Mazoezi |
NAMNA YA KUFANYA MAZOEZI KWA AFYA.
Mazoezi ni shughuli yoyote ya mwili ambayo huongeza au kudumisha utimamu wa mwili, afya na ustawi kwa ujumla.
NI KWA NINI WATU HUFANYA MAZOEZI?
- kusaidia ukuaji wa mwili
- kuboresha nguvu ya mwili
- kupunguza kasi ya uzee
- kuboresha au kukuza misuli
- kuboresha mfumo wa moyo na mishipa
- kuboresha ujuzi wa riadha
- kupunguza uzito/unene au kudumisha uzito sahihi
- kuboresha afya
- starehe na sababu nyinginezo
ISTILAHI MUHIMU ZA KUZIJUA
Kabla ya kuona jinsi ya kufanya mazoezi kadhaa, ni vyema kufahamu istilahi chache muhimu ambazo zitakuongoza katika ufanyaji mazoezi yako. Istilahi nyingine utaendelea kujifunza kadiri ynavyoendelea kubobea katika mazoezi.
REP: Hiki ni kifupisho cha neno Repeatition. katika mazoezi neno hili humaanisha kurudia kitendo flani. kwa mfano: mtu akisema 10 Reps, anamaanisha kufanya hicho kitendo husika mara 10. Kwa mtu ambae anapiga push up, akienda juu na chini amemaliza mara moja. hivyo 10 reps maana yake ni push ups 10.
SET: Hii ni kukamilisha marudio kadhaa ya zoezi husika kwa mpigo. kwa mfano mtu akipiga push up 10 kwa mpigo hapo tutasema amefanya set 1 ya zoezi la push up. hivyo akipiga push up 10 mfululizo, kisha akapumzika na kisha akapiga tena nyingine 10. Tutasema amepiga Set 2 za push up. lakini hapa tutaandika 2x10 (Set 2 zenye reps 10)
REST: Ni muda unaopumzika kati ya Set moja na Nyingine. Mara nyingi rest tunaziweka kwa sekunde, mfano mtu anaweza kuamua kupumzika sekunde 30 anapomaliza Set 1 kabla ya kwenda nyingine. Kwa mfano ukiona zoezi limeandikwa PUSH UP 2x10, 30 sec Rest. maana yake ni kwamba utapiga Set 2 za push up kila Set iwe na Reps 10, utapumzika kwa sekunde 30 baada ya kila set.
JINSI YA KUJUA KIWANGO CHA REPS KATIKA SET MOJA
Ikiwa unataka kufanya mazoezi, miili inatofautiana, kuna ambao wapo fit zaidi ya wengine katika ufanyaji mazoezi kulingana na sababu mbali mbali, hivyo kila mtu ni lazima ajue kiwango chake cha kuanzia.
Jambo la kufanya, katika zoezi husika, fanya REPS nyingi kadiri unavyoweza mpaka mwili wako utakapokua hauwezi kuendelea tena. kisha zile REPS utagawanya kwa 3, na namba utakayoipata basi ndio REPS unazotakiwa kupiga katika kila SET. Tazama mfano huu;
Tuseme unataka kujua kiwango cha Push up katika set husika. utakachofanya ni utapiga push up mpaka kufikia kikomo. tuseme utakua umepiga push up 30 ambapo utakua huwezi kuendelea tena kwa mara moja.
Ukigawanya 30 kwa 3 utapata 10, maana yake katika kila SET yako inatakiwa iwe na REPS 10 za push up. Hivyo unaweza kufanya 3x10, 30 sec Rest (ikiwa na maana ya kwamba utapiga SET 3 ambazo kila SET itakua na REPS 10 za push up, utapumzika kwa sekunde 30 baada ya kila set.
BAADHI YA MAZOEZI MAZURI UNAYOWEZA KUYAFANYA.
Mazoezi ya kupunguza tumbo
Mazoezi ya kupunguza nyama za mgongoni
Jitahidi uwe unafanya mazoezi ambayo utayafurahia na unayaweza, usifanye mazoezi ambayo yatakuumiza sana.
Kumbuka kuanza taratibu, utakua unaongeza ukali wa mazoezi kadiri muda unavyokwenda. Nitakua naweka mazoezi kuongezea kila nitakapokua napata.
Comments
Post a Comment