FUNGA KULA ILI UEPUKANE NA MARADHI.
Mwili wa mwanadamu haukuumbwa ili uwe na maradhi au kuugua.
Lakini ni kwa nini mwanadamu hua anasumbuliwa na maradhi?
Jaribu kuangalia wanyama kama sokwe, papa au mbwa mwitu. Ni
wanyama ambao ni nadra kuona wanaugua. Lakini umeshawahi kujiuliza ni kwa nini?
Jarbu kuangalia mazingira ya ulaji unaokuzunguka. Karibia
kila kitu unachokula hakifai katika mwili wako lakini bado unakula. Wanadamu
wanakula PRODUCTS Zaidi kuliko wanavyokula CHAKULA. Products ni vitu ambavyo
miili yetu haiwezi kumeng`enya vinapofika tumboni. Na ndio maana mwanadamu
anazungukwa na maradhi katika maisha yake.
Ipo mbinu moja ya kale sana ambayo mwanadamu yoyote yule
akiwa anaitumia hatakua mtu anayepata maradhi au kuugua ugonjwa wa aina yoyote
ule. Mbinu hiyo si nyingine bali KUFUNGA KULA (FASTING)
Unapokua umezuia mwili wako kula chakula kwa walau muda wa
masaa 16 na Zaidi, mwili wako utakua katika hali ijulikanayo kama AUTOPHAGY.
Yaani mwili wako hautafuni chakula, ila unaaza kutafuna sehemu za seli ambazo
ni mbaya na zingeweza kusababisha ugonjwa. Seli zako za mwili zinaanza
kushambulia sehemu mbaya za seli ili kuweza kuzitumia kama nishati badala ya
kuruhusu zisababishe madhara katika mwili.
Mwili wako ni mfumo ambao una akili sana, ila wewe ndio ambae
ni mjinga kwa kuulisha takataka na kutokufunga. Mwili una akili kiasi kwamba
unafahamu ni vitu gani vinatakiwa kuondolewa kwanza pale ambapo mtu anakua
amefunga. Hii huruhusu kuzaliwa kwa seli mpya ambazo zina manufaa. (na ndio
maana watu ambao hufunga kula mara kwa mara huchelewa kuzeeka ukilinganisha na
watu ambao hua wanakula kila siku)
Unapofunga kula, mwili huachilia homoni ya kukua (growth
hormone) ambayo itasaidia katika mchakato wa uponyaji.
Hivi ni vitu ambavyo hutaambiwa hospitali, lakini ndio siri
ambazo wazee wa kale walitumia wakaishi muda mrefu pasipokua na maradhi.
na Samuel Macha 0753068572
Comments
Post a Comment