Faida Za Kutumia Majani ya Nanaa (Mint leaves). Majani ya nanaa hutumika kwa sababu mbali mbali duniani, wengi wakiwa wanatumia kama kiungo katika mapishi, dawa za meno hutumia majani haya kwa ajili ya kuleta harufu nzuri kwenye kinywa na kuzuia ukuaji wa bakteria kwenye meno na sababu nyingine nyingi. Zifuatazo ni faida zinazopatikana kwa kutumia majani ya Nanaa (mint) ki afya. Faida za Kutumia Majani ya Nanaa (Mint) 1. Hutibu Matatizo ya Tumbo Mint husaidia kutibu matatizo mbalimbali ya tumbo pamoja na kusaidia mmeng`enyo wa chakula na hivyo kuondokana na shida ya kukosa choo au kupata choo kigumu. 2. Hupandisha Kinga ya Mwili Kutokana na kua na wingi wa madini ya Phosphorus, calcium pamoja na Vitamin A,C,D na E ambazo huongeza kinga ya mwili kwa kulinda seli za mwili kutoka kwenye uharibifu. 3. Huondoa Chunusi Kwenye Ngozi Kutokana na tabia yake ya kua anti-inflammatory pamoja na anti-bacterial, majani ya nanaa husaidia kulainisha ngozi na kuondoa chunusi. Pia yana salicylic a...
Blog hii ni kwa ajili ya kukusaidia kutatua changamoto za ki afya ambazo zinaweza kutatulika kwa kubadilisha jinsi ya kula na mtindo wa maisha