Mbinu Zinazosaidia Kua Mwanaume Rijali na Kuondoa Upungufu Wa Nguvu Za Kiume.
Upungufu wa nguvu za kiume (Erectile Dysfunction) ni hali ya kukosa uwezo wa kudumisha kusimama kwa uume wakati wa kufanya ngono.
Hali hii huleta fedheha ambayo huteteresha mahusiano yaliyo mengi, husababishwa na matukio au hali ambazo huvuruga utimamu wa misuli, vhichochezi (hormones), mishipa ya fahamu pamoja na mishipa ya damu katika uume.
Visababishi Vya Upungufu Wa Nguvu Za Kiume.
- Sababu za Kisaikolojia
- Sababu za kimetaboliki
- Sababu za mfumo wa neva za fahamu pamoja na mifupa ya misuli.
1. Sababu za Kisaikolojia
- Sonona/ msongo wa mawazo
- Unywaji wa pombe na sigara: (hudhoofisha mfumo wa neva, ubongo pamoja na mishipa ya damu kadiri mtumiaji anavyotumia)
- Wasiwasi
- Hali ya hatia
- Kujiona huna thamani (low self esteem)
- Picha ama video za ngono na punyeto: Hizi ndio mbaya zaidi kwani huleta ganzi katika sehemu zihusikazo na ladha za kimahaba katika ubongo.
2. Sababu Za Kimetaboliki
- Ugonjwa wa kisukari
- Shinikizo la juu la damu (High blood pressure/Hypertension)
- Magonjwa ya tezi
- Unene/uzito uliozidi.
3. Sababu Za Mifupa na Misuli
- Unene/uzito uliozidi
- Udhaifu wa misuli kama vile dystrophy
- Magonjwa ya damu kama vile sickle cell
- Magonjwa ya mishipa ya fahamu
- Magonjwa mengineyo kama vile ngiri (hernia)
Dalili Za Upungufu Wa Nguvu Za Kiume
Kila mara unapojiandaa kwa ajili ya Tendo, unashindwa kudumisha kusimama kwa uume kwa lengo la tendo.
Kukosa kusimamisha uume mara tatu kwa siku pasipo kufanya au kufikiria jambo lolote lihusikanalo na ngono. kwa kawaida Mwanaume anatakiwa kusimamisha Uume wake mara tatu kwa siku, Asubuhi anapoamka, mida ya nyakati za mchana pamoja na Jioni. Na hii inatakiwa iwe inatokea akiwa hafikirii chochote kuhusiana na ngono.
Ni kutokana na mfumo wa kibaiolojia ujulikanao kama Circardian Rhythm
Ili Kupona Shida Ya Upungufu wa Nguvu Za Kiume
- Kubali kwanza kama unatatizo, mshirikishe mwenza wako, usiogope, wewe ni mwanaume. wewe sio wa kwanza wala hutakua wa mwisho kua na tatizo hilo.
- Hakikisha unatambua kisababishi kilichopelekea tatizo hilo na utatue
- Acha kabisa matumizi ya pombe na sigara
- Punguza unene kama unao.
- Tibu magonjwa ya kimetaboliki kama unayo
Tiba Bora Zaidi Dhidi ya Upungufu Wa Nguvu Za Kiume.
- Kula mlo safi (clean diet), ikiwa na maana ya kwamba usitumie kabisa sukari na vitu vya sukari.
- Fanya mazoezi aina ya Strength Training au kunyanyua vitu vizito; itakupatia stamina, kupandisha kiwango chako cha homoni ya Testosterone pamoja na kuongeza uhai wa tendo la ngono.
- Siku zote kua na mawazo chanya kama mwanaume.
- Kunywa maji mengi ya kutosha kila siku
- Usikose protini na mboga za majani katika mlo wako; protini huchochea uzalishwaji wa homoni ya testosterone pamoja na nyingine zihusikazo na afya ya uzazi.
- Tembea juani haswa nyakati za asubuhi; utapata Vitamin D
- Lala kwa walau masaa 7 kwa siku, itakuongezea urijali wako.
- Oga maji ya baridi kila siku (usioge maji ya moto kama ni mwanaume)
Zingatia:
- Usinunue dawa za kuongeza nguvu za kiume, hamna itakayokusaidia, badilisha mtindo wako wa maisha na utapona.
- kupona huchukua muda, hivyo kua na subira. ROMA HAIKUJENGWA WA SIKU MOJA
- Unahitaji uthubutu, uthabiti na uvumilivu.
Vyakula Ambavyo Kila Mwanaume Anapaswa Kuepuka.
- Sukari (kama una watoto wa kiume waepushe na vitu vya sukari, ili waanze kua rijali mapema)
- Unga wa ngano
- Unga wa mahindi
- Mafuta yatokanayo na mbegu (vegetable oils and seed oils)
- Maziwa ya kiwandani
- Energy drinks
- Rangi ya chakula kama vile ubuyu, juice cola n.k
Uhusiano wa Homoni ya Testosterone, Urijali na Nguvu za Kiume.
Testosterone ni homoni ya kiume inayotengenezwa ndani ya korodani.
Ni kichocheo muhimu sana katika afya ya uzazi wa mwanaume pamoja na urijali wake. Ndio homoni inayohusika na Nguvu, tamaa ya makuu (ambition), motisha, hamu ya tendo la ndoa pamoja na furaha.
kwa kifupi ndio homoni inayompa mwanaume tabia za kiume endapo ipo katika kiwango sahihi.
Nini Hutokea Endapo Testosterone Ikiwa Pungufu?
- Kukosa hamu ya tendo la ndoa
- Upungufu wa nguvu za kiume
- uchovu na kutokua na nguvu
- Sonona
Vyakula Vinavyosababisha Kushuka kwa Testosterone
- Sukari (kama una watoto wa kiume waepushe na vitu vya sukari, ili waanze kua rijali mapema)
- Unga wa ngano
- Unga wa mahindi
- Mafuta yatokanayo na mbegu (vegetable oils and seed oils)
- Maziwa ya kiwandani
- Energy drinks
- Rangi ya chakula kama vile ubuyu, juice cola n.k
- Beer
Ni Kwa nini Mwanaume Anapaswa Kutokutumia Beer?
- Man Boobs (kua na matiti)
- Unene
- Hisia za kike (feminin emotions)
- Kuongezeka kwa makalio na hips
- Kupungua kwa hamu ya tendo
- Upungufu wa nguvu za kiume na kuwahi kumwaga.
- Ini lenye mafuta (Fatty liver)
Jinsi ya Kupandisha Kiwango cha Testosterone (kiwe na uwiano unaotakiwa)
- Usitumie kabisa sukari au vitu vya sukari
- Aacha kuangalia picha na video za ngono
- Acha kupiga punyeto
- Fanya tendo na mwanamke badala ya kuangalia porn na kujichua.
- Fanya mazoezi ya kunyanyua uzito au aina ya HIIT
- Tembea juani haswa nyakati za asubuhi
- Lala kwa walau saa 8 au 7 kwa siku
- Oga maji ya Baridi
- kula nyama (isiwe imekaangwa/deep fried) na shahamu (fats) nzuri kama vile zeituni, nazi, parachichi, korosho, karanga, mlozi pamoja na mboga za majani haswa jamii ya kabichi kama vile kabichi, broccoli, cauliflower.
- kua na tabia ya kumsifia mwanamke ambaye unadhani ni mzuri au anavutia. maneno kama Umependeza, wewe ni mzuri n.k: haimaanishi kwamba unataka kufanya nae ngono, hisia za ngono unaweza kufanya (transmute) kitu chanya.
- Kua na tabia ya kufunga kula mara kwa mara. Wiki isiishe bila kufunga kula. unaweza kjifunza zaidi katika link hii JINSI YA KUFUNGA KULA
- Tumia supu haswa ya kongoro au kichwa mara kwa mara: hua ina protini za kutosha na shahamu muhimu kwa ajili ya urijali.
- Acha pombe kwani inaharibu uwiano wa testosterone.
- Tumia boga mara kwa mara: lina wingi wa Vitamin A, Vitamin C, Vitamin K, madini ya Zince na Shaba ambazo ni muhimu sana kwa urijali.
Jinsi Ambavyo Kuoga Maji Baridi Husaidia Kuongeza Kiwango Cha Testosterone
Mwanaume anapoogea maji ya baridi huamsha T-receptor cells ambazo hupelekea msukumo wa homoni ya testosterone kutoka kwenye gonads na kukuweka katika hali ya kukabiliana na jambo (Beast mode).
Beast Mode huchochea silika zako za awali (primal insticts). na Testosteron ndio homoni ijulikanayo kama beast mode hormone.
Comments
Post a Comment