UZITO/UNENE HUPOTEA KIUNONI NA SIO KWENYE MZANI.
Ukitaka kutambua mwenendo wako wa kupungua uzito au unene,
basi tumia kiuno chako na wala usitumie mzani.
Mzani hauwezi kukupa ufanisi wa kujua uzito au unene ambao
umepungua. Mzani hua unakupa tu uhakika, lakini kiuhalisia haikuonyeshi
maendeleo yako kwa ufasaha.
Usitumie muda mwingi sana kuangalia mzani wako unasemaje, kwa
sababu mizani tofauti hua na calibration ya tofauti na pia unapopima kwa
nyakati tofauti hua unapata namba tofauti.
NJIA BORA YA KUJUA UZITO AU UNENE ULIOPUNGUA NI IPI?
Njia bora Zaidi ni WAIST-TO-HEIGHT
RATIO (WSR). Lakini pia, kuna mambo kadhaa ambayo unaweza kuangalia na
kujua ya kwamba unapata matokeo mazuri. Mfano wa njia hizo ni; -
·
Kupata
usingizi mzuri ambao mwanzoni hukua unaupata.
·
Kutokupata
njaa mara kwa mara na kushiba mapema hata kama umekula chakula kidogo au mara
moja kwa siku (improved insulin sensitivity) ambapo hapo awali ulikua unakula
sana na kupakua chakula kingi ili ushibe.
·
Presha
ya chini (diastolic blood pressure) kusoma kiwango cha chini ukilinganisha na
hapo awali.
·
Kupungua
kwa mapigo ya moyo tofauti na mwanzo.
·
Uwezo
mkubwa wa kufanya kazi kwa muda mrefu bila kujihisi mchovu.
·
Kutokupatwa
na hasira mara kwa mara tofauti na mwanzo.
·
Na
mengine mengi sana ambayo siwezi kuyataja yote.
Hivyo basi, ni vyema ukazingatia mabadiliko ya kiuno chako
Zaidi kuliko kuangalia kilo zako kwenye mzani.
JINSI YA KUANGALIA KIWANGO CHA UNENE WAKO KUTUMIA WSR.
Kama wewe ni MWANAUME, basi kiuno chako kinatakiwa kuwakati
ya inches 31 hadi 35. Na kwa MWANAMKE inatakiwa isizidi inches 36.
JINSI YA KUKOKOTOA WSR YAKO.
Pima mzunguko wa kiuno chako katika cm (sentimita), ugawanye kwa urefu wako kwa cm (sentimita).
WSR= Waist (kiuno) cm ÷ Height (urefu) cm
Jibu utakalopata inatakiwa isizidi 0.5 kwa MWANAUME na MWANAMKE.
Mfano.
SAMUEL MACHA, Kiuno ni inches 31. Ambayo ni sawa na cm 78.7 na Urefu ni cm 175.
WSR= Waist (kiuno) cm ÷ Height (urefu)
WSR= 78.7cm ÷ 175 cm = 0.4
Hivyo WSR ya SAMUEL MACHA ni 0.4
Na hivyo ndio jinsi ya kujua kama upo ndani ya unene
unaotakiwa au la. Ila kikubwa ni PROGRESS OVER PERFECTION. Yaani huezi kua
mkamilifu kwa siku moja, bali unatakiwa kuhakikisha ya kwamba kila siku unapiga
hatua, na leo uhakikishe unakua bora kuliko jana. ROMA HAIKUJENGWA KWA SIKU MOJA.
Reference:
Comments
Post a Comment