NJIA RAHISI JINSI YA KUANZA KUPUNGUZA UNENE/KITAMBI.
Inakadiriwa ya kwamba, katika kila familia hapa Tanzania, hapakosekani walau mtu mmoja ambae ana uziro uliopitiliza. Yaani Obese.
Wapo watu kadhaa ambao wamekua wakisema ya kwamba wao wana unene wa kurithi. Kwa sababu katika familia au ukoo wao wengi ni wanene. Lakini hili halina ukweli, Ila tu ni kwamba familia nyingi zinarithishana mtindo wa maisha. Na hivyo ndio maana unaweza kuona familia flani au ukoo flani wote ni wanene.
Inapokuja swala la kupunguza unene, hamna njia za mkato kama ambavyo watu wengi hupendelea. Mtu anasahau ya kwamba hakunenepa ndani ya muda mfupi, bali alinenepa kwa muda mrefu. Lakini leo hii mtu atataka kupungua haraka sana ndani ya muda mfupi. ROMA HAIKUJENGWA KWA SIKU MOJA.
Njia bora zaidi ya kupunguza Unene ni kwa kuzingatia ulaji sahihi pamoja na kubadilisha mtindo wa maisha kwa ujumla.
Zipo dawa zinazosaidia kurahisisha safari ya kupunguza unene, lakini ieleweke ya kwamba, dawa hizi husaidia kurahisisha. lakini usipobadilisha mtindo wa kula na wa maisha, utakua huna tofauti na mtu ambaye amefua nguo nyeupe na kisha kuitupa kwenye matope.
JINSI YA KUANZA KUPUNGUZA UNENE/KITAMBI
- Anza kwa kupunguza wingi wa chakula cha wanga. (haswa wanga uliokobolewa). Kama ulikua umezoea kupakua chakula cha kiwango flani, anza kupunguza nusu sahani.
- Anza kuweka mboga nyingi za majani na matunda. (Hapa wanga uwe kiasi kama cha ngumi ya mkono wako)
- Punguza matumizi ya sukari. kama ulikua ukitumia vijiko viwili au zaidi, anza kwa kuweka kijiko kimoja pekee. (kumbuka sukari husababisha unene zaidi kuliko hata mafuta)
- Kunywa maji glasi moja walau nusu saa (dakika 30) kabla ya kula chakula. Hii itakusaidia kupata shibe mapema.
- Tumia sahani ndogo kupakua chakula chako. kwani Sahani kubwa itaudanganya ubongo wako ya kwamba chakula ni kidogo wakati ni kingi.
Kama utapendelea kupata Programu nzuri ya kuweza kupunguza Unene. Wasiliana nami kwa namba 0753068572 au Whatsapp 0621068072. au Bonyeza HAPA
Imeandikwa na SAMUEL MACHA, FIT BY WAYNE.
Comments
Post a Comment