HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE.
Uzito Unaotakiwa kua nao Kulingana na Urefu Pamoja na Jinsia
UREFU (CM) |
UREFU (FT &
INCH) |
UZITO (KG) |
|
|
|
MWANAUME |
MWANAMKE |
147 |
4' 10" |
- |
45-59 |
150 |
4' 11" |
- |
45-60 |
152 |
5' 0" |
- |
46-62 |
155 |
5' 1" |
55-66 |
47-63 |
157 |
5' 2" |
56-67 |
49-65 |
160 |
5' 3" |
57-68 |
50-67 |
162 |
5' 4" |
58-70 |
51-69 |
165 |
5' 5" |
59-72 |
53-70 |
167 |
5' 6" |
60-74 |
54-72 |
170 |
5' 7" |
61-75 |
55-74 |
172 |
5' 8" |
62-77 |
57-75 |
175 |
5' 9" |
63-79 |
58-77 |
177 |
5' 10" |
64-81 |
60-78 |
180 |
5' 11" |
65-83 |
61-80 |
182 |
6' 0" |
66-85 |
- |
185 |
6' 1" |
68-87 |
- |
187 |
6' 2" |
69-89 |
- |
190 |
6' 3" |
71-91 |
- |
MAMBO YA KUFANYA KABLA YA KUANZA DETOX
- Jua kwanza uzito wako
- Weka malengo ya uzito unaotaka kuufikia
(hii itakusaidia kutokukata tamaa)
- Ondoa vitu vyote vitakavyokushawishi
kuharibu Diet yako na ujiepushe katika mazingira hayo.
- Fanya maandalizi ya vitu utakavyovihitaji
kwa kila siku, hii itakusaidia kutokua na visingizio vya kutokufwata ratiba. KUSHINDWA KUJIANDAA NI KUJIANDAA KUSHINDWA.
- Nunua Tape measure ili uwe unajipima cm za
tumbo lako kuweza kujua maendeleo yako, utakua ukifanya hivi kila siku ya 7 ya
wiki. Unaweza pia kua na mzani utakaotumia kama ukiweza.
- Chukia unene kutoka ndani ya moyo, fikiria madhara yote yanayotokana na unene na ujue kabisa umri unavyozidi kwenda una chance kubwa za kupatwa na athari hizo. Na kisha fikiria mwili wako utakavyokua endapo ukiwa na uzito sahihi
Mabadiliko Utakayokua nayo Ukiweka Nia kwa Miezi 6 |
PROGRAMU YA DETOX (D7)
Nini maana
ya Detox?
DETOX ni kifupisho cha neno DETOXIFICATION
ikiwa na maana ya mchakato au kipindi cha muda flani ambacho mtu hujizuia
kuingiza mwilini ama kuondoa dutu (substances) zenye sumu mwilini au ambazo
hazina faida kiafya.
KUNA FAIDA GANI KUFANYA DETOX?
- Kupunguza uzito uliozidi na kua na
mmeng'enyo mzuri wa chakula
- Kuongeza nguvu katika mwili. (boost
energy levels)
- Kupunguza uchochezi (inflammation)
- Kua na ngozi yenye afya
- Kuongeza kinga ya mwili
- Kuamsha ari (mood) au kua mchangamfu.
DALILI ZINAZOASHIRIA KUA MWILI UNAHITAJI DETOX
- Kuongezeka uzito
- Kua na hamu ya kula hovyo na kupenda
sana vitu vya sukari
- Kuchoka mara kwa mara
- Kutokupata usingizi wakati wa usiku
- Kupungua kwa ufanisi wa kufikiri
- Maumivu ya kichwa mara kwa mara
- Kubadilika kwa mihemko mara kwa mara
(mood swings)
- Harufu mbaya ya kinywa na maeneo
mengine
- Kukosa choo au kupata choo kigumu
- Maumivu ya misuli
- Matatizo ya ngozi (skin reactions)
JINSI YA KUANDAA DETOX
Hapa tutakua na aina 2 za detox.
Detox type 1 ambayo ni mchanganyiko wa tango, limao,
mdalasini, tangawizi pamoja na majani ya mint.
Pamoja na detox type 2, ambayo ni supu ya kabichi.
Hapa utakua na uhuru wa kutumia yoyote unayoona ni rahisi
kwako na zote ukapata matokeo mazuri.
Uamuzi ni wa kwako, kua huru kutumia aina yoyote unayopenda.
Lakini kwa wale ambao wana vidonda vya tumbo, nawashauri
kutumia Detox type 2. Kwani haina vile vitu ambavyo wagonjwa wa vidonda vya
tumbo hua wanashauriwa wasitumie.
DETOX TYPE 1.
Andaa vitu vifwatavyo;
- Tango 1 kubwa
- Limao 1 kubwa au ndimu
- Mdalasini kipande 1 kikubwa (kama ni
ya unga basi tumia kijiko 1 cha chakula)
- Tangawizi 1 kubwa, kisha iponde au
kata vipande vidogo.
- Majani ya mint kiasi cha nusu
kikombe. Au ukikosa majani ya mint tumia majani ya giligilani (kotmil kwa jina
jingine au coriander kwa kingereza). (Mint kwa kiswahili ni majani ya Nanaa)
- Maji lita 1.
JINSI YA KUTENGENEZA DETOX YAKO
- Kata tango lako katika vipande vya
mviringo au vipande vidogo kisha weka kwenye blenda yako. (usilimenye, ila
hakikisha umeosha vizuri).
- Kamulia limao/ndimu yako (usije ukasaga na maganda yake au mbegu, bali kamulia)
- Weka mdalasini, tangawizi na majani
ya mint/giligilani kwenye mchanganyiko wako.
- Saga hadi utakapopata mchanganyiko
wako ambao umelainika. (hakikisha unasaga hadi vilainike)
- Mchanganyiko utakaoupata, hifadhi
kwenye friji. (kama una friji, unaweza kutengeneza hata mchanganyiko wako wa
wiki nzima)
- Kama huna friji, hifadhi sehemu
ambayo imetulia. Ila usitengeneze ya kutumia Zaidi ya siku mbili, kwani
isipokaa kwenye friji mda mrefu inachacha.
KAMA HUNA BLENDA FANYA HIVI;
- Kata tango lako katika vipande vya
mviringo (slices) kisha weka kwenye jagi
lenye maji (usilimenye, ila hakikisha umeosha vizuri)
- Kata limao/ndimu yako katika vipande
vya mviringo (slices) na kisha uweke kwenye lile jagi lenye maji (pia usimenye,
ila hakikisha umeosha vizuri)
- Weka mdalasini, tangawizi na majani
ya mint kwenye jagi (vipimo kama nilivyoeleza awali)
- Weka sehemu iliyotulia na uhifadhi
kwa usiku mzima. Au muda usiopungua masaa 2
Ø Kisha utakapoamka asubuhi, (au baada ya masaa 2) detox yako itakua tayari kwa matumizi. Yale mabaki unaweza kuyatumia kwa kula au ukayatupa, ila usitumie yale mabaki mara ya 2, inatakiwa iwe mara moja tu.
DETOX TYPE 2
Andaa vifuatavyo;
- Kabichi nusu
- Kitunguu maji 1
- Pili pili hoho 1
- Kitunguu swaumu 1
- Nyanya 3
- Karoti 3
- Chumvi
- Pilipili manga au pilipili kiasi
(kama sio mtumiaji wa pilipili sio lazima)
- Viungo vingine vyovyote kulingana na
uhitaji.
JINSI YA KUTENGENEZA DETOX YAKO
- Likate kabichi lako katika vipande
ambayo umezoea.
- Kata kitunguu maji pamoja na pilipili
hoho.
- Ponda kifundo kimoja cha kitunguu
swaumu.
- Kata nyanya zako au ponda kulingana
na ulivyozoea. (nyanya sio lazima kutumia kama hupendelei)
- Kata karoti zako 3 katika mtindo
unaopendelea.
- Weka chumvi, pili pili manga au
pilipili, (kama hupendi pilipili sio lazima). Unaweza kuongezea na viungo
vingine ukipenda.
IPIKE HIVI
- Kaanga mboga mboga (zilizotajwa hapo
juu) pamoja na kitunguu (kabla ya kuweka kabichi na nyanya). Kaanga hadi
kitunguu kibadilike rangi lakini usiunguze
- Kisha weka kabichi na nyanya pamoja
na maji hadi vichemke na kabichi kulainika na kuiva.
- Baada ya kuiva, epua na sasa inakua
tayari kwa matumizi. Unaweza kuhifadhi kwenye chupa ya chai (thermos) ili uweze
kuhifadhi na kutumia mda wowote ule.
UNAWEZA KUIFANYA KAMA MTORI UKIPENDA;
- Kama kuna supu yoyote ile, yaweza kua
ya ng'ombe, mbuzi, samaki, kuku n.k. chukua ile supu yake na kisha ukasaga
pamoja na ile supu yako ya kabichi. Na kisha ukatumia mchanganyiko utakaopata.
- Au unaweza kuchukua supu yako ya
kabichi uliyotengeneza na kisha ukasaga kupata mtori wa supu ya kabichi na
ukatumia vizuri tu bila shida
JINSI YA KULA KATIKA SIKU 7 ZA DETOX.
Kabla ya kuelezea jinsi ya kula katika siku hizi 7. Ifahamike
ya kwamba lengo la detox sio diet. Lengo la detox ni kuandaa mwili wako ili
uweze kuingia hatika hatua ya kupungua uzito na kupokea virutubisho.
Hivyo mtindo huu wa
kula usiutumie Zaidi ya siku saba. Unatakiwa kutumika kwa siku 7 TU.
Ifahamike ya kwamba, katika siku yoyote, asubuhi kabla ya
kula chochote unaanza na glass moja ya detox type 1, au bakuli moja la detox
type 2. (ni uamuzi wako kutumia kati ya type 1 au type 2.
Hivyo kama unatumia type 1. Utakua ukitumia glass 1 asubuhi,
glass moja mchana na glass moja jioni. (hivyo utaanza na detox yako, ndipo ule
kulingana na ratiba iliyopangwa)
Na kama unatumia type 2. Utakua ukitumia bakuli 1 asubuhi,
bakuli 1 mchana na bakuli 1 jioni. (hivyo utaanza kunywa detox soup yako ndipo
ule kulingana na ratiba ya siku husika)
Vyakula hivi unaweza kupika na kuunga kwa mtindo wowote ule
ambao unapendelea. (ila jitahidi kutokutumia chumvi nyingi na mafuta mengi)
JINSI YA KULA KATIKA SIKU 7 ZA DETOX |
|
SIKU YA 1 |
Tumia matunda peke
yake (parachichi na tango). Unaweza kuchanganya kati ya Tango au Parachichi asubuhi, mchana pamoja na
jioni. Hapa utakula matunda mpaka pale utakapojihisi umeshiba. |
SIKU YA 2 |
Tumia mboga mboga
tu. Kula mpaka utakapohisi umeshiba. Utafanya hivyo asubuhi mchana na jioni.
Mfano maboga, spinachi, mchicha, matembele, bilinganya na chochote kile
ambacho kipo katika kundi la mboga mboga. |
SIKU YA 3 |
Tumia mboga mboga
pamoja na matunda mpaka utakapohisi shibe. Unaweza kuchanganya katika mtindo
wowote ule, ilimradi iwe ni mboga mboga pamoja na matunda. |
SIKU YA 4 |
Tumia matunda pamoja na mayai au maziwa ya mtindi hadi lita moja na nusu kwa siku. (usizidishe lita moja na nusu). mayai utatumia mawili kwa kila mlo. |
SIKU YA 5 |
Tumia nyama pamoja
na nyanya walau 3 hadi 5. Nyama inaweza kua ya kuchoma au kuchemsha. Ila
usizidishe Zaidi ya nusu kilo kwa siku. Nyama yaweza kua ya ng'ombe, mbuzi,
kuku, samaki n.k Kama sio mtumiaji wa nyama, unaweza kutumia vyanzo vingine vya protini kama vile mayai, maharage, njegere, mbaazi, njugumawe, choroko pamoja na kunde. |
SIKU YA 6 |
Tumia protini (nyama au mayai) pamoja na mbogamboga zozote hadi uhisi umeshiba. |
SIKU YA 7 |
Tumia wanga mzuri kama vile viazi vitamu, ugali wa dona au wa mtama, magimbi au boga. Tumia viazi vitamu 2 pamoja na mboga mboga zozote. |
NB: siku ya 1 na ya 2 zinaweza kua na
changamoto. Kwani ndio unautoa mwili wako kutoka kwenye ulaji mbaya na usiofaa
kwenda kwenye ulaji mzuri. Hivyo wakati mwili wako unafanya mabadiliko hayo,
huenda ukasikia ugumu kwa siku ya 1 na ya 2. Lakini kuanzia siku ya 3, mwili
wako utakua umezoea na utaanza kujihisi mwepesi sana.
katika kutumia matunda, kama unataka matokeo mazuri zaidi, basi tumia parachichi au tango tu. na sio matunda mengine. (hapa ni kama unataka matokeo mazuri zaidi na kama unaweza kufanya hivyo). ikiwa inashindikana, basi utatumia aina nyingine za matunda.
MAMBO YA KUZINGATIA
- Usisahau kutumia ile detox yako (type
1 au type 2) kila siku. Asubuhi mchana na jioni.
- Kunywa maji mengi kadri uwezavyo,
kwani maji yanasaidia katika kusafisha mwili.
- Kwa kua program hii ni maalum,
jitahidi usikiuke mwongozo kwa siku 7 ili uweze kupata matokeo mazuri.
- Punguza matumizi ya pombe
(ikiwezekana usitumie wakati wa D7)
- Pata usingizi wa kutosha. (angalau
masaa 8 kwa siku)
- Punguza matumizi ya sukari na vyakula
vya viwandani
- Punguza matumizi ya chumvi
- Shughulisha mwili, tembea (jambo
rahisi kabisa), fanya mazoezi, ruka Kamba, endesha baiskeli (walau nusu saa kwa
siku)
NINI KITATOKEA BAADA YA DETOX?
- Utajisikia mwepesi sana kwa sababu ya
kuweza kutoa taka mwili
- Utapungua uzito au kitambi, kama nguo
zilikua zinakubana, basi utaona zinaanza kukutosha au kupwaya. Au kama unavaa
mkanda basi utaona ni lazima uongeze tundu jingine ili uweze kukutosha.
- Utapungua wastani wa kilo 3 mpaka 7
ndani ya siku 7 (hii inategemea na mwili wa mtu. Hivyo ikitokea umepungua
chache wala usishtuke)
- Utapoteza hamu ya kula vyakula
visivyo na faida kama vile soda, vyakula vya sukari n.k
- Wakati wa detox, utaona ya kwamba
unakojoa sana. Hii ni hali ya kawaida kwani figo zako sasa zinafanya kazi kwa
ufanisi. Kitaalam kuna kitu tunaita WATER
RETENTION. Hii ni hali ambayo maji yanabaki ndani ya mwili badala ya
kutoka. Hali hii husababishwa sana na ulaji mbovu na utumiaji wa chumvi nyingi.
Hii hupelekea maji mengi kubaki mwilini badala ya kutoka. Na kama
inavyofahamika, maji hua yana uzito, hivyo yanapobaki mwilini yanachangia kwa
kiasi kikubwa kua na uzito mkubwa. Hivyo ukiona unakojoa sana, ni hali ya
kawaida.
NINI CHA KUFANYA ENDAPO UTAHISI NJAA KALI WAKATI WA DETOX
Hapa utatumia vyakula vifwatavyo ili usishinde na njaa.
Kumbuka kua detox ni kwa ajili ya kusafisha mwili wako, lakini usikubali
kushinda na njaa.
- Gimbi
- Kiazi
kitamu
- Uji wa ulezi
- Ugali
wa dona/uji wa dona
- Wali
wa brown
- Mhindi
- Uji/ugali
wa mtama
- Bagia
za dengu au kunde
- Maharage,
njegere, choroko, kunde au dengu.
Orodha hii ni vyakula vya wanga mzuri. Kama ukiona sjaandika
kitu flani, basi ujue sio rafiki kwa detox, hata kama ni wanga.
Kipimo ni cha ukubwa wa ngumi au kipimo cha bakuli 1 kwa
wanga wa kumiminikakama vile uji.
IKIWA UNANYONYESHA MTOTO ZAIDI YA MIEZI 3
Tumia vyakula hivi ili upate maziwa mengi ya kutosha kwa
mtoto huku ukiendelea na programu. Kama mtoto ana chini ya umri wa miezi 3,
nashauri usubiri kwanza atomize miez 3.
- Spinachi
- Karoti
- Papai
- Mayai
- Parachichi
- Samaki
- Boga
- Maziwa
- Vitunguu
swaumu
- Wali wa brown
- Kiazi
kitamu
ANGALIZO
- Usifanye detox hii Zaidi ya siku 7.
Kumbuka kua detox ni kwa ajili ya kuandaa mwili wako uweze kupokea virutubisho
ili uweze kupungua kwa urahisi. Ukizidisha unaweza kupata hormonal imbalance.
Baada ya siku 7, kuna mwongozo mwingine.
- Kama ni mjamzito. Hutakiwi kutumia
detox au program yoyote ya kupungua uzito. Na kama unanyonyesha, basi mtoto awe
na umri wa kuanzia miezi 3 au Zaidi.
- Kama unaumwa au upo kwenye dozi.
Nakushauri usitumie detox, ni vyema ukasubiri upone. Labda kama upo kwenye dozi
za muda mrefu mf kisukari, presha n.k ndo unaweza kutumia
NB; ENDAPO UTAZINGATIA
MWONGOZO HUU KAMA NILIVYOELEZA, NINAKUHAKIKISHIA YA KWAMBA UTAPATA MATOKEO
MAZURI MNO. NA SAFARI YAKO YA KUPUNGUA NDO ITAKUA IMEANZA SASA RASMI.
CHUKUA HATUA, UNENE SIO
MZURI HATA KIDOGO.
KARIBU KATIKA
ULIMWENGU WA AFYA
Imeandaliwa na SAMUEL MACHA, (FIT BY WAYNE)
Asanteee kw mwongoz nzuri
ReplyDeletekaribu sana
DeleteDoctor mim sjaelewa Ayo majani ya kuchanganya kwenye detox nimajan gan
DeleteAsanteee
ReplyDeletekaribu sana
DeleteNashkur umenielewesha maana nlkua najiwazia tu maana nanyonyesha.
ReplyDeletekaribu sana
DeleteÁsante sana doctor soon ndakuletea mlejesho
ReplyDeletenakutakia kila la kheri katika safari hii ya kupunguza unene na kua na afya iliyo bora
DeleteAsante sana.. naanza soon...
ReplyDeletekaribu sana
Deleteyou are warmly welcomed
ReplyDeleteAsante sana doctor
ReplyDeleteAsante Sana doctor mungu akulipe kwa haya yote
ReplyDeleteAsantee
DeleteAsante sana kwa huu mwongozo yani nimeuelewa alf nimeuelewa tena na tena, Mungu akubariki sana
ReplyDeletethanks dr
ReplyDeleteDuuu asantee Sana unene ni tatizo siku hizi
ReplyDeleteDr nilikuwa nauliza kwaiyo dotex yakwanza unakunywa vya moto au ata baridi
ReplyDelete???
Honger kwa kazi mzur swali ni kwamb nawez kuweka nazi ktka viazi au ndizi
ReplyDeleteAsante Sana kwa mwongozo mzuri
ReplyDeleteAsa
ReplyDeleteAsant sana swali langu liko iv je baada y kutumia iyo ditox kwa siku saba nini kinafuata
ReplyDeleteunafwata mwongozo mwingine ambao utaendelea nao na kukufanya uweze kupungua zaidi. ni mwongozo rahisi sana. 0621068072 whatsapp
Delete