Skip to main content

Posts

Showing posts with the label vidonda vya tumbo

P TATU ZA KUA NA AFYA NZURI

  P TATU ZA KUZINGATIA ILI UWE NA AFYA NZURI. Tupo katiika dunia ambayo watu wengi hupenda sana njia za mkato katika kila kitu. Na katika afya, wengi hukimbilia vidonge na dawa badala ya kubadilisha mtindo wa maisha yao ili waweze kuishi pasipo kutumia dawa ambazo mwisho wa siku zina madhara katika mwili.  Moja ya adui wakubwa ni UNENE, ni kwa sababu unene unakuanika katika kupata athari nyingi za ki afya mfano saratani, kisukari pamoja na magonjwa mengine mengi. Ila wengi hawataki kufanya hivyo wakidhani kuna vidonge vya kila tatizo wanalopata.  Dawa haziwezi kamwe kukuponya ugonjwa sugu, zitaondoa tu dalili kwa wakati huo na kukufanya uitegemee dawa hiyo katika maisha yako yote bila kupona kabisa. Utakua tu ukipata nafuu ili na kesho utumie tena na tena.  Chukulia mfano wa watu wenye vidonda vya tumbo, presha na kisukari. Kila siku watameza vidonge vitakavyowapa nafuu kwa muda mfupi, ila baadae wanarudi palepale. Maana yake ni kwamba kila siku itawabidi kut...

Vidonda Vya Tumbo: Jinsi ya Kukabiliana na Kuvitibu.

  Jinsi Ya Kukabiliana Na Kutibu Vidonda Vya Tumbo Vidonda vya tumbo hutokea pale ambapo sehemu ya kuta za kwenye umio (Oesophagus),  tumbo au Utumbo kua na kidonda. Na hii hutokea baada ya kuharibika kwa Ute (mucus) ambao hulinda kuta hizo. Unaweza kusoma zaidi kuhusiana na Vidonda Vya Tumbo na dalili zake kwa kubofya  HAPA Watu wengi hudhania ya kwamba bacteria anaefahamika kwa jina la H-pylori ni adui. Bacteria huyu sio adui yako, kwa sababu unaishi nae tangu siku unayozaliwa. Ila tu huleta shida pale ambapo tunakula lishe mbivu pamoja na mtindo mbaya wa maisha. Ni Kwa Nini Vidonda Vya Tumbo Hutokea? Matumizi ya pombe Matumizi ya Nafaka (wanga) zilizokobolewa Matumizi ya viungo vya kiwandani kama vile Royco Matumizi ya Mafuta ya Mbegu (vegetable oils) mfano mafuta ya alizeti Matumizi ya dawa za maumivu kama vile diclofenac na bufren Matumizi mabaya ya dawa za antibiotics Uvutaji wa sigara Kutokupata usingizi wa kutosha Kulakula hovyo au kila wakati (huvuruga uwiano wa ...

VIDONDA VYA TUMBO (ULCERS)

 NINI CHA KUFANYA KAMA UNA VIDONDA VYA TUMBO (ULCERS) Peptic Ulcer VIDONDA VYA TUMBO NI NINI? Vidonda vya tumbo ni tatizo linalotokea pale ambapo kuta za tumbo kua na vidonda. Hii hutokea baada ya kuharibika kwa ute (mucus) ambao hulinda kuta za tumbo. Ute huu huharibiwa na acid ambayo hua inamwagika tumboni kwa lengo la kuyeyusha chakula na kuua vijidudu visivyotakiwa kwenye chakula.  AINA ZA VIDONDA VYA TUMBO. 1 .Vidonda vya kwenye Tumbo (Gastric ulcers) : Hivi hutokea ndani ya tumbo. Gastric/stomach ulcers 2. Vidonda vya kwenye Utumbo (Duodenal Ulcers): Hivi hutokea kwenye utumbo. Duodenal Ulcer NINI HUSABABISHA VIDONDA VYA TUMBO? Bakteria waitwao Helicobacter Pylori (H.pylori) Matumizi ya mara kwa mara ya dawa za maumivu kama vile Aspirin na NSAIDs nyingine. Uvutaji wa sigara Kua na msongo wa mawazo Unywaji mkubwa wa pombe Saratani ya tumbo Visababishi vingine kama vile kukaa muda mrefu bila kula chakula. NI DALILI ZIPI ZA VIDONDA VYA TUMBO? Maumivu makali ya tumbo (kama...