Skip to main content

Faida 8 Za Kutumia Majani Ya Nanaa (Mint Leaves)

 

Faida Za Kutumia Majani ya Nanaa (Mint leaves).

Majani ya nanaa hutumika kwa sababu mbali mbali duniani, wengi wakiwa wanatumia kama kiungo katika mapishi, dawa za meno hutumia majani haya kwa ajili ya kuleta harufu nzuri kwenye kinywa na kuzuia ukuaji wa bakteria kwenye meno na sababu nyingine nyingi.

Zifuatazo ni faida zinazopatikana kwa kutumia majani ya Nanaa (mint) ki afya.

Faida za Kutumia Majani ya Nanaa (Mint)

1. Hutibu Matatizo ya Tumbo

Mint husaidia kutibu matatizo mbalimbali ya tumbo pamoja na kusaidia mmeng`enyo wa chakula na hivyo kuondokana na shida ya kukosa choo au kupata choo kigumu.

2. Hupandisha Kinga ya Mwili

Kutokana na kua na wingi wa madini ya Phosphorus, calcium pamoja na Vitamin A,C,D na E ambazo huongeza kinga ya mwili kwa kulinda seli za mwili kutoka kwenye uharibifu.

3. Huondoa Chunusi Kwenye Ngozi

Kutokana na tabia yake ya kua anti-inflammatory pamoja na anti-bacterial, majani ya nanaa husaidia kulainisha ngozi na kuondoa chunusi. Pia yana salicylic acid ambayo husaidia kuondoa chunusi na mabaka.

4. Hondoa Ugonjwa wa Asubuhi na Kichefuchefu

Majani haya huamsha enzymes ambazo zinahusika na kumeng`enya chakula pamoja na kuondokana na kichefuchefu. Ni mazuri sana kwa wamama wajawazito ambao husumbuliwaga na ugonjwa wa asubuhi.

5. Husaidia kuondoa Mzio (Allergy) pamoja na Pumu (asthma)

Yana antioxidants zenye nguvu pamoja na anti-inflammatory ijulikanayo kama rosmarinic acid. Kazi yake ni kuzuia visababishi vya mzio katika mwili.

6. Dawa nzuri kwa Mafua na Kikohozi

Nanaa husaidia kuondoa kuziba kwa pua, mafua na kikohozi, huondoa visababishi vya mafua na kikohozi katika nyia ya pua, koo pamoja na mapafu. Pia husaidia kuondoa maumivu yatokanayo na kukohoa.

7. Hulinda Afya ya Kinywa

Ndio maana dawa nyingi za meno huwekewa Mint kwa sababu ya antibacterial property ya Mint. Huondoa harufu mbaya ya kinywa na kuua vijidudu vinavyoshambulia meno.

8. Husaidia Kutokula Vitu Vya Sukari

Umeshawahi kujiuliza ni kwa nini ukitoka kupiga mswaki unashindwa kula vitu vya sukari au unashindwa kuhisi ladha ya sukari? Nanaa ni majani ambayo yatakufanya uchukie vitu vya sukari endapo utatumia mara kwa mara.

Jinsi Ya Kutumia Majani ya Nanaa (Mint)

  • Unaweza Kutafuna majani yake kama yalivyo kwa ajili ya kukupa harufu nzuri ya kinywa
  • Unaweza kuongezea vipande vya majani ya mint katika chakula au mboga uliyopika
  • Unaweza kuloweka kwenye maji yako ya kunywa
  • Unaweza Kuongezea katika kachumbari yako
  • Unaweza kutumia katika Detox yako


Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

DETOX YA SIKU 7. HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE

  HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE. Uzito Unaotakiwa kua nao Kulingana na Urefu Pamoja na Jinsia UREFU (CM) UREFU (FT & INCH) UZITO (KG)       MWANAUME MWANAMKE 147 4' 10" - 45-59 150 4' 11" - 45-60 152 5' 0" - 46-62 155 5' 1" 55-66 47-63 157 5' 2" 56-67 49-65 160 5' 3" 57-68 50-67 162 5' 4" 58-70 51-69 165 5' 5" 59-72 53-70 167 5' 6" 60-74 54-72 170 5' 7" 61-75 55-74 172 5' 8" 62-77

Hormonal Imbalance, Visababishi na Tiba yake

  Hormonal Imbalance HORMONAL IMBALANCE    Hormonal imbalance ama kwa Kiswahili ni mvurugiko wa kichochezi (hormone). Mara nyingi huwakumba wanawake Zaidi, ingawa hata wanaume wanaweza kua na tatizo hili. na kusababisha kiwango kidogo sana au kikubwa sana cha hormone au kichochezi chochote kutokukaa sawa.  NINI HUSABABISHA HORMONAL IMBALANCE  1️⃣Ulaji Mbovu wa chakula 2️⃣Unene (uzito uliopitiliza) 3️⃣Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango.  4️⃣Stress na msongo wa mawazo 5️⃣kisukari 6️⃣Hyperglycemia (uzalishwaji wa kuzidi wa glucagon) 7️⃣Hypoglycemia (insulin kuzalishwa nyingi kuliko glucose kwenye damu) 8️⃣Saratani pamoja na vimbe kwenye via vya kizazi.  DALILI ZA HORMONAL IMBALANCE  1️⃣Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa 2️⃣Kutokushika mimba (infertility) 3️⃣Kutokua na uwezo wa kusimamisha uume 4️⃣Mbegu za uzazi kuwa chache (low sperm count) 5️⃣Uke kua mkavu (vaginal dryness) 6️⃣Kubadilika badilika kwa mzunguko wa hedhi au maumivu makali 7️⃣Kutokupata usingizi vizuri 8️⃣Kuongezeka uzito

BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI

 BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI.   💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊   BAWASIRI NI NINI?   Bawasiri (kikundu, future, puru au mjiko ) ni hali ya kutuna kwa mishipa ya damu katika mfereji wa sehemu ya haja kubwa (anus). Kuna aina mbili za Bawasiri;   1. Bawasiri za ndani ( internal haemorroids )   2. Bawasiri za nje ( external haemorroids )  Bawasiri za ndani hua na dalili ya kupata kinyesi kilichokua na damu,  bawasiri za nje hua na dalili ya maumivu makali wakati wa kujisaidia pamoja na kinyama kutoka kwa nje.  NINI VISABABISHI VYA BAWASIRI?   1️⃣Historia ya familia, mara nyingi baadhi ya familia hukumbwa na changamoto hii. Na hua watu wa familia hiyo husika wanakua na hili tatizo. 2️⃣Kupata choo kigumu mara kwa mara husababisha mtu kutumia nguvu nyingi (straining) ambayo husababisha bawasiri kutokea. 3️⃣Unene (uzito uliopitiliza) hua ni kisababishi cha bawasiri kwa sababu ya kuongezeka kwa Rectal Vein Pressure. 4️⃣Kukaa sehemu moja kwa muda mrefu au kutokufanya mazoezi. (sed