P TATU ZA KUZINGATIA ILI UWE NA AFYA NZURI.
Tupo katiika dunia ambayo watu wengi hupenda sana njia za mkato katika kila kitu. Na katika afya, wengi hukimbilia vidonge na dawa badala ya kubadilisha mtindo wa maisha yao ili waweze kuishi pasipo kutumia dawa ambazo mwisho wa siku zina madhara katika mwili.
Moja ya adui wakubwa ni UNENE, ni kwa sababu unene unakuanika katika kupata athari nyingi za ki afya mfano saratani, kisukari pamoja na magonjwa mengine mengi. Ila wengi hawataki kufanya hivyo wakidhani kuna vidonge vya kila tatizo wanalopata.
Dawa haziwezi kamwe kukuponya ugonjwa sugu, zitaondoa tu
dalili kwa wakati huo na kukufanya uitegemee dawa hiyo katika maisha yako yote
bila kupona kabisa. Utakua tu ukipata nafuu ili na kesho utumie tena na tena.
Chukulia mfano wa watu wenye vidonda vya tumbo, presha na
kisukari. Kila siku watameza vidonge vitakavyowapa nafuu kwa muda mfupi, ila
baadae wanarudi palepale. Maana yake ni kwamba kila siku itawabidi kutumia dawa
hizo. Au wengine dawa zao ni lazima wameze kila mwezi. Sasa ni kwa nini
usibadilishe mtindo wako wa maisha ili upone moja kwa moja? Hii ni aina
nyingine ya utumwa.
Suluhisho la kuondokana na magonjwa yasioambukiza (chronic
inflammatory diseases) ni kubadilisha mtindo mbaya wa maisha na kua mzuri na ulaji
sahihi.
Hapa ni lazima tutumie P tatu za kua na afya Nzuri.
1.
Proper
diet (mlo sahihi)
2.
Physical
activity (kushuhulisha mwili ni lazima)
3.
Purposeful
rest (lazima uwe na muda wa kupumzika)
1. PROPER DIET. Maana yake inajibu swali la WHAT TO EAT?
Kabla ya kula au kunywa chochote, ni lazima ujiulize maswali
haya muhimu,
·
KINA FAIDA GANI? Ni lazima ujiulize kama hicho
chakula au kinywaji kina virutubisho vinavyofaa kujenga mwili wako au ni sum
utu ambazo zinaharibu mwili wako.
· NILE SAA NGAPI? Ni lazima ujue na kutambua muda sahihi wa kula. Kwa sababu unapokula muda sahihi huharibu mfumo wa mwili ujulikanao kama circadian rhythm.
·
KWA NINI NAKULA? Ni lazima ujiulize kama ni kweli
unanjaa au unakula tu kwa sababu ya ulafi.
Utakapoijali na kuitunza afya yako leo, na yenyewe itakuja
kukutunza na kukujali katika siku za usoni.
Comments
Post a Comment