Skip to main content

Posts

Showing posts with the label tumbo

JE, MAJI YA MOTO HUSAIDIA KUPUNGUZA KITAMBI?

  JE, MAJI YA MOTO HUSAIDIA KUPUNGUZA KITAMBI? Bila shaka umeshawahi kuona watu ambao hunywa maji ya moto na limao kila asubuhi huku wakisema ya kwamba wanafanya hivyo ili kupunguza kitambi. Cha ajabu ni kwamba watu hawa wanafanya hivi lakini hawafanyi mabadiliko yoyote juu ya vyakula wanavyokula au mtindo wa maisha. Kwa kifupi ni kwamba, ukiona mtu anasema anakunywa maji ya moto kwa lengo la kupunguza kitambi, ujue ni mvivu wa kubadilisha mtindo wake wa maisha na anapenda njia za mkato. Ila ukweli ni kwamba, katika kupunguza unene na kuondokana na kitambi, hua hamna njia za mkato. UKWELI KUHUSU MAJI YA MOTO Maji ya moto hayayeyushi mafuta kama wengi wanavyodhani. Na pia hayana mchango wowote katika kuyeyusha mafuta yanayosababisha unene mwilini mwa mwanadamu. Tindikali ya Hydrocloric tumboni ndio husaidia katika kumeng`enya chakula, lakini sio maji ya moto. Mtu anayekunywa maji ya moto na anayekunywa maji ya baridi, wote wanakunywa maji. Na hamna kitu cha ziada kinac...

Vidonda Vya Tumbo: Jinsi ya Kukabiliana na Kuvitibu.

  Jinsi Ya Kukabiliana Na Kutibu Vidonda Vya Tumbo Vidonda vya tumbo hutokea pale ambapo sehemu ya kuta za kwenye umio (Oesophagus),  tumbo au Utumbo kua na kidonda. Na hii hutokea baada ya kuharibika kwa Ute (mucus) ambao hulinda kuta hizo. Unaweza kusoma zaidi kuhusiana na Vidonda Vya Tumbo na dalili zake kwa kubofya  HAPA Watu wengi hudhania ya kwamba bacteria anaefahamika kwa jina la H-pylori ni adui. Bacteria huyu sio adui yako, kwa sababu unaishi nae tangu siku unayozaliwa. Ila tu huleta shida pale ambapo tunakula lishe mbivu pamoja na mtindo mbaya wa maisha. Ni Kwa Nini Vidonda Vya Tumbo Hutokea? Matumizi ya pombe Matumizi ya Nafaka (wanga) zilizokobolewa Matumizi ya viungo vya kiwandani kama vile Royco Matumizi ya Mafuta ya Mbegu (vegetable oils) mfano mafuta ya alizeti Matumizi ya dawa za maumivu kama vile diclofenac na bufren Matumizi mabaya ya dawa za antibiotics Uvutaji wa sigara Kutokupata usingizi wa kutosha Kulakula hovyo au kila wakati (huvuruga uwiano wa ...