Skip to main content

Umuhimu Wa Kufunga Kula na Jinsi ya Kufunga Ipasavyo

 

Kufunga Kula Kuna Faida Gani?

Kufunga kula kulianza tangu enzi za kale. Hata wanadamu walioshi miaka mingi iliyopita walifunga kwa sababu mbali mbali.

Hivi ni nani ambae alisema ya kwamba mwanadamu anatakiwa kula mara tatu kwa siku? Umeshawahi kujiuliza swali hilo? Je, kuna sababu za msingi zinazomfanya mwanadamu ale mara tatu kwa siku, na kuna faida gani endapo atakula pungufu ya hapo?

Wagiriki wa kale waliamini ya kwamba kufunga huongeza uwezo wa utambuzi (cognitive ability). Wanafalsafa wengi waliamini ya kwamba kufunga kula ni moja wapo ya tiba katika mwili.

Hippocrates ambae ni Baba wa Tiba (father of medicine) aliwaagiza wagonjwa wake wafunge kula ikiwa njia ya kwanza ya tiba kwao kabla ya kuwapa dawa yoyote ile. Hippocrates alisema " To eat when you are sick is to feed your illness" ikiwa na maana ya kwamba " kula chakula wakati ni mgonjwa ni sawa na kuulisha ugonjwa"

Mwanafalsafa aitwaye Plutarch pia alisema " Instead of using medicine, better fast today" ikiwa na maana ya kwamba, " Kuliko kutumia dawa, ni heri ufunge kula leo"

Wagiriki waliamini ya kwamba ili kupata matibabu mazuri, ni vyema kuangalia na kuchunguza asili ya mazingira. Haswa kutazama wanyama, kwani mwanadamu naye ni mnyama.

Kwa mfano kama mbwa au paka akiumwa, hua wanakaa mbali na chakula. Mwili wa mwanadamu huhisi kichefuchefu, hutapika, huharisha au kupoteza hamu ya kula kwa sababu mwili hujiandaa wenyewe kwa ajili ya kujiponya.

Kufunga kula ni daktari wetu wa kwanza ambae yupo ndani yetu.

Ni Kwa Nini Watu Hufunga Kula?

1. Kwa sababu za kiroho/kidini

Mtu hujitenga na uchafu wote wa kimwili au wakidunia na kutafakari kwa kina mambo ya kiroho ili awe karibu na Mungu wake.

2. Kwa sababu za Kiafya/Kitabibu

Kwa mfano kabla ya kwenda kufanyiwa upasuaji, madaktari humshauri mtu aache kula kwa muda fulani ili kuzuia Kucheua wakati wa kufanyiwa upasuaji.

3. Kwa sababu za kisiasa

Baadhi ya wanasiasa hufunga ili waweze kua na mawazo yaliyotulia.

4. Kwa sababu za Lishe

Kwa mfano kupunguza unene, kuzuia tabia ya kula hovyo pamoja na kua na mtindo wenye adabu wa kula.

Tofauti Kati Ya Kufunga Na Kushinda Njaa

Kufunga Kula: Ni maamuzi ya ufahamu wa mtu ya kukaa mbali na chakula kwa wakati maalum na muda maalum.

Kushinda na Njaa: Haihusishi ufahamu wa mtu kwa kupenda, ikiwa na maana ya kwamba kama chakula kikiwepo kitaliwa.

Faida Za Kitabibu na Kilishe Za Kufunga Kula

  • Kurekebisha Kisukari aina ya pili, unapofunga kula unadhibiti Homoni ya Insulin pamoja na kiwango cha sukari kwenye damu.
  • Udhibiti wa kisukari aina ya pili hupelekea kuzuia Shinikizo la juu la damu (hypertension), magonjwa ya moyo, kiharusi (stroke) pamoja na saratani.
  • kuondoa sumu mwilini (detoxification), seli za mwili hujitafuna ili kuharibu dutu zisizofaa
  • kufunga kula hupunguza gharama ambazo ungetumia kwa milo mitatu kwani sio lazima kula mara tatu kwa siku.
  • kufunga kula husaidia kuokoa muda na kufanya mambo mengine muhimu kuliko kuandaa chakula au kupika na kula.

Jinsi Ya Kufunga Kula

  1. Mfungo wa Kawaida: kuanzia saa 12 jioni hadi saa 12 alfajiri (wakati wa usiku unapokua umelala
  2. Mfungo wa aina ya Ramadhani: Kuanzia saa 12 alfajiri hadi saa 12 Jioni
  3. Mfungo wa muda maalum (Time Restricted fasting): ni mtindo wa kugawanya masaa 24 katika mtindo wa 16:8 (kufunga masaa 16 na kula masaa 8), 20:4 (kufunga masaa 20 na kula 4), 18:6, pamoja na 22:2 [Kikubwa ni kwamba mgawanyo utimie masaa 24]
  4. Mfungo wa Mlo Mmoja kwa siku (OMAD/One Meal a Day)
  5. Mfungo wa kupokezana kwa siku: kwa mfano kuchagua siku za kufunga katika wiki kama vile jumanne na alhamisi kila wiki.

Ni Nani Anapaswa Kufunga Kula Na Nani Hapaswi?

Wasiopaswa Kufunga

  1. Watoto chini ya umri wa miaka 9
  2. Wamama wajawazito
  3. Wamama wanaonyonyesha
  4. Watu wenye uzito mdogo kupita kiasi (BMI chini ya 18.5)

Kundi tajwa hapo juu hawapaswi kufunga kwa sababu wanahitaji virutubisho endelevu.

Wanaopaswa Kufunga

Mtu mwingine yeyote anaweza kufunga.

Ni Nini Hutokea Pale Unapofunga Kula?

  • Huhusisha mabadiliko katika seli zako za mwili ambazo huathiri metabolism ya mwili
  • Mwanzoni kiwango cha glucose kwenye damu hutegemea hifadhi ya glycogen kwenye Ini pamoja na misuli
  • Unapofunga kula, glycogen zaidi huondolewa kutoka kwenye ini na baada ya saa 24 mwili huanza kutumia vyanzo vingine ambavyo vimehifadhi mafuta. Mwili huchukua mafuta hayo na kuyatumia kama nishati katika mchakato ujulikanao kama Ketosis.
  • Hapa ndipo mwili huanza kutumia mafuta kama chanzo cha nishati.
  • Kuzoea kufunga kula kunaweza kuchukua muda na unaweza kuhisi athari kama vile njaa kali, kukaza kwa misuli, kuwashwa na hata wakati mwingine kichwa kuuma. Hii yote hutokea kwa sababu mwili unatupa dutu hatarishi na zilizojaa sukari ambazo hazitakiwi tena.
  • Mwili utaanza kuzoea kadiri muda unavyozidi kwenda.
  • Katika kipindi cha kufunga kula, haswa wakati wa asubuhi, watu huwa na kiwango kikubwa cha glucose kwenye damu. Ni kutokana na hali ijulikanayo kama Dawn Phenomenon 
  • Dawn phenomenon huletwa na kitu kinachofahamika kama Circardian Rthythm ambayo ni saa ya kibaiolojia. ndio ambayo inadhibiti jinsi homoni zinavyofanya kazi kwa siku nzima

Kabla ya kuamka (majira ya saa kumi alfajiri), mwili huwa na kiwango kikubwa cha adrenaline, growth hormone, glucagon pamoja na cortisol kwa ajili ya kuandaa mwili kukabiliana na siku husika.

Adrenaline kwa ajili ya kuupa mwili nguvu, growth hormone kwa ajili ya kutengeneza na kurekebisha protini mpya, glucagon kwa ajili ya kusafirisha glucose kutoka sehemu ilipohifadhiwa kwenda kwenye damu ili itumike kama nishati, Cortisol (stress hormone) kwa ajili ya kuandaa mwili kwa kazi mbalimbali.

Hii ndio sababu kwa nini ukipima sukari asubuhi utakuta ipo kwa kiwango cha juu kuliko wakati mwingine.

Maana yake ni kwamba, huna haja ya kula chakula wakati wa asubuhi kwa sababu tayari una nguvu ya kutosha. Hivyo dhana ya kwamba Chakula cha asubuhi ni cha muhimu kuliko vyote, haina ukweli wowote wala faida yoyote katika mwili. 

Jinsi Ya Kuanza Kufunga Kula

Hatua ya kwanza, acha kabisa kula vyakula vidogo vidogo (snacks) katikati ya milo mikubwa. Kisha baada ya muda, usitumie kifungua kinywa (mlo wa asubuhi). Mlo wako wa kwanza wa siku unatakiwa kua mchana (haswa saa 6 mchana)

Mlo wako wa mwisho (chakula cha jioni) kinatakiwa kiwe saa 2 usiku. Itakua ni mfungo wa 16:8. kwa maana ya kwamba mlo wako mwingine utakua kesho yake saa 6 mchana. [hapa utakua umefunga kwa masaa 16 na kula kwa masaa 8]

Endelea na mtindo huu kwa wiki 1 au 2 ili kutoa muda kwa mwili wako kuzoea. Baada ya mwili kuzoea unaweza kwenda 18:6 ikiwa na maana utafunga kwa masaa 18 na kula kwa masaa 6.

Endelea kuongeza hadi 20:4, 22:2 lakini ukiwa unausikiliza mwili wako kama unaweza kumudu. Ila jitahidi walau kila baada ya wiki 1 au 2 ndipo uongeze.

Baada ya mwili kuzoea, sasa unaweza kutumia Mfungo wa OMAD (One Meal a Day). Hapa ni mlo mmoja kwa siku.

Mwili ukishazoea mlo mmoja kwa siku, ingia sasa katika mtindo wa Alternate fasting (kupokezana kwa siku). Utachagua siku kadhaa katika wiki ambazo ndio utakua unafunga.

Jambo la Kuzingatia

Ni lazima uwe na lengo la kufunga. usikurupuke tu na kuamua kufunga kula, ni lazima ujue ni kwa nini unafunga na uwe na lengo. Lengo litakusaidia kuchagua mtindo wa kufunga.

Maisha ya kufunga yanatakiwa yawe tabia yako, usiwe mtu ambae mara anafanya na mara hafanyi. Kuliko kufanya hivi, ni afadhali usifunge ukajua moja. Kwani hutapata faida ya kufunga. 

Tengeneza au chagua mtindo ambao ni wa kuaminika na rahisi kua endelevu.

Zingatia mazingira uliyonayo na kisha chagua mtindo ambao utaendana na mazingira ambayo unayo ili iwe rahisi kua na tabia ya kufunga.

Mambo Unayopaswa Kufanya Na Usiyopaswa Kufanya Wakati Wa Kufunga kula.

Mambo ya Kufanya

Kunywa maji ya kutosha (Rehydrate), kwa sababu mwili huondoa glycogen kutoka kwenye Ini na hutumia maji kufanya hivyo. Ndio maana katika wiki ya kwanza mtu hupungua uzito (ila ni uzito wa maji), lakini baada uzito hurudi sehemu yake.

Unaweza kunywa maji yenye chumvi (saline water), maji haya hutengenezwa kwa kuweka maji ya vuguvugu kwenye glasi na kisha ukaweka chumvi kiasi kidogo sana kwa sababu mwili utahitaji Sodium pamoja na Chloride.

Unaweza pia kutumia Apple Cide Vinegar (siki ya tufaa), hii itasaidia kuondoa hamu ya kula na njaa kali, pamoja na kichwa kuuma. Weka vijiko 2 vya chakula kwenye glasi ya maji ya vuguvugu na unywe asubuhi. (Hakikisha unatumia ORGANIC Apple Cider Vinegar).

Unaweza kunywa kahawa lakini usiweke sukari, itasaidia kupandisha metabolism na kupunguza njaa kali. lakini usinywe zaidi ya saa 7 mchana ili usije ukapata shida kupata usingizi usiku.

Unaweza kunywa green tea kwa sababu ina viondosha sumu (antioxidants) vya kutosha, hivi husaidia kuondoa free radicals. (free radicals ndizo ambazo husababisha kubadilika kwa DNA ya Mitochondria kusababisha magonjwa ya kimetaboliki kama vile saratani, kisukari na kadhalika.

Unaweza pia kunywa chai ya rangi bila sukari.

Mambo Usiopaswa Kufanya

Usinywe kitu chochote chenye calorie kama vile maji ya limao/ndimu, asali, matunda, juisi, soda, pombe n.k Utakapokunywa utakua umeharibu mfungo wako kwa sababu lengo ni mwili kutumia mafuta yaliyohifadhiwa mwilini kwa ajili ya nishati. Unapokunywa au kula kitu chenye calorie, mwili utaacha kutumia mafuta na kuanza kutumia calorie ambazo umeingiza mwilini.

Faida Za Kufunga

  • Huondoa hatari ya kupata magonjwa ya kimetaboliki kama vile kupunguza kiwango cha lehemu, kushusha presha ya juu, kuongeza Insulin sensitivity ili kudhibiti sukari na kufanya kua na metabolism nzuri.
  • Huimarisha afya ya Ubongo na Akili kwani unakua na utulivu mkubwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi
  • Huimarisha mchakato wa seli kupitia autophagy ambapo seli hatarishi hujitafuna.
  • Husaidia kuweka sawa kiwango cha homoni na kazi zake
  • Husaidia kuondoa mafuta yasiokua na faida mwilini.
  • Ni tiba ya magonjwa mengi. (unapokua na tatizo lolote la ki afya, jaribu kufunga)
Kumbuka ya kwamba, mtindo huu wa kufunga, utafunga kula tu, lakini utakunywa maji pamoja na vinywaji vilivyotajwa. kasoro tu kama ni Mtindo wa Kufunga aina ya Ramadhan.

Reference:

Diabetic Code by Dr. Jason Fung

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

DETOX YA SIKU 7. HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE

  HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE. Uzito Unaotakiwa kua nao Kulingana na Urefu Pamoja na Jinsia UREFU (CM) UREFU (FT & INCH) UZITO (KG)       MWANAUME MWANAMKE 147 4' 10" - 45-59 150 4' 11" - 45-60 152 5' 0" - 46-62 155 5' 1" 55-66 47-63 157 5' 2" 56-67 49-65 160 5' 3" 57-68 50-67 162 5' 4" 58-70 51-69 165 5' 5" 59-72 53-70 167 5' 6" 60-74 54-72 170 5' 7" 61-75 55-74 172 5' 8" 62-77

Hormonal Imbalance, Visababishi na Tiba yake

  Hormonal Imbalance HORMONAL IMBALANCE    Hormonal imbalance ama kwa Kiswahili ni mvurugiko wa kichochezi (hormone). Mara nyingi huwakumba wanawake Zaidi, ingawa hata wanaume wanaweza kua na tatizo hili. na kusababisha kiwango kidogo sana au kikubwa sana cha hormone au kichochezi chochote kutokukaa sawa.  NINI HUSABABISHA HORMONAL IMBALANCE  1️⃣Ulaji Mbovu wa chakula 2️⃣Unene (uzito uliopitiliza) 3️⃣Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango.  4️⃣Stress na msongo wa mawazo 5️⃣kisukari 6️⃣Hyperglycemia (uzalishwaji wa kuzidi wa glucagon) 7️⃣Hypoglycemia (insulin kuzalishwa nyingi kuliko glucose kwenye damu) 8️⃣Saratani pamoja na vimbe kwenye via vya kizazi.  DALILI ZA HORMONAL IMBALANCE  1️⃣Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa 2️⃣Kutokushika mimba (infertility) 3️⃣Kutokua na uwezo wa kusimamisha uume 4️⃣Mbegu za uzazi kuwa chache (low sperm count) 5️⃣Uke kua mkavu (vaginal dryness) 6️⃣Kubadilika badilika kwa mzunguko wa hedhi au maumivu makali 7️⃣Kutokupata usingizi vizuri 8️⃣Kuongezeka uzito

BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI

 BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI.   💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊   BAWASIRI NI NINI?   Bawasiri (kikundu, future, puru au mjiko ) ni hali ya kutuna kwa mishipa ya damu katika mfereji wa sehemu ya haja kubwa (anus). Kuna aina mbili za Bawasiri;   1. Bawasiri za ndani ( internal haemorroids )   2. Bawasiri za nje ( external haemorroids )  Bawasiri za ndani hua na dalili ya kupata kinyesi kilichokua na damu,  bawasiri za nje hua na dalili ya maumivu makali wakati wa kujisaidia pamoja na kinyama kutoka kwa nje.  NINI VISABABISHI VYA BAWASIRI?   1️⃣Historia ya familia, mara nyingi baadhi ya familia hukumbwa na changamoto hii. Na hua watu wa familia hiyo husika wanakua na hili tatizo. 2️⃣Kupata choo kigumu mara kwa mara husababisha mtu kutumia nguvu nyingi (straining) ambayo husababisha bawasiri kutokea. 3️⃣Unene (uzito uliopitiliza) hua ni kisababishi cha bawasiri kwa sababu ya kuongezeka kwa Rectal Vein Pressure. 4️⃣Kukaa sehemu moja kwa muda mrefu au kutokufanya mazoezi. (sed