Vyakula 8 Vinavyosaidia Kusafisha Damu Kwa Asili.
Mara zote huwa tunavuta hewa, tunakula pamoja na kunywa kemikali za hatari na kuingiza katika miili yetu. Miili yetu hua inafanana sana na injini mfano magari.
Gari ni lazima ulifanyie service kama vile kubadilisha oil n.k kila baada ya muda flani. Vivyo hivyo na miili yetu, ni lazima kujifunza kuisafisha na kuondoa taka mwili ambazo huingia kupitia njia mbali mbali kila siku.
Katika mlo wako wa kila siku, kuna vyakula unaweza kuviongeza na vikasaidia sana kusafisha mwili wako kuanzia ndani.
1. Giligilani
Majani ya giligilani |
Zina wingi wa vitakasa sumu (antioxidants) pamoja na Vitamin A, K pamoja na C, husaidia moyo, Figo pamoja na Ini kuondoa taka mwili ambazo hujishikiza humo.
Mafuta yaliyomo kwenye giligilani (volatile Oil) husawazisha seli zinazosababisha saratani.
Juisi ya giligilani husaidia sana afya ya macho pamoja na kuzuia uono hafifu wa macho kwa kuongeza mtiririko wa damu kwenye mishipa midogo midogo kwenye macho.
Tumia giligilani kama kiungo, juisi au chai mara kwa mara, na kisha uone matokeo utakayoyapata.
2. Kahawa
Kahawa |
Kikombe kimoja cha kahawa asubuhi kinatosha kukusaidia kusafisha damu kwa siku, pia kinaweza kukupa nguvu za kukukinga dhidi ya magonjwa.
Kahawa ni moja kati ya dawa za kukuongezea nguvu kulingana na tafiti mbali mbali zilizofanywa na wataalam.
Kahawa inaweza kupunguza hatari ya kupatwa na magonjwa ya Ini pamoja na saratani, pia inauwezo wa kuzuia mafuta kuzidi mwilini na yasihifadhiwe na Ini, lakini hii ni kama utatumia kahawa bila kuweka sukari.
Unaweza kuweka mdalasini, mnanaa (mint), cocoa au tangawizi.
NB: usitumie kahawa kama una changamoto ya shinikizo la juu la damu (high blood pressure)
3. Green Tea
Matumizi ya mara kwa mara ya green tea husaidia kuongeza uchomwaji wa kalori mwilini pamoja na kupunguza mlundikano wa mafuta yanayozunguka Ini, Hivyo kusaidia kupunguza hatari ya saratani.
Unaweza kuongezea ndimu/limao au asali kwa ajili ya ladha.
4. Manjano
manjano |
Kupakaa kwenye kidonda husaidia kutokushambuliwa na bakteria na hivyo kusaidia kidonda kupona haraka,
Matumizi ya chai ya manjano au kuitumia kama kiungo husaidia sana afya ya ngozi na kufanya ngozi isiwe na chunusi, mzio, vipele pamoja na muwasho.
5. Kabeji
kabeji |
Linauwezo mkubwa wa kusawazisha free radicles katika mwili kutokana na wingi wa Magnesium, phosphorus, Vitamin C, Calcium pamoja na anti-oxidants.
Pia linapunguza hatari ya kupata saratani ya figo, lakini endapo haitapikwa kwa kuiva sana. Hivyo ni nzuri ikitumika kama kachumbari.
6. Beetroot
beetroot |
7. Mboga za majani za kijani.
Ni chakula bora zaidi duniani chenye wingi wa Vitamins muhimu ambazo husaidia mwili kufanya kazi kama mashine ambayo ina vilainishi bora.
Enzymes zake husaidia detoxification ya Ini, zina phytonutrients ambazo husaidia afya ya ngozi, kumbukumbu nzuri pamoja na tumbo lenye afya.
8. Tangawizi
Tangawizi |
Tangawizi husaidia kuondoa magonjwa ya Ini pamoja na kuongeza ufanisi wa kazi ya Ini na hivyo kuboresha usafishwaji wa damu unaofanywa na Ini.
Comments
Post a Comment