MADHARA YA PAMPERS (DIAPERS) KWA WATOTO.
Kwa wale ambao ni wakongwe kidogo, yaani waliozaliwa miaka ya
90 kurudi nyuma, wengi hawakuvalishwa pampers na wazazi wao, bali walivalishwa
nepi au vinginevyo.
Lakini miaka ya hivi karibuni na tunapoelekea, kila mtoto
anavalishwa pampers kulingana na utandawazi unavyozidi.
Kadiri siku zinavyozidi kwenda, ndivyo ambavyo mwanadamu
anazidi kua mbali na asili yake na kuingia kwenye usasa ambao hauna chochote
cha asili. Kadiri mwanadamu anavyoacha asili yake, ndivyo ambavyo matatizo ya
ki afya huzidi Zaidi na Zaidi.
Pampers za watoto zimetengenezwa na kemikali hatarishi ambazo
huathiri afya ya mtoto ambae anakua. Kemikali hizo hufanya mambo yafuatayo; -
·
Huharibu
ngozi ya mtoto na kusababisha mzio wa ngozi maeneo ya sehemu zake za siri.
·
Kemikali
hizi hufyonzwa katika tishu za mwili na kusababisha shida katika kinga ya mwili
wa mtoto anaeivaa pampers hiyo.
·
Kemikali
hizi ni neurotoxic (husababisha shida katika mfumo wa fahamu). Hii hupelekea
kuharibika kwa mfumo wa fahamu wa mtoto (neurological failure)
·
Kemikali
hizi huharibu mfumo wa homoni wa mtoto, matokeo yake ni kuleta shida kama vile
matiti kwa mtoto wa kiume, hips na matako makubwa kama ya mwanamke wakati ni
jinsi ya ME. Kuharibika kwa mfumo wa hedhi na afya ya uzazi kwa ujumla kwa
watoto wa kike na mengine mengi.
·
Kuchelewa
kukua kwa maumbile ya mtoto wa kiume kutokana na kufungiwa ndani ya pampers kwa
muda mrefu yenye kemikali.
Kuna muda kama wazazi tunapaswa kujiuliza, je, kitu ambacho
kinauwezo wa kufyonza mkojo, ni salama kwa ngozi ya mtoto?
Yatupasa kukaa chini na kutafakari kwa kina. Kitu hakiozi
endapo kitatupwa. Hakiliwi na bacteria endapo utakifukia ardhini, ni salama kwa
mtoto? Ni hatari hata kwa mazingira yetu ya kawaida.
Usikubali mtoto wako kutumia pampers (diapers). Hua
inasikitisha kuona mtoto ana umri wa mwaka 1 bado anavaa pampers. Hii ni ishara
ya kwamba jamii yetu ina wazazi wavivu. Ni AIBU kubwa.
Kuanzia umri wa miezi 6, mtoto anatakiwa aachwe huru, na mara
nyingine acheze bila nguo. Haswa kama ni mtoto wa kiume.
Dunia inavyoenda na wakati, sio lazima asili yetu kuisahau,
sio kila maendeleo ni mazuri.
Comments
Post a Comment