NINI CHA KUFANYA KAMA UNA VIDONDA VYA TUMBO (ULCERS)
Peptic Ulcer |
VIDONDA VYA TUMBO NI NINI?
Vidonda vya tumbo ni tatizo linalotokea pale ambapo kuta za tumbo kua na vidonda. Hii hutokea baada ya kuharibika kwa ute (mucus) ambao hulinda kuta za tumbo. Ute huu huharibiwa na acid ambayo hua inamwagika tumboni kwa lengo la kuyeyusha chakula na kuua vijidudu visivyotakiwa kwenye chakula.
AINA ZA VIDONDA VYA TUMBO.
1.Vidonda vya kwenye Tumbo (Gastric ulcers): Hivi hutokea ndani ya tumbo.
|
2.Vidonda vya kwenye Utumbo (Duodenal Ulcers): Hivi hutokea kwenye utumbo.
Duodenal Ulcer |
NINI HUSABABISHA VIDONDA VYA TUMBO?
- Bakteria waitwao Helicobacter Pylori (H.pylori)
- Matumizi ya mara kwa mara ya dawa za maumivu kama vile Aspirin na NSAIDs nyingine.
- Uvutaji wa sigara
- Kua na msongo wa mawazo
- Unywaji mkubwa wa pombe
- Saratani ya tumbo
- Visababishi vingine kama vile kukaa muda mrefu bila kula chakula.
NI DALILI ZIPI ZA VIDONDA VYA TUMBO?
- Maumivu makali ya tumbo (kama kuunguza) mara baada ya kula au mda mwingine kabla.
- kiungulia
- kichefuchefu au kutapika (hali ikiwa mbaya zaidi unatapika damu)
- Tumbo kujaa gesi
- Kupata choo cheusi au chenye damu na harufu mbaya (hali ikiwa mbaya)
- Kutokupata hamu ya kula na kupungua uzito
NINI CHA KUFANYA KAMA UNA VIDONDA VYA TUMBO.
- Acha kutumia vyakula ambayo havifai kwa vidonda vya tumbo: Kwa kawaida, kuna tofauti baina ya mtu na mtu katika vyakula vinavyosumbua vidonda. ila ni vyema kuepuka vyakula vyenye caffein kama vile kahawa. epuka kula chocolate, pombe, pilipili pamoja na vyakula vinavyotengenezwa kutumia nyanya.
- Usile chakula usiku mwngi sana: kwa sababu ukila utafanya tumbo liachilie acid kwa ajili ya digestion wakati umelala.
- Punguza vyakula vyenye mafuta na maziwa: vyakula hivi husababisha tumbo kuchelewa kuondoa chakula na matokeo yake acidi kumwagika kwa wingi. Maziwa huondoa maumivu kwa muda, ila baada ya muda husababisha acid imwagike nyingi zaidi tumboni.
- Punguza matumizi ya viungo vikali: hivi husababisha acid kumwagika kwa wingi (increased gastric secretions). mfano pilipili, kitunguu swaumu, karafuu n.k
- Kula vyakula vyenye madini ya chuma: kwa sababu kama una vidonda ambavyo vinakusababishia kutoka damu kwa ndani, utapata kitu tunaita Irone deficiency Anemia. Hivyo tumia sana nyama ambayo haina mafuta, kuku au bata, mkate wa brown (epuka sana mkate mweupe. tumia wa brown ambao ngano yake haijakobolewa)
- Tumia maziwa ya mtindi: mara nyingi yana bacteria wanaofahamika kama live lactobacilli pamoja na bifidobacteria, hua wanapunguza kuumwa kwa vidonda hivi tumboni.
- Kunywa juice ya alovera ukiweza: nusu kikombe mara tatu kwa siku husaidia.
UKIACHILIA MBALI KWENYE MLO, EPUKA VITU HIVI...
- Usivute sigara: husababisha vidonda visipone na pia hufanya viwe vinajirudia kila wakati.
- Usitumie dawa za maumivu bila kupata ushauri wa mtu wa afya.
- Fanya mazoezi mara kwa mara ili kufanya Endorphin ipande: endorphine husaidia kuondoa maumivu mwilini. Hii ni kemikali ya kwenye ubongo
VYAKULA HATARISHI KWA VIDONDA VYA TUMBO
- kahawa (au vinywaji vyote vyenye caffein)
- pombe
- pilipili
- pilipili manga
- nyanya
- kitunguu swaumu
- karafuu
VYAKULA VYA KUTUMIA VINAVYOSAIDIA.
- Nyama isiyo na mafuta (lean meat)
- mkate wa brown (ambao ngano yake haijakobolewa)
- Vyakula jamii ya kunde (legumes)
- Mtindi
VYAKULA VYA KUTUMIA KWA KIASI.
- Vyakula vyenye mafuta
- Maziwa
TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO.
ikiwa unahitaji dawa ya vidonda vya tumbo, tafadhali bonyeza Hapa. WHATSAPP kisha utume neno VIDONDA VYA TUMBO
Imeandikwa na SAMUEL MACHA
FIT BY WAYNE.
Mimi nasikia maumivu ya tumbo upande wa kushoto yanakuja mpaka mgongoni , nilipina nikaambiwa Sina shida, ila maumivu yanakuja na kupotea, yaani nahisi Moto unawaka kabisa.
ReplyDeleteebu tuwasiliane zaidi tujue tatizo ni nini. whatsapp 0621068572
Delete