Skip to main content

MAUMIVU YA KICHWA MARA KWA MARA

 

MAUMIVU YA KICHWA MARA KWA MARA.

Yawezekana hua unasumbuliwa au umeshaona mtu ambae hua anasumbuliwa na maumivu ya kichwa ya mara kwa mara.

Na mara nyingi maumivu haya hua hayaishi hata kama ukimeza paracetamol au dawa yoyote ya kutuliza maumivu.

Wengine huenda hospitali, kila vipimo wanavyofanyiwa huonyesha ya kwamba hawana shida yoyote ile. Mpaka wengine hudhania ya kwamba kuna mtu anawaloga.

NI KWA NINI MAUMIVU HAYA HUTOKEA?

Kisababishi kikuu hua ni upungufu wa madini ya Sodium mwilini. Kua na upungufu wa sodium kitaalam huitwa HYPONATRAEMIA.

Watu wenye upungufu wa Sodium hua na shida kwenye pampu ya umeme katika seli zao ijulikanayo kama Sodium-Potassium Channel Pump.

Pampu hii hutoa chaj za umeme kwa ajili ya kupeleka nguvu katika misuli na mfumo wa fahamu ili iweze kufanya kazi vizuri.

Kukiwa na shida katika pampu hiyo, hutoa potassium kwa wingi sana katika seli za ubongo na hivyo kusababisha hali ya excitation katika chaneli za fahamu na matokeo yake kupata maumivu ya kichwa.

Unapofanya shughuli za kutumia nguvu au akili na kuwaza sana, chaleni hiyo huleta voltage kubwa ya umeme inayoendeshwa na uwiano kati ya elektroliti za sodium pamoja na potassium.

Uwiano huu unapokosekana, pampu hiyo huanza kutoa elektroliti za potassium pasipo mpangilio maalum, na hivyo kusababisha maumivu ya kichwa.

JE, NINI CHA KUFANYA KUKABILIANA NA HILO?

Ni rahisi sana, tumia chumvi.

Chumvi itakupa Sodium ambayo itasaidia katika uwiano sawa wa chaneli ya pampu ya potassium.

        I.            Chukua chumvi kidogo katika vidole vyako kwa kufinya dole gumba pamoja na kidole cha kwanza. (pinch of salt). Au nusu kijiko cha chai na kisha uweke kwenye glass au kikombe cha maji ya vuguvugu.

      II.            Kunywa maji hayo kila asubuhi na kabla ya kwenda kulala usiku.

Kwa kufanya hivyo, utaondokana na tatizo la kuumwa kichwa mara kwa mara.

Okoa pesa zako kwa kumeza paracetamol kila siku.

Imeandikwa na SAMUEL MACHA, mwanzilishi wa FIT BY WAYNE

Reference:

www.amerix.co.ke


Comments

Popular posts from this blog

DETOX YA SIKU 7. HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE

  HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE. Uzito Unaotakiwa kua nao Kulingana na Urefu Pamoja na Jinsia UREFU (CM) UREFU (FT & INCH) UZITO (KG)       MWANAUME MWANAMKE 147 4' 10" - 45-59 150 4' 11" - 45-60 152 5' 0" - 46-62 155 5' 1" 55-66 47-63 157 5' 2" 56-67 49-65 160 5' 3" 57-68 50-67 162 5' 4" 58-70 51-69 165 5' 5" 59-72 53-70 167 5' 6" 60-74 54-72 170 5' 7" 61-75 55-74 172 5' 8" 62-77 ...

FANYA HIVI KAMA UNASUMBULIWA NA CHUNUSI

  FANYA HIVI KAMA UNASUMBULIWA NA CHUNUSI. Chunusi ni vimbe zinazosababishwa na kuzibika kwa folikoli za nywele na mafuta ya ngozi (sebum), seli za ngozi zilizokufa, na protini zilizokufa. Kuziba huku kunavuta bakteria wa ngozi ambao husababisha uvimbe na kuongezeka kwa vimbe hizi. Sebum ni dutu yenye mafuta inayozalishwa na tezi za mafuta kwenye ngozi yako. Sebum inalinda ngozi, lakini unapozalishwa kupita kiasi, inaweza kuziba njia za ngozi, kufunga seli za ngozi zilizokufa, na kuvuta bakteria wa ngozi, hivyo kusababisha uvimbe na chunusi.   Uzalishaji wa sebum kupita kiasi unatokana na homoni za ngono zinazosambaa sana kwenye damu. Hii ndiyo sababu chunusi ni kawaida kwa vijana na watu wazima vijana. Protini inayojulikana kama Sex Hormone Binding Globulin (SHBG) inapunguza homoni za ngono zisizo na mpangilio.   SHBG inashikilia homoni hizi za ngono ili zisilete athari zisizohitajika kwenye seli na viungo kama ngozi. Homoni hizi za ngono ni estrogeni na testos...

BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI

 BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI.   💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊   BAWASIRI NI NINI?   Bawasiri (kikundu, future, puru au mjiko ) ni hali ya kutuna kwa mishipa ya damu katika mfereji wa sehemu ya haja kubwa (anus). Kuna aina mbili za Bawasiri;   1. Bawasiri za ndani ( internal haemorroids )   2. Bawasiri za nje ( external haemorroids )  Bawasiri za ndani hua na dalili ya kupata kinyesi kilichokua na damu,  bawasiri za nje hua na dalili ya maumivu makali wakati wa kujisaidia pamoja na kinyama kutoka kwa nje.  NINI VISABABISHI VYA BAWASIRI?   1️⃣Historia ya familia, mara nyingi baadhi ya familia hukumbwa na changamoto hii. Na hua watu wa familia hiyo husika wanakua na hili tatizo. 2️⃣Kupata choo kigumu mara kwa mara husababisha mtu kutumia nguvu nyingi (straining) ambayo husababisha bawasiri kutokea. 3️⃣Unene (uzito uliopitiliza) hua ni kisababishi cha bawasiri kwa sababu ya kuongezeka kwa Rectal Vein Pressure. 4️⃣Ku...