Madhara 7 Yanayowapata Wanawake Wanene.
Unene au uzito uliopitiliza una madhara kwa jinsia zote mbili, wanaume na wanawake, Ingawa kwa wanawake hupata madhara makubwa zaidi ukilinganisha na wanaume.
Madhara Yanayowapata Wanawake Wanene.
1. Kushindwa Kubeba Ujauzito
Wanawake wanene hupata changamoto nyingi zinazoathiri kizazi kama vile Polycistic Ovarian Syndrom ijulikanayo kama PCOS, Mji wa mimba kuzungungwa na mafuta au kuvurugika kwa hedhi inayosababishwa na kuvurugika kwa homoni.
2. Kupata Shida Wakati Wa Kujifungua
Wengi hupata tabu katika kusukuma mtoto au mtoto kua mkubwa (macrosomia). Hii husababishwa na uchochezi wa insulini kwa kiumbe kinachokua tumboni mwa mama kutokana na ulaji mbovu wa mama kwa muda mrefu.
3. Neuroticism (kutokua sawa kisaikolojia)
Mara nyingi hawa huwa na hasira za mara kwa mara, kujiona hawana thamani, kukosa kujiamini, kua na hisia hasi wakati mwingi, kua na ugomvi n.k. Hua wanajihisi kama vile kila mtu anawaona ni wabaya kutokana na miili yao ilivyo.
4. Sonona (Dpression)
Thamani ya mwanamke hua katika uzuri wake, tabia pamoja na Uzazi (kua mama), ndivyo jamii inavyowachukulia. Inapotokea amekua na uzito mkubwa, hukumbwa na msongo wa mawazo na kupelekea kua na sonona.
5. Magonjwa ya Kingamwili (Autoimmune)
Wanawake wanene wapo hatarini kupata magonjwa kama vile Lupus Disease (ni ugonjwa ambao mwili hushambulia viungo vya mwili), magonjwa ya ngozi, matatizo ya homoni n.k.
6. Magonjwa ya Kimetaboliki
Kama vile kisukari, shinikizo la juu la damu (presha), saratani ya matiti n.k
7. kupungua kwa Hamu ya Tendo la Ndoa
Hii huwapata wanawake wengi wanene, na matokeo yake wengi huwalaumu wanaume ya kwamba wana Uume mdogo, wanawahi kumwaga na wengi wao hudanganya ya kwamba wanafika kileleni, ila ukweli ni kwamba wengi hua hawafurahii Tendo hilo.
NB: Hamna unene wa kurithi, ila kuna kurithi mtindo mbaya wa maisha na mlo mbovu. Epuka Unene kwa nguvu zako zote, Chagua Afya, Chagua maisha.
Reference: Amerix
Comments
Post a Comment