3. Neuroticism (kutokua sawa kisaikolojia) Mara nyingi hawa huwa na hasira za mara kwa mara, kujiona hawana thamani, kukosa kujiamini, kua na hisia hasi wakati mwingi, kua na ugomvi n.k. Hua wanajihisi kama vile kila mtu anawaona ni wabaya kutokana na miili yao iliv...

NAMNA YA KUFANYA MAZOEZI

  Mazoezi NAMNA YA KUFANYA MAZOEZI KWA AFYA. Mazoezi ni shughuli yoyote ya mwili ambayo huongeza au kudumisha utimamu wa mwili, afya na ustawi kwa ujumla. NI KWA NINI WATU HUFANYA MAZOEZI? kusaidia ukuaji wa mwili kuboresha nguvu ya mwili kupunguza kasi ya uzee kuboresha au kukuza misuli kuboresha mfumo wa moyo na mishipa kuboresha ujuzi wa riadha kupunguza uzito/unene au kudumisha uzito sahihi kuboresha afya starehe na sababu nyinginezo ISTILAHI MUHIMU ZA KUZIJUA Kabla ya kuona jinsi ya kufanya mazoezi kadhaa, ni vyema kufahamu istilahi chache muhimu ambazo zitakuongoza katika ufanyaji mazoezi yako. Istilahi nyingine utaendelea kujifunza kadiri ynavyoendelea kubobea katika mazoezi. REP : Hiki ni kifupisho cha neno Repeatition. katika mazoezi neno hili humaanisha kurudia kitendo flani. kwa mfano: mtu akisema 10 Reps, anamaanisha kufanya hicho kitendo husika mara 10. Kwa mtu ambae anapiga push up, akienda juu na chini amemaliza mara moja. hivyo 10 reps maana yake ni push ups 10. SET...

NJIA RAHISI JINSI YA KUANZA KUPUNGUZA UNENE/KITAMBI

  NJIA RAHISI JINSI YA KUANZA KUPUNGUZA UNENE/KITAMBI. Inakadiriwa ya kwamba, katika kila familia hapa Tanzania, hapakosekani walau mtu mmoja ambae ana uziro uliopitiliza. Yaani Obese. Wapo watu kadhaa ambao wamekua wakisema ya kwamba wao wana unene wa kurithi. Kwa sababu katika familia au ukoo wao wengi ni wanene. Lakini hili halina ukweli, Ila tu ni kwamba familia nyingi zinarithishana mtindo wa maisha. Na hivyo ndio maana unaweza kuona familia flani au ukoo flani wote ni wanene. Inapokuja swala la kupunguza unene, hamna njia za mkato kama ambavyo watu wengi hupendelea. Mtu anasahau ya kwamba hakunenepa ndani ya muda mfupi, bali alinenepa kwa muda mrefu. Lakini leo hii mtu atataka kupungua haraka sana ndani ya muda mfupi. ROMA HAIKUJENGWA KWA SIKU MOJA. Njia bora zaidi ya kupunguza Unene ni kwa kuzingatia ulaji sahihi pamoja na kubadilisha mtindo wa maisha kwa ujumla. Zipo dawa zinazosaidia kurahisisha safari ya kupunguza unene, lakini ieleweke ya kwamba, dawa hizi husaidia kura...

DETOX YA SIKU 7. HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE

  HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE. Uzito Unaotakiwa kua nao Kulingana na Urefu Pamoja na Jinsia UREFU (CM) UREFU (FT & INCH) UZITO (KG)       MWANAUME MWANAMKE 147 4' 10" - 45-59 150 4' 11" - 45-60 152 5' 0" - 46-62 155 5' 1" 55-66 47-63 157 5' 2" 56-67 49-65 160 5' 3" 57-68 50-67 162 5' 4" 58-70 51-69 165 5' 5" 59-72 53-70 167 5' 6" 60-74 54-72 170 5' 7" 61-75 55-74 172 5' 8" 62-77 ...