UZURI WA VIAZI VITAMU.
Viazi vitamu ni moja kati ya
vyakula vya wanga bora kabisa unavyoweza kula.
Hii ni kwa sababu ni Wanga Tata,
(Ccomplex carbohydrates), ikiwa inamaanisha havisababishi kupanda kwa insulin
na hivyo hamna kupanda kwa sukari. Glucose iliyopo ndani yake huachiliwa
taratibu kwa sababu vina wingi wa nyuzinyuzi.
Kama unauwezo wa kuvipanda
mwenyewe na kuvuna, ni bora Zaidi.
Inapendekezwa, kama unavila basi
ule na maganda yake kwa ajili ya kupata faiza zake zote (kama unaweza).
Viazi vitamu husaidia kuleta
uwiano wa bacteria wazuri wa kwenye utumbo ambao husababisha uzalishwaji wa
Butyrate. Kazi ya Butyrate ni kulinda kuta za tumbo zisitoboke na kuvuja.
Kumbuka ya kwamba, glucose sio
adui endapo wewe ni mwembamba na hua unashuhulisha mwili. Bali fructose
(inayopatikana kwenye sukari) ndio adui yetu mkubwa.
Napendekeza utumie vya
kuchemshwa, weka chumvi na ufurahie mlo wako.
Pia unaweza kuvianika juani, na
ukatengeneza unga wake ambao ni mzuri sana. Achana na unga wa sembe, hauna
faida yoyote kwako.
Comments
Post a Comment