Skip to main content

Posts

Showing posts with the label maumivu

USITUMIE DAWA ZA MAUMIVU AU ANTIBIOTIKI PASIPO SABABU ZA MSINGI

  USITUMIE DAWA ZA MAUMIVU PASIPO SABABU ZA MSINGI. Mara nyingi dawa hua hazitibu au kuondoa tatizo, bali zinatuliza dalili ambazo zinatokana na tatizo husika. Dawa za antibiotic hua zina ufanisi kwa sababu hua zinaenda kuangamiza vimelea vinavyosababisha ugonjwa, ila shida yake ni moja, hua zinaangamiza pia bacteria wazuri ambao wapo ndani ya mwili wako. Ndio maana ni busara sana kama umetoka kutumia dawa za antibiotic kwa ajili ya matibabu, uwe unatumia vyakula vichachu (fermented foods), mfano maziwa ya mtindi ili kuweza kurudisha uwiano wa bacteria wazuri katika tumbo. Usitumie antibiotic, dawa za maumivu au antacids kwa Zaidi ya siku 5 mfululizo. Kwani utaangamiza bacteria wako wazuri katika tumbo, ambao ndio wanaosaidia kuweka mwili wako sawa. Ni vyema kujua haswa chanzo cha tatizo ni nini, badala ya kukimbilia kumeza dawa. Usiwe mtumwa wa madawa. Kila dawa unayomeza inakuachia sumu mwilini mwako. Kumbuka ya kwamba CHEMBE NA CHEMBE MKATE HUWA . Na SAMUEL MACHA F...