Skip to main content

Posts

Showing posts with the label ulcers

Vidonda Vya Tumbo: Jinsi ya Kukabiliana na Kuvitibu.

  Jinsi Ya Kukabiliana Na Kutibu Vidonda Vya Tumbo Vidonda vya tumbo hutokea pale ambapo sehemu ya kuta za kwenye umio (Oesophagus),  tumbo au Utumbo kua na kidonda. Na hii hutokea baada ya kuharibika kwa Ute (mucus) ambao hulinda kuta hizo. Unaweza kusoma zaidi kuhusiana na Vidonda Vya Tumbo na dalili zake kwa kubofya  HAPA Watu wengi hudhania ya kwamba bacteria anaefahamika kwa jina la H-pylori ni adui. Bacteria huyu sio adui yako, kwa sababu unaishi nae tangu siku unayozaliwa. Ila tu huleta shida pale ambapo tunakula lishe mbivu pamoja na mtindo mbaya wa maisha. Ni Kwa Nini Vidonda Vya Tumbo Hutokea? Matumizi ya pombe Matumizi ya Nafaka (wanga) zilizokobolewa Matumizi ya viungo vya kiwandani kama vile Royco Matumizi ya Mafuta ya Mbegu (vegetable oils) mfano mafuta ya alizeti Matumizi ya dawa za maumivu kama vile diclofenac na bufren Matumizi mabaya ya dawa za antibiotics Uvutaji wa sigara Kutokupata usingizi wa kutosha Kulakula hovyo au kila wakati (huvuruga uwiano wa ...

VIDONDA VYA TUMBO (ULCERS)

 NINI CHA KUFANYA KAMA UNA VIDONDA VYA TUMBO (ULCERS) Peptic Ulcer VIDONDA VYA TUMBO NI NINI? Vidonda vya tumbo ni tatizo linalotokea pale ambapo kuta za tumbo kua na vidonda. Hii hutokea baada ya kuharibika kwa ute (mucus) ambao hulinda kuta za tumbo. Ute huu huharibiwa na acid ambayo hua inamwagika tumboni kwa lengo la kuyeyusha chakula na kuua vijidudu visivyotakiwa kwenye chakula.  AINA ZA VIDONDA VYA TUMBO. 1 .Vidonda vya kwenye Tumbo (Gastric ulcers) : Hivi hutokea ndani ya tumbo. Gastric/stomach ulcers 2. Vidonda vya kwenye Utumbo (Duodenal Ulcers): Hivi hutokea kwenye utumbo. Duodenal Ulcer NINI HUSABABISHA VIDONDA VYA TUMBO? Bakteria waitwao Helicobacter Pylori (H.pylori) Matumizi ya mara kwa mara ya dawa za maumivu kama vile Aspirin na NSAIDs nyingine. Uvutaji wa sigara Kua na msongo wa mawazo Unywaji mkubwa wa pombe Saratani ya tumbo Visababishi vingine kama vile kukaa muda mrefu bila kula chakula. NI DALILI ZIPI ZA VIDONDA VYA TUMBO? Maumivu makali ya tumbo (kama...