Skip to main content

CALORIE ZA VYAKULA VYA TANZANIA


 CALORIES ZA VYAKULA TANZANIA 


 NINI MAANA YA CALORIE? 


 Calorie ni kiasi cha nishati kinachohitajika ili kuongeza joto la gramu moja ya maji (°C).

Kwa lugha nyepesi, calorie katika chakula hutoa nishati (energy) kwa njia ya joto ili miili yetu iweze kufanya kazi.

Hii ni kwa sababu miili yetu huhifadhi na kuchoma calorie kama mafuta.


 UHUSIANO WA CALORIE NA UZITO WA MWILI. 

Kwa kawaida, kila chakula kina kiwango chake cha calorie. Hivyo unapokula chakula, unaingiza mwilini calorie kadhaa, na mwili wako pia unatumia calorie katika kuweka uhai.

Lakini unapokula chakula, unaingiza calorie mwilini. Na mwili wako pia unatumia calorie kama nishati. Hivyo unapokula calorie nyingi kuliko mwili unavyoweza kutumia, zinahifadhiwa kama mafuta na utaongezeka uzito.

Unapotumia calorie nyingi kuliko unavyoingiza mwilini, unapungua uzito. Na ukitumia kiasi sawa na unachoingiza, basi unabaki na uzito ule ule.


 MWANADAMU ANAHITAJI WASTANI WA CALORIE NGAPI? 

Kwa kawaida, mwanaume anahitaji Calorie 2500 ili aishi, na mwanamke anahitaji Calorie 2000 ili aishi. Maana yake ni kwamba, kama mwanaume atazidisha calorie Zaidi ya 2500 kwa siku, basi ataongezeka uzito, na pungufu ya hapo anapungua. 

Kiwango hiki hutegemeana pia na shughuli ambazo mtu husika anazifanya. Kwa mfano mtu anayefanya mazoezi sana au kufanya kazi ngumu, atahitaji calorie nyingi Zaidi kuliko mtu ambae anafanya shughuli za kawaida.


 JE, WINGI (UJAZO) WA CHAKULA HUMAANISHA CALORIE NYINGI? 

Hapana, kila chakula, tunda, kinywaji au mboga mboga zina kiwango chake.

Tazama mfano huu…

Unaweza ukala bakuli zima kubwa la mboga za majani hadi ukashiba, na ukawa umekula calorie 400 tu. 

Unaweza kula kipande kimoja cha kuku wa kukaanga, ukawa umeingiza calorie 400.

Na pia, unaweza ukatumia vijiko viwili vya mafuta ukawa umeingiza calorie 400.


Hivyo katika mifano hii, utagundua ya kwamba, ukila mboga mboga kwa wingi, utafanya tumbo lijae na kujihisi shibe, lakini ukawa umeingiza calorie kidogo, kuliko kusema ule kuku wa kukaanga hadi ushibe, itakufanya uingize calorie nyingi sana mwili kuliko mahitaji ya mwili.

Hivyo utaona ya kwamba, kwenye kupakua chakula, wanga unatakiwa uwe kiasi kidogo, lakini mboga mboga na matunda ndio viwe kwa kiwango kikubwa. (tofauti na ambavyo tumezoea ya kwamba chakula ndio kinakua kingi na mboga kua kidogo)


 KIWANGO CHA CALORIE KWA KILA GRAMU 100 ZA CHAKULA HUSIKA. 


 VYAKULA VYA WANGA 

Kitumbua 416

Chapatti 372

Ugali 123

Wali 199

Wali wa nazi (bila mafuta mengine) 170

Mkate 239

Chapatti za maji (pancake) 291

Pilau ya nyama 177

Ndizi za kupika 116

Muhogo mbichi 160

Muhogo wa kukaanga 346

Viazi vibichi 58

Viazi vitamu 103

Viazi vitamu vya kuchemsha 97

Viazi vitamu vya kukaanga 146

Mtori wa nyama 105

Mtori wa samaki 118

Ndizi nyama na nazi 130

Ndizi za kuchemsha 110

Ndizi za kukaanga 159

Ndizi za kuroast 116

Ugali wa muhogo 140

Viazi vya kuchemsha 93


 SEEDS & NUTS 

Mlozi 578

Maharagwe mekundu 166

Korosho 589

Karanga 567

Siagi ya karanga (peanut butter) 520

Sesame seed 573

Alizeti 588

Mbegu za maboga 435

Maharagwe ya soya 415

Maharagwe ya figo 117


 VYAKULA VYA NYAMA 

Nyama nyekundu 323

Nyama ya kukaangwa 813

Nyama ya mbuzi 269

Nyama ya nguruwe 537

Maini 191

Samaki 335

Samaki wa kukaangwa 230

Dagaa wabichi 84

Samaki (smoked fish) 177

Dagaa wakavu 335

Maini ya kuku 167

Kuku wa kuchemshwa 285

Kuku wa kukaangwa 315

Mchuzi wa samaki (bila samaki) 85

Maini ya kukaangwa 175

Sausage 369

Sambusa ya nyama 280

Mshkaki wa nyama 343

Kiini yai 278

Yai la kukaanga 245

Yai la kuchemsha 155

Omlette 274


 MAZIWA NA PRODUCTS ZAKE 

Chedder cheese 403

Cheese mozarrela 126

Ice cream 196

Milk powder full cream (Nido) 496

Yoghurt plain (maziwa mgando) 61


 MATUNDA 

Tofaa (apple) 52

Parachichi 160

Ndizi 89

Ubuyu 305

Tende 240

Grape fruit (madansi) 33

Embe 65

Zabibu 33

Pera 68

Fenesi 94

Ndimu/limao 29

Chungwa 42

Papai 39

Passion 43

Ukwaju 270

Nanasi 48

Chenza 53

Tikiti maji 30


 MBOGA MBOGA 

Mchicha 23

Kabichi 14

Karoti 41

Kisamvu 37

Cauliflower 12

Tango 15

Biringanya 24

Hoho 19

Majani ya maboga 19

Mchunga 10

Okra 31

Nyanya 21

Matembele 35

Kisamvu cha nazi 113

Bamia yenye mafuta 74.3


 MISCELLANEOUS 

Beer 41

Coca-cola 37

Kahawa (coffee instant) 200

Fruit flavored drink 27

Asali 304

Kahawa na maziwa bila sukari 11.5

Kahawa na sukari bila maziwa 35.4

Kahawa na maziwa na sukari 31.5

Halwa 511.7

Chai maziwa bila sukari 11

Chai na sukari 35.4

Chai maziwa na sukari 31


Kujua calorie za vyakula huweza kukusaidia kujua ni vyakula gani ule kwa wingi, na vyakula gani ule kwa kiasi. Kulingana na mahitaji yako ya mwili.


Imeandaliwa na:

 SAMUEL MACHA 

 FIT BY WAYNE 

 0621068072 (whatsapp) 

Au BONYEZA HAPA WHATSAPP

 0753068572 (mobile)



Comments

  1. Ahsantee kwa SoMo lako zurii tutalitendea kazi m natak kupungua tumbo too je hii detox siinapunguza mwili wote

    ReplyDelete
    Replies
    1. habari, detox inasaidia kupunguza mafuta yanayosababisha unene. Lakini lengo kuu la detox sio kupungua, bali kusafisha mwili na kuweza kupokea virutubisho kwa upya

      Delete
  2. Asante kwa SoMo nzuri,mungu akubariki,nahitaji kupungua tumbo tu,

    ReplyDelete
  3. Unge elekeza tule nini wenye miaka 30 na zaidi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Habari, katika masomo yangu mengi kuna vyakula kadha wa kadha ambavyo hua naviongelea kwa ajili ya matumizi. hivyo vyote vinafaa. endelea kufwatilia ukurasa huu kwa masomo mbali mbali

      Delete
  4. Nikiangalia beer, Coca-Cola, fruit flavored drink na chai na sukari vina calories ndogo sana lakini mnavipiga vita sana kwenye diet. Kwanini?

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

DETOX YA SIKU 7. HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE

  HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE. Uzito Unaotakiwa kua nao Kulingana na Urefu Pamoja na Jinsia UREFU (CM) UREFU (FT & INCH) UZITO (KG)       MWANAUME MWANAMKE 147 4' 10" - 45-59 150 4' 11" - 45-60 152 5' 0" - 46-62 155 5' 1" 55-66 47-63 157 5' 2" 56-67 49-65 160 5' 3" 57-68 50-67 162 5' 4" 58-70 51-69 165 5' 5" 59-72 53-70 167 5' 6" 60-74 54-72 170 5' 7" 61-75 55-74 172 5' 8" 62-77

Hormonal Imbalance, Visababishi na Tiba yake

  Hormonal Imbalance HORMONAL IMBALANCE    Hormonal imbalance ama kwa Kiswahili ni mvurugiko wa kichochezi (hormone). Mara nyingi huwakumba wanawake Zaidi, ingawa hata wanaume wanaweza kua na tatizo hili. na kusababisha kiwango kidogo sana au kikubwa sana cha hormone au kichochezi chochote kutokukaa sawa.  NINI HUSABABISHA HORMONAL IMBALANCE  1️⃣Ulaji Mbovu wa chakula 2️⃣Unene (uzito uliopitiliza) 3️⃣Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango.  4️⃣Stress na msongo wa mawazo 5️⃣kisukari 6️⃣Hyperglycemia (uzalishwaji wa kuzidi wa glucagon) 7️⃣Hypoglycemia (insulin kuzalishwa nyingi kuliko glucose kwenye damu) 8️⃣Saratani pamoja na vimbe kwenye via vya kizazi.  DALILI ZA HORMONAL IMBALANCE  1️⃣Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa 2️⃣Kutokushika mimba (infertility) 3️⃣Kutokua na uwezo wa kusimamisha uume 4️⃣Mbegu za uzazi kuwa chache (low sperm count) 5️⃣Uke kua mkavu (vaginal dryness) 6️⃣Kubadilika badilika kwa mzunguko wa hedhi au maumivu makali 7️⃣Kutokupata usingizi vizuri 8️⃣Kuongezeka uzito

BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI

 BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI.   💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊   BAWASIRI NI NINI?   Bawasiri (kikundu, future, puru au mjiko ) ni hali ya kutuna kwa mishipa ya damu katika mfereji wa sehemu ya haja kubwa (anus). Kuna aina mbili za Bawasiri;   1. Bawasiri za ndani ( internal haemorroids )   2. Bawasiri za nje ( external haemorroids )  Bawasiri za ndani hua na dalili ya kupata kinyesi kilichokua na damu,  bawasiri za nje hua na dalili ya maumivu makali wakati wa kujisaidia pamoja na kinyama kutoka kwa nje.  NINI VISABABISHI VYA BAWASIRI?   1️⃣Historia ya familia, mara nyingi baadhi ya familia hukumbwa na changamoto hii. Na hua watu wa familia hiyo husika wanakua na hili tatizo. 2️⃣Kupata choo kigumu mara kwa mara husababisha mtu kutumia nguvu nyingi (straining) ambayo husababisha bawasiri kutokea. 3️⃣Unene (uzito uliopitiliza) hua ni kisababishi cha bawasiri kwa sababu ya kuongezeka kwa Rectal Vein Pressure. 4️⃣Kukaa sehemu moja kwa muda mrefu au kutokufanya mazoezi. (sed