USITUMIE DAWA ZA MAUMIVU PASIPO SABABU ZA MSINGI.
Mara nyingi dawa hua hazitibu au kuondoa tatizo, bali
zinatuliza dalili ambazo zinatokana na tatizo husika.
Dawa za antibiotic hua zina ufanisi kwa sababu hua zinaenda
kuangamiza vimelea vinavyosababisha ugonjwa, ila shida yake ni moja, hua
zinaangamiza pia bacteria wazuri ambao wapo ndani ya mwili wako.
Ndio maana ni busara sana kama umetoka kutumia dawa za
antibiotic kwa ajili ya matibabu, uwe unatumia vyakula vichachu (fermented
foods), mfano maziwa ya mtindi ili kuweza kurudisha uwiano wa bacteria wazuri
katika tumbo.
Usitumie antibiotic, dawa za maumivu au antacids kwa Zaidi ya
siku 5 mfululizo. Kwani utaangamiza bacteria wako wazuri katika tumbo, ambao
ndio wanaosaidia kuweka mwili wako sawa.
Ni vyema kujua haswa chanzo cha tatizo ni nini, badala ya
kukimbilia kumeza dawa. Usiwe mtumwa wa madawa. Kila dawa unayomeza inakuachia
sumu mwilini mwako. Kumbuka ya kwamba CHEMBE NA CHEMBE MKATE HUWA.
Na SAMUEL MACHA
FIT BY WAYNE
Reference:
Comments
Post a Comment