JE, MAJI YA MOTO HUSAIDIA KUPUNGUZA KITAMBI?
Bila shaka umeshawahi
kuona watu ambao hunywa maji ya moto na limao kila asubuhi huku wakisema ya
kwamba wanafanya hivyo ili kupunguza kitambi.
Cha ajabu ni kwamba watu
hawa wanafanya hivi lakini hawafanyi mabadiliko yoyote juu ya vyakula
wanavyokula au mtindo wa maisha.
Kwa kifupi ni kwamba,
ukiona mtu anasema anakunywa maji ya moto kwa lengo la kupunguza kitambi, ujue
ni mvivu wa kubadilisha mtindo wake wa maisha na anapenda njia za mkato. Ila ukweli
ni kwamba, katika kupunguza unene na kuondokana na kitambi, hua hamna njia za
mkato.
UKWELI KUHUSU MAJI YA MOTO
Maji ya moto hayayeyushi
mafuta kama wengi wanavyodhani. Na pia hayana mchango wowote katika kuyeyusha
mafuta yanayosababisha unene mwilini mwa mwanadamu.
Tindikali ya Hydrocloric
tumboni ndio husaidia katika kumeng`enya chakula, lakini sio maji ya moto.
Mtu anayekunywa maji ya
moto na anayekunywa maji ya baridi, wote wanakunywa maji. Na hamna kitu cha
ziada kinachowatofautisha.
Mdomo wa mwanadamu
utapooza maji ili yawe katika joto linalotakiwa kabla ya kumeza. Ndio maana
hakuna mtu anayeweza kumeza maji ya moto sana au yabaridi sana. Ni lazima
atayachezesha mdomoni kwa sekunde kadhaa ili kuyafanya yawe na joto
linalotakiwa kabla ya kumeza.
Wengine hudhania ya
kwamba kwa sababu wanatoka jasho wanapokunywa maji ya moto, basi ndio
wanapoteza mafuta ya unene. Ukweli ni kwamba, unatokwa na jasho kwa sababu
mwili wako unajipooza. Hii ni kutokana na mfumo wa kibaiolojia ujulikanao kama
HOMEOSTASIS.
Maji ya moto hayana
kirutubisho chochote wala calorie ya aina yoyote. Hayana amino acids, ni maji
tu ya kawaida kama ilivyo maji ya baridi.
Hivyo hamna ukweli wowote
kama maji ya moto yanapunguza kitambi. Mafuta ya unene hayayeyuki kwa moto kama
wengi wanavyodhani.
Na FIT BY WAYNE
www.amerix.ke.com (Reference)
Comments
Post a Comment