Jinsi Ya Kukabiliana Na Kutibu Vidonda Vya Tumbo
Vidonda vya tumbo hutokea pale ambapo sehemu ya kuta za kwenye umio (Oesophagus), tumbo au Utumbo kua na kidonda. Na hii hutokea baada ya kuharibika kwa Ute (mucus) ambao hulinda kuta hizo.
Unaweza kusoma zaidi kuhusiana na Vidonda Vya Tumbo na dalili zake kwa kubofya HAPA
Watu wengi hudhania ya kwamba bacteria anaefahamika kwa jina la H-pylori ni adui. Bacteria huyu sio adui yako, kwa sababu unaishi nae tangu siku unayozaliwa. Ila tu huleta shida pale ambapo tunakula lishe mbivu pamoja na mtindo mbaya wa maisha.
Ni Kwa Nini Vidonda Vya Tumbo Hutokea?
- Matumizi ya pombe
- Matumizi ya Nafaka (wanga) zilizokobolewa
- Matumizi ya viungo vya kiwandani kama vile Royco
- Matumizi ya Mafuta ya Mbegu (vegetable oils) mfano mafuta ya alizeti
- Matumizi ya dawa za maumivu kama vile diclofenac na bufren
- Matumizi mabaya ya dawa za antibiotics
- Uvutaji wa sigara
- Kutokupata usingizi wa kutosha
- Kulakula hovyo au kila wakati (huvuruga uwiano wa uzalishwaji wa Hydrochloric acid tumboni)
- Unene au Uzito uliozidi
- Dawa za usingizi au za msongo wa mawazo (sonona), pamoja na dawa za presha
Nini Cha Kufanya Endapo Una Vidonda Vya Tumbo?
1. Kua Na Tabia ya Kufunga Kula
Mtindo wa 20:4 ni mwanzo mzuri katika tiba ya vidonda vya tumbo. 20:4 ni mtindo ambao unamaanisha ya kwamba utafunga kwa masaa 20 na utakula kwa masaa 4. (Kujua zaidi kuhusiana na jinsi ya Kufunga Bonyeza HAPA)
Unapofunga, utaruhusu kuta zilizochubuka kujitibu na kurudi katika hali yake ya kawaida. (regeneration)
Mkusanyiko wa Tindikali (acid concentration) hushuka na kua katika pH scale ya 1-3, na hivyo hufanya bacteria wa H-pylori asiwe adui, kuondoa bacteria hatarishi pamoja na kupona kwa oesophageal valve ambayo huzuia kucheua kwa gastric juice (juisi ya tumbo)
Kufunga kutasaidia pia uponyaji wa kibofu cha mkojo na hivyo kuzalishwa kwa Bile salts, na mwishowe kusaidia kuweka uwiano wa bacteria wazuri kwenye matumbo. (balance of gut bacteria)
2. Tumia Juice Ya Kabichi
Juisi ya Kabichi |
Hii inatumika kama unashida yoyote ile kwenye tumbo au utumbo kama vile Vidonda vya tumbo, Ugonjwa wa Tumbo (gastritis), Diverticulitis, Gastroesophageal Reflux Disease (GERD) nakadhalika.
Kabichi ina glutamine ambayo husaidia kuponya Inflammation ya kwenye utumbo.
Mahitaji:
- Kabichi ambayo ni fresh
- Tango au Broccoli au vyote kwa pamoja
- Karoti
- Nazi
- Chumvi
Jinsi ya Kuandaa:
- Katakata kabichi yako, karoti pamoja na Tango au broccoli katika vipande vidogo vidogo
- Weka kwenye blender na kisha usage kwa dakika moja
- Chukua sehemu nyeupe ya nazi yako na uweke kwenye blender
- Ongezea na Maji ya nazi yako pamoja na chumvi katika mchanganyiko wako.
- Saga kwa dakika 2 au 3.
Matumizi:
Kunywa Juisi yako (mchanganyiko utakaoupata) muda ambao utakua unafungua au katika mlo wako wa kwanza wa siku. Na iwe masaa 3 au 4 kabla ya kwenda kulala.
(Kumbuka Utakua ukitumia mfumo wa kufunga wa 20:4, Hivyo Mlo wako wa mwisho unatakiwa uwe saa mbili usiku, na mlo wako wa kufungua utakua ni saa 10 jioni kesho yake. Na hapo utakua umefunga kwa masaa 20.)
Reference:
FIT BY WAYNE
Hongera sana kaka kwa makala hii safi. Mungu akujalie na uendelee na moyo yako wa kutetea afya ya jamii.
ReplyDeleteAmen, nashukuru sana
DeleteBarkiwa sana
ReplyDeleteAmen. Ubarikiwe pia
DeleteAsante Sana kwa SoMo nzuri limenisaidia
ReplyDelete