Skip to main content

Posts

Showing posts with the label mfungo

Mbinu za Kukusaidia Kua Mwanaume Rijali na Kuondokana na Upungufu wa Nguvu za Kiume

  Mbinu Zinazosaidia Kua Mwanaume Rijali na Kuondoa Upungufu Wa Nguvu Za Kiume. Upungufu wa nguvu za kiume (Erectile Dysfunction) ni hali ya kukosa uwezo wa kudumisha kusimama kwa uume wakati wa kufanya ngono. Hali hii huleta fedheha ambayo huteteresha mahusiano yaliyo mengi, husababishwa na matukio au hali ambazo huvuruga utimamu wa misuli, vhichochezi (hormones), mishipa ya fahamu pamoja na mishipa ya damu katika uume. Visababishi Vya Upungufu Wa Nguvu Za Kiume. Sababu za Kisaikolojia Sababu za kimetaboliki Sababu za mfumo wa neva za fahamu pamoja na mifupa ya misuli. 1. Sababu za Kisaikolojia Sonona/ msongo wa mawazo Unywaji wa pombe na sigara: (hudhoofisha mfumo wa neva, ubongo pamoja na mishipa ya damu kadiri mtumiaji anavyotumia) Wasiwasi Hali ya hatia Kujiona huna thamani (low self esteem) Picha ama video za ngono na punyeto: Hizi ndio mbaya zaidi kwani huleta ganzi katika sehemu zihusikazo na ladha za kimahaba katika ubongo. 2. Sababu Za Kimetaboliki Ugonjwa wa kisukari Shi...

Umuhimu Wa Kufunga Kula na Jinsi ya Kufunga Ipasavyo

  Kufunga Kula Kuna Faida Gani? Kufunga kula kulianza tangu enzi za kale. Hata wanadamu walioshi miaka mingi iliyopita walifunga kwa sababu mbali mbali. Hivi ni nani ambae alisema ya kwamba mwanadamu anatakiwa kula mara tatu kwa siku? Umeshawahi kujiuliza swali hilo? Je, kuna sababu za msingi zinazomfanya mwanadamu ale mara tatu kwa siku, na kuna faida gani endapo atakula pungufu ya hapo? Wagiriki wa kale waliamini ya kwamba kufunga huongeza uwezo wa utambuzi (cognitive ability). Wanafalsafa wengi waliamini ya kwamba kufunga kula ni moja wapo ya tiba katika mwili. Hippocrates ambae ni Baba wa Tiba (father of medicine) aliwaagiza wagonjwa wake wafunge kula ikiwa njia ya kwanza ya tiba kwao kabla ya kuwapa dawa yoyote ile. Hippocrates alisema " To eat when you are sick is to feed your illness" ikiwa na maana ya kwamba " kula chakula wakati ni mgonjwa ni sawa na kuulisha ugonjwa" Mwanafalsafa aitwaye Plutarch pia alisema " Instead of using medicine, better fast...