HALI YA KUKOSA CHOO AU KUPATA CHOO KIGUMU.
Kukosa choo ni hali ya kushindwa
kupata choo baada ya saa 72 tangu upate choo mara ya mwisho.
Kama muda haujafika saa 72
haitaitwa hali ya kukosa choo. Ni lazima saa 72 zitimie.
Zipo sababu kadhaa zinazoweza
kusababisha mtu kuchelewa kupata choo kama vile;-
I.
Unapokua umefunga kula
II.
Unapobadilisha mazingira uliyoyazoea kujisaidia.
III.
Unapovadilisha muda ambao umezoea kujisaidia.
Endapo utazidisha Zaidi ya saa 72
bila kupata choo basi fanya yafuatayo;-
I.
Usizidishe kiwango cha nyuzi nyuzi, kwani ni
sawa na kuongeza idadi ya magari katika barabara ambayo tayari ina foleni
kubwa.
II.
Kunywa SALINE WATER (maji yenye chumvi) mara 2
kwa siku. Hii itasaidia kusisimua shughuli za utumbo wako. Utumbo umetengenezwa
kwa misuli laini ambayo hua inatanuka na kusinyaa kupitia chaneli ya
sodium-potassium pump.
III.
Tumia maziwa ya mtindi au sauerkraut. Kwa sababu
mzunguko wa utumbo husimama pale ambapo bacteria wa tumboni huzidiwa na mabaki
ya chakula ambacho mtu amekula. Mtindi na sauerkraut husaidia kuleta uwiano
mzuri wa bacteria katika tumbo.
IV.
Usitumie antibiotics (kutokana na sababu tajwa
(iii) hapo juu)
V.
Usitumie antacids. Hizi husababisha bacteria
wako wa tumboni wazubae. Ni mchakato ujulikanao kama SIBO. (Small Intestinal
Bacteria Overgrowth)
VI.
Usitumie dawa za vidonda vya tumbo (ANT-ACIDS):
hizi ndio sababu kubwa kwa nini bacteria wako wa tumboni hawafanyi kazi kwa
ufasaha. Ni kwa sababu ya hali ijulikanayo kama SIBO (Small Intestinal Bacteria
Overgrowth).
VII.
Tumia shahamu (short chain fatty acids) kutoka
kwenye mafuta ya wanyama au kutoka kwenye siki ya tufa (apple cider vinegar).
Utatumia vijiko 5 katika glass ya maji ya vuguvugu
VIII.
Chuchumaa unapokua unajisaidia, hii itasisimua
utumbo wako uweze kusukuma. (Initiate bowel movements). Epuka kabisa kutumia
vyoo vya kukaa unapojisaidia.
BONUS: usikimbilie kwa haraka kununua madawa unapopata shida, 80%
ya muda hua huzihitaji.
Reference; www.amerix.co.ke
Comments
Post a Comment