FAIDA 10 UTAKAZOZIPATA UKIACHANA NA MLO WA ASUBUHI.
FAIDA 10 ZA KUTOKULA ASUBUHI.
1. UTIMAMU WA AKILI/ KUMBUKUMBU NZURI
Unapokula chakula cha asubuhi,
unafanya domapine zako zimwagike bila sababu za msingi na hivyo kufanya uzito
katika ufanyaji kazi wa ubongo wako.
Watu ambao hula mlo wa asubuhi hua wanapata
uvivu na ufanisi wa kazi zao kwa siku husika hua mdogo kwa sababu ubongo unakua
bize kutengeneza dopamine ambayo imemwagika (dysregulated dopamine) pamoja na
kusimamia umeng`enywaji wa chakula.
2. ARI YENYE NGUVU (ENERGETIC SOUL)
Kila alfajiri kuanzia mida ya saa 10,
mwili wako huachilia homoni zijulikanazo kama counter-regulatory hormones
ambazo hukusaidia kukupa nguvu ya kuweza kupambana na siku husika.
Hata kama una kazi ngumu kwa asubuhi
hiyo, mwili wako unaweza kukupatia nguvu inayojitosheleza wewe kufanya shuhuli
zako pasipo shida yoyote.
Watu ambao hula asubuhi hupata kitu
kijulikanacho kama sugar crash ambapo miili yao hua dhaifu kwa sababu inakua
bize kuweka uwiano wa sukari ambayo hupanda ghafla baada ya kula.
Umeshawahi kujiuliza ni kwa nini watu
ambao hula asubuhi hua ni wachovu sana inapofika mchana? Ni kwa sababu ya sugar
crash ambayo wanaipata.
3. UWEZO MKUBWA WA KUDHIBITI HISIA ZAKO.
Unapokua hujala asubuhi, jambo la
kwanza tayari umeshinda kizuizi cha kwanza, ambapo unakua umeweza kuzuia
mtiririko wa neurochemicals usio na sababu katika ubongo wako.
Unakua na control na hamna kitu
kinachoweza kukuteteresha. Kwa sababu unakua na akili iliyotulia.
4. INSULIN SENSITIVITY NZURI.
Kila mara unapokula chakula,
unasababisha insulin kupanda (insulin spike). Na hii hua ni mbaya Zaidi wakati
wa asubuhi kwa sababu mwili wako tayari umeshaachilia counter-regulatory
hormones zake.
Hivyo basi, mwili hulazimika kumwaga
homoni ya glucagon ili kuweza kuleta uwiano wa insulin.
Unapokua huli asubuhi, insulin yako
hubaki katika kiwango kidogo na hivyo afya yako inabaki kua imara.
5. UWIANO MZURI WA KIWANGO CHA SUKARI.
Kwa kua huli asubuhi, insulin hubakia
kwa kiwango kidogo katika damu. Glucose ambayo iliachiliwa na homoni ya
glucagon alfajiri ya saa 10 inatumika ili kufanya shuhuli zako zote za asubuhi.
Iwe unatembea au kukimbia au unafanya
mazoezi, glucose ambayo iliachiliwa inatosha kabisa kukufikisha mchana ukiwa na
nguvu.
Endapo kukawa na upungufu wa glucose
inayohitajika, basi mwili wako utaanza kuchukua nishati kutoka kwenye mafuta
ambayo yamehifadhiwa mwilini katika mchakato ujulikanao kama GLUCONEOGENESIS.
Hivyo mlo wa asubuhi bado unabaki
hauna maana, mwili wako sio mjinga.
6. KUZALIWA KWA HOMONI YA TESTOSTERON.
Mwili pia huachilia homoni ya Growth
Hormone ambayo huchochea kuzalishwa kwa testosterone.
Endapo utafanya mazoezi wakati wa
asubuhi, kiwango chako cha testosterone kitapanda, ndio maana ndani ya nusu saa
baada ya mazoezi ya asubuhi utaona unasimamisha sana uume (kwa wanaume).
Testosterone ni hormone ya kiume,
unaweza kupata picha ni kwa nini wanaume ambao hawali asubuhi hua na nidhamu
kubwa na nguvu Zaidi ukilinganisha na wanaokula asubuhi.
7. UIMARA WA KINGA YA MWILI.
Homoni za cortisole pamoja na
adrenaline ambazo huzalishwa alfajiri hua ni anti-inflammatory. Husaidia
chembechembe nyeupe za damu kupambana na inflammation kwa kuzuia njia za
inflammation kutokea.
Ndio maana kwa wale wagonjwa, endapo
wasipokula asubuhi na kula mchana, hupata nafuu kubwa ukilinganisha na siku
ambazo wanakula asubuhi.
8. UIMARA WA AFYA YA TUMBO.
Endapo usipojaza tumbo lako na
chakula, maana yake unatoa nafasi kwa tumbo lako kufanya regeneration na
kupona, hivyo kua na afya imara Zaidi. (kumbuka afya ya mwili huanzia tumboni).
Hii hupelekea kuzalishwa kwa tindikali
ya HCL, enzymes, gut microbiome, nyongo yenye afya, ini lenye afya pamoja na
kibofu chenye afya.
9. KUONDOKANA NA NJAA KALI ZA MARA KWA MARA.
Umeshajiuliza ni kwa nini watu ambao
hula asubuhi hua ni wachovu sana inapofika mida ya mchana? Na ambao hawakula
asubuhi hufika mchana wakiwa na nguvu na wanakua wachangamfu (active).
Ni kwa sababu hupatwa na uraibu wa
sukari. Miili yako inakua inawaomba sukari muda wote. Na kama kuna duka karibu,
hua wanashindwa kujizuia na ni lazima wale au wanywe kitu cha sukari.
Hivyo kwa maelezo hayo machache, nina
Imani utakua umejifunza moja kati ya vitu muhimu sana katika maisha yako.
Hamna anaekulazimisha kuyafwata haya.
Ila tukumbuke ya kwamba matibabu hua ni gharama sana. Na matatizo mengi
tunaweza kuyaepuka kabla hayajatokea au kabla hayajawa makubwa.
Imeandikwa na FIT BY WAYNE.
Reference: www.amerix.co.ke
Comments
Post a Comment