JE, MLO WA ASUBUHI UNA FAIDA YOYOTE?
MLO WA ASUBUHI HAUNA FAIDA YOYOTE KWAKO.
Bila shaka umeshawahi kusikia au kuambiwa ya kwamba mlo wa
asubuhi ni mlo wa muhimu kuliko mlo wowote ule. Tena ukaambiwa maneno kama vile
‘Kula mlo wa asubuhi kama mfalme, mlo wa mchana kama mtoto wa mfalme na mlo wa
jioni kama ombaomba/maskini’
Je, kuna ukweli wowote kuhusiana na hili? Jibu ni HAPANA. Mlo
wa asubuhi ni mlo usio na maana au faida yoyote kwako kuliko mlo wowote ule.
NI KWA NINI MLO WA ASUBUHI HAUNA MAANA AU FAIDA YOYOTE KWAKO?
Inapofika saa kumi alfajiri, mwili wako huachilia kiwango cha
juu cha homoni aina nne.
I.
Glucagon
II.
Adrenaline
III.
Cortisol
IV.
Growth
hormone
Homoni hizi hupandisha kiwango chako cha sukari kwenye damu
wakati wa alfajiri kupitia mfumo wa kibaiolojia ujulikanao kama DAWN PHENOMENON. (ndio mfumo ambao
hufanya mwanaume au mtoto wa kiume awe amesimamisha uume wake wakati anapoamka
asubuhi).
Kiwango cha sukari kwenye damu hupanda kwa ajili ya kuandaa
mwili kuweza kupambana na siku husika.
Growth hormone huandaa misuli kwa ajili ya
kukabiliana na mchana wa siku husika na Adrenaline
huleta uchangamfu wa akili kwa ajili ya asubuhi.
Hali ya sukari kwenye damu kupanda itakua hivyo mpaka dakika
chache baada ya mchana (saa sita) ambapo itaanza kushuka, mwili sasa utaanza
kutumia njia nyingine ya kupata glucose kutoka kwenye misuli pamoja na Ini.
Katika hatua hii, mwili utaanza kugeuza mafuta ambayo yamehifadhiwa kwenye Ini
kua glucose.
Hivyo basi, wakati wa asubuhi huna haya ya kula, hamna faida
yoyote kwako. Mwili wako hauna ujinga wowote. Mwili hua unajua jinsi ya
kujiweka sawa, ni wewe mwenyewe ndie ambae unaupeleka ndivyo sivyo.
JARIBU HIVI.
Pima nguvu na uchangamfu wa mwili wako siku ukiwa umekula
asubuhi na siku ambayo haukula asubuhi. Utagundua yafuatayo…
Siku ukila asubuhi, utakua ni mtu mwenye uchovu mwingi, na
utakua unapata njaa kali sana kama ikifika mchana usipokula kwa wakati.
Siku usipokula asubuhi, unakua na utimamu wa akili, unakua na
uchangamfu pamoja na nguvu nyingi. Na unakua na uwezo wa kukaa muda mrefu bila
kula.
TABIA YA KULA ASUBUHI
IMETOKEA WAPI?
Afrika hatukua na tabia ya kula asubuhi, tabia hii ililetwa
na wazungu. Waafrika walikua wanakula tu pale ambapo jua limeshafika kati.
Tabia ya kula asubuhi iliundwa na kampuni zinazotengeneza
Breakfast kama vile Kellogs, General mills pamoja na Nestle ili wauze nafaka
zao kama vile corn flakes, Oats meal, wheetabix n.k
Ndio maana kuna msemo wazee wengi hupenda kutumia unaosema. HAKUNA MWANADAMU WA KAWAIDA ANATAKIWA KULA
WAKATI KUKU WAMELALA.
Imeandikwa na SAMUEL
MACHA
Mwanzilishi wa FIT BY
WAYNE.
Comments
Post a Comment