Skip to main content

BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI


 BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI.
 

πŸ’ŠπŸ’ŠπŸ’ŠπŸ’ŠπŸ’ŠπŸ’ŠπŸ’ŠπŸ’ŠπŸ’ŠπŸ’ŠπŸ’ŠπŸ’ŠπŸ’Š


 BAWASIRI NI NINI? 


Bawasiri (kikundu, future, puru au mjiko) ni hali ya kutuna kwa mishipa ya damu katika mfereji wa sehemu ya haja kubwa (anus).


Kuna aina mbili za Bawasiri; 

 1. Bawasiri za ndani (internal haemorroids

 2. Bawasiri za nje (external haemorroids


Bawasiri za ndani hua na dalili ya kupata kinyesi kilichokua na damu, 

bawasiri za nje hua na dalili ya maumivu makali wakati wa kujisaidia pamoja na kinyama kutoka kwa nje.


 NINI VISABABISHI VYA BAWASIRI? 


1️⃣Historia ya familia, mara nyingi baadhi ya familia hukumbwa na changamoto hii. Na hua watu wa familia hiyo husika wanakua na hili tatizo.


2️⃣Kupata choo kigumu mara kwa mara husababisha mtu kutumia nguvu nyingi (straining) ambayo husababisha bawasiri kutokea.


3️⃣Unene (uzito uliopitiliza) hua ni kisababishi cha bawasiri kwa sababu ya kuongezeka kwa Rectal Vein Pressure.


4️⃣Kukaa sehemu moja kwa muda mrefu au kutokufanya mazoezi. (sedentary lifestyle)


5️⃣Lishe kukosa nyuzi nyuzi (fiber), matumizi ya vyakula visivyo na fiber za kutosha huchangia kutokea kwa bawasiri.


6️⃣Mimba (ujauzito) huweza kusababisha kwa sabau ya kuongezeka kwa intra-abdominal pressure.


 NINI DALILI ZA BAWASIRI? 


1️⃣Kupata choo chenye rangi nyekundu au damu wakati wa kujisaidia (hii hua ni dalili ya kwanza kabisa, na katika hatua hii hua hamna maumivu)


2️⃣Kinyama kutoka nje baada ya kujisaidia na kurudi chenyewe ndani (ila hatua za baadae, kinaweza kutoka na kisirudi hadi urudishe kwa kidole)


 TIBA ZA ASILI ZINAZOSAIDIA KUTIBU BAWASIRI


πŸ₯¬πŸ₯¬πŸ₯¬πŸ₯¬πŸ₯¬πŸ₯¬πŸ₯¬πŸ₯¬πŸ₯¬πŸ₯¬πŸ₯¬πŸ₯¬πŸ₯¬


1️⃣ HABAT SAUDA  (Black seed powder) 


Kijiko kimoja kikubwa cha unga wa Habat sauda, 

koroga kwenye glass moja ya maji na kisha uwe unakunywa mara mbili kwa siku. Kwa muda wa wiki 2 hadi mwezi mmoja. (inategemea na ukubwa wa tatizo.)


2️⃣ MSHUBIRI (ALOE VERA) 


Kipande cha aloe vera, kikate kisha tumia ule ute wake na upake sehemu ya utupu yako wa nyuma kila mara baada ya kuoga.


3️⃣ HABAT SAUDA NA ASALI 


Changanya kijiko cha chai kimoja cha habit sauda pamoja na nusu lita ya asali. Lamba kijiko kimoja kikubwa kutwa mara tatu. 

Kisha kunywa maji glass moja baada ya kunywa dawa yako.


4️⃣ JUISI YA LIMAO/NDIMU NA ASALI 


Chukua asali nusu lita 


malimao yapatayo 12 na uzikate kwa nusu. 

Chemsha maji lita 3 huku ukiweka zile limao zichemke na maji hadi ziive. Baada ya juisi kupoa, zikamue zile limao na kisha uchuje kupata juisi yako


changanya ile asali nusu lita na juisi yako ya limao, 

ongezea maji safi hadi upate ujazo wa lita 5. hifadhi katika friji. (kama huna friji tengeneza kidogo kidogo ili isije ikachacha, walau ya kutumia siku 3)

ongezea vijiko vitatu vya mdalasini wa unga.

kunywa glass moja kutwa mara 2 kwa  kwa wiki 2 au Zaidi (kulingana na ukubwa wa tatizo)


5️⃣ APPLE CIDER VINEGAR (SIKI YA TUFAA) 


Kama ni bawasiri ya ndani, chukua kijiko kimoja cha Apple cider vinegar na uchanganye na glass 1 ya maji na unywe kutwa mara 2.


Kama ni bawasiri ya nje, chukua pamba ambayo ni safi na uchovye kwenye Apple cider vinegar na kisha ujipake kwenye tupu yako ya nyuma (sehemu iliyoathirika). [unaweza kusikia maumivu, ila jipake kidogo kidogo, yataisha kadri muda unavyokwenda].


 Kisha uwe unakunywa glass 1 kutwa mara 2 (kama ilivyoelekezwa kwenye bawasiri ya ndani)


6️⃣ MAFUTA YA NYONYO (CASTOR OIL) 


Paka mafuta ya nyonyo sehemu yako ya utupu wa nyuma kutwa mara 2 kwa muda wa wiki 3 hadi 4 (kulingana na ukubwa wa tatizo). 




 Katika njia zikizotanjwa hapo juu. Sio lazima utumie zote. Zipo njia 6 ambazo unaweza kuchagua 1 hadi 3 kati ya hizo. Ambayo unaona kwako ni rahisi


 (Au kama utapenda dawa ambayo ni tayari kwa matumizi. Fwata maelekezo mwishoni mwa ujumbe huu) 


Au bonyeza hapa NAHITAJI TIBA YA BAWASIRI




 ZINGATIA YAFUATAYO 


1️⃣Kunywa maji mengi Zaidi ya unayokunywa kila siku kwa matokeo mazuri, kusafisha mwili na kuepuka kufunga kwa choo.


2️⃣Kula mboga za majani na matunda katika kila mlo.


3️⃣Kula vyakula vyenye fiber nyingi (punguza sana matumizi ya wanga uliokobolewa)


4️⃣Epuka kufanya mapenzi kinyume na maumbile (kwa wale wanaofanya)


Kwa msaada Zaidi na kupata Tiba juu ya ugonjwa wa bawasiri, 

Tuwasiliane kwa namba 0621068072 (whatsapp), 0676068572 (mobile), 0753068572 (mobile)



Angalizo, bonyeza hiyo link tu kama unahitaji msaada zaidi juu ya Tiba ya Bawasiri.

Comments

Popular posts from this blog

DETOX YA SIKU 7. HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE

  HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE. Uzito Unaotakiwa kua nao Kulingana na Urefu Pamoja na Jinsia UREFU (CM) UREFU (FT & INCH) UZITO (KG)       MWANAUME MWANAMKE 147 4' 10" - 45-59 150 4' 11" - 45-60 152 5' 0" - 46-62 155 5' 1" 55-66 47-63 157 5' 2" 56-67 49-65 160 5' 3" 57-68 50-67 162 5' 4" 58-70 51-69 165 5' 5" 59-72 53-70 167 5' 6" 60-74 54-72 170 5' 7" 61-75 55-74 172 5' 8" 62-77 ...

CALORIE ZA VYAKULA VYA TANZANIA

 CALORIES ZA VYAKULA TANZANIA   NINI MAANA YA CALORIE?    Calorie ni kiasi cha nishati kinachohitajika ili kuongeza joto la gramu moja ya maji (Β°C). Kwa lugha nyepesi, calorie katika chakula hutoa nishati (energy) kwa njia ya joto ili miili yetu iweze kufanya kazi. Hii ni kwa sababu miili yetu huhifadhi na kuchoma calorie kama mafuta.  UHUSIANO WA CALORIE NA UZITO WA MWILI.  Kwa kawaida, kila chakula kina kiwango chake cha calorie. Hivyo unapokula chakula, unaingiza mwilini calorie kadhaa, na mwili wako pia unatumia calorie katika kuweka uhai. Lakini unapokula chakula, unaingiza calorie mwilini. Na mwili wako pia unatumia calorie kama nishati. Hivyo unapokula calorie nyingi kuliko mwili unavyoweza kutumia, zinahifadhiwa kama mafuta na utaongezeka uzito. Unapotumia calorie nyingi kuliko unavyoingiza mwilini, unapungua uzito. Na ukitumia kiasi sawa na unachoingiza, basi unabaki na uzito ule ule.   MWANADAMU ANAHITAJI WASTANI WA CALORIE NGAPI? ...