ILI MWANAMKE AZALISHE
MAZIWA MENGI
Kwa muda mrefu sana wanawake wanaonyonyesha wamekua
wakiambiwa mambo kadhaa ili kuweza kuzalisha maziwa ya kutosha kwa ajili ya
watoto wao.
Mfano wa vitu wanavyoambiwa ni;
·
Kula
mara kwa mara upate maziwa
·
Kunywa
maziwa ili upate maziwa
·
Kunywa
soda ya coca ili uzalishe maziwa
·
Kula
matunda mengi
·
Kunywa
juisi ya Ribena
·
Na
mengine mengi.
Maziwa ya mama huzalishwa katika FAT LOBULES. Na ndio sababu kwa nini matiti ya mama hua makubwa
pale anapokua mjamzito.
Hakuna bomba kwenye titi la mwanamke ambalo litazalisha
maziwa eti kwa sababu amekula chakula flani. Chakula anachokula mama ni lazima
kipitie mmeng`enyo na kuweza kufyonzwa katika mwili.
Maziwa ya mama huhifadhiwa katika Fat Lobules kabla ya
kusisimuliwa ili yatoke katika chuchu.
Vyakula pekee amavyo mama anahitaji ni;
·
Nyama
·
Mayai
(ya kienyeji)
·
Samaki
·
Shahamu
muhimu (essential fats) kama vile mafuta ya wanyama, nazi na parachichi.
Mama anatakiwa kuzingatia kumnyonyesha mtoto mara kwa mara
ili kuweza kusisimua uzalishwaji wa maziwa.
Ni lazima mama afwate kanuni ya PQRSTU kwa ajili ya kuzalisha
maziwa ya kutosha kwa mtoto.
·
POSITION: mkao wa mtoto wakati ananyonya
·
QUALITY: ubora wa chakula ambacho amma
anakula, ni lazima kiwe chenye thamani kubwa ya lishe.
·
REGULARITY: mama anamnyonyesha mtoto mara ngapi
kwa siku?
·
SLEEP: mama anatakiwa ajitahidi kupata
usingizi na kupumzika pale anapopata nafasi.
·
UNINTERRUPTED BREAST FEEDING TIME: mama anatakiwa kumnyonyesha mtoto
bila kukatishakatisha.
Bila kuzingatia kanuni hizi, mama hawezi kupata maziwa ya
kutosha kwa ajili ya mtoto.
Kama ni mama unanyonyesha, wasiliniana nami uweze kupata
mwongozo wa mama anayenyonyesha. Bonyeza HAPA kisha unitumie ujumbe mfupi.
Reference; www.amerix.co.ke
Comments
Post a Comment