UZURI WA VIAZI VITAMU. Viazi vitamu ni moja kati ya vyakula vya wanga bora kabisa unavyoweza kula. Hii ni kwa sababu ni Wanga Tata, (Ccomplex carbohydrates), ikiwa inamaanisha havisababishi kupanda kwa insulin na hivyo hamna kupanda kwa sukari. Glucose iliyopo ndani yake huachiliwa taratibu kwa sababu vina wingi wa nyuzinyuzi. Kama unauwezo wa kuvipanda mwenyewe na kuvuna, ni bora Zaidi. Inapendekezwa, kama unavila basi ule na maganda yake kwa ajili ya kupata faiza zake zote (kama unaweza). Viazi vitamu husaidia kuleta uwiano wa bacteria wazuri wa kwenye utumbo ambao husababisha uzalishwaji wa Butyrate. Kazi ya Butyrate ni kulinda kuta za tumbo zisitoboke na kuvuja. Kumbuka ya kwamba, glucose sio adui endapo wewe ni mwembamba na hua unashuhulisha mwili. Bali fructose (inayopatikana kwenye sukari) ndio adui yetu mkubwa. Napendekeza utumie vya kuchemshwa, weka chumvi na ufurahie mlo wako. Pia unaweza kuvianika juani, na ukatengeneza unga wake ambao ni mzuri sana. Ac...
Blog hii ni kwa ajili ya kukusaidia kutatua changamoto za ki afya ambazo zinaweza kutatulika kwa kubadilisha jinsi ya kula na mtindo wa maisha