Skip to main content

Posts

JE, MAJI YA MOTO HUSAIDIA KUPUNGUZA KITAMBI?

  JE, MAJI YA MOTO HUSAIDIA KUPUNGUZA KITAMBI? Bila shaka umeshawahi kuona watu ambao hunywa maji ya moto na limao kila asubuhi huku wakisema ya kwamba wanafanya hivyo ili kupunguza kitambi. Cha ajabu ni kwamba watu hawa wanafanya hivi lakini hawafanyi mabadiliko yoyote juu ya vyakula wanavyokula au mtindo wa maisha. Kwa kifupi ni kwamba, ukiona mtu anasema anakunywa maji ya moto kwa lengo la kupunguza kitambi, ujue ni mvivu wa kubadilisha mtindo wake wa maisha na anapenda njia za mkato. Ila ukweli ni kwamba, katika kupunguza unene na kuondokana na kitambi, hua hamna njia za mkato. UKWELI KUHUSU MAJI YA MOTO Maji ya moto hayayeyushi mafuta kama wengi wanavyodhani. Na pia hayana mchango wowote katika kuyeyusha mafuta yanayosababisha unene mwilini mwa mwanadamu. Tindikali ya Hydrocloric tumboni ndio husaidia katika kumeng`enya chakula, lakini sio maji ya moto. Mtu anayekunywa maji ya moto na anayekunywa maji ya baridi, wote wanakunywa maji. Na hamna kitu cha ziada kinac...

MADHARA YA UNENE KWA WANAWAKE

  MADHARA YA UNENE KWA WANAWAKE. Wanawake hupata madhara makubwa Zaidi kwa sababu ya unene ukilinganisha na wanaume. Ingawa ifahamike ya kwamba, unene una madhara na athari kubwa wa mtu yoyote bila kujali ni wa jinsia gani. NI KWA NINI MWANAMKE ANA ATHIRIKA ZAIDI? ·          MATATIZO YA UZAZI : wanawake wanene huwa wanakumbwa na changamoto nyingi za uzazi kutokana na kuvurugika kwa homoni pamoja na mzunguko wa hedhi. ·          KUPUNGUA KWA HAMU YA TENDO LA NDOA : mara nyingi huwalaumu wanaume kwamba wana uume mdogo au wanamwaga mapema. Lakini uhalisia ni kwamba wanawake wanene hua hawana hamu ya tendo la ndoa, ni ngumu kuamsha hisia zao za mahaba ukilinganisha na wanawake wenye uzito sahihi. ·          MATATIZO KATIKA KUJIFUNGUA: hua wanapoteza nguvu katika kusukuma mtoto wakati wa kujifungua. Au pia hua na watoto wakubwa (macrosomia) kutokana na athar...

USITUMIE DAWA ZA MAUMIVU AU ANTIBIOTIKI PASIPO SABABU ZA MSINGI

  USITUMIE DAWA ZA MAUMIVU PASIPO SABABU ZA MSINGI. Mara nyingi dawa hua hazitibu au kuondoa tatizo, bali zinatuliza dalili ambazo zinatokana na tatizo husika. Dawa za antibiotic hua zina ufanisi kwa sababu hua zinaenda kuangamiza vimelea vinavyosababisha ugonjwa, ila shida yake ni moja, hua zinaangamiza pia bacteria wazuri ambao wapo ndani ya mwili wako. Ndio maana ni busara sana kama umetoka kutumia dawa za antibiotic kwa ajili ya matibabu, uwe unatumia vyakula vichachu (fermented foods), mfano maziwa ya mtindi ili kuweza kurudisha uwiano wa bacteria wazuri katika tumbo. Usitumie antibiotic, dawa za maumivu au antacids kwa Zaidi ya siku 5 mfululizo. Kwani utaangamiza bacteria wako wazuri katika tumbo, ambao ndio wanaosaidia kuweka mwili wako sawa. Ni vyema kujua haswa chanzo cha tatizo ni nini, badala ya kukimbilia kumeza dawa. Usiwe mtumwa wa madawa. Kila dawa unayomeza inakuachia sumu mwilini mwako. Kumbuka ya kwamba CHEMBE NA CHEMBE MKATE HUWA . Na SAMUEL MACHA F...

BAWASIRI NA JINSI YA KUJITIBU UKIWA NYUMBANI.

  BAWASIRI NA JINSI YA KUKABILIANA NAYO NYUMBANI. Bawasiri ni sehemu katika njia ya haja kubwa mwishoni (rectum) au dalili ya tatizo lenyewe. Mishipa ya fahamu ya Bawasiri (Haemorrhoidal Plexus): ni mfumo wa mishipa ya fahamu, mishipa ya damu, tishu pamoja na misuli laini. Haemorroidal Plexus ni kama sehemu laini ambayo husaidia kudhibiti haja kubwa wakati wa haja kutokana na mgandamizo mkubwa unaokuepo katika tumbo. Plexus hii pia huhakikisha ya kwamba njia ya haja kubwa (anus) hufunga vizuri wakati mtu amepumzika au ametulia Kuna aina mbili za haemorroidal plexus.         I.             Internal plexus       II.             External plexus External plexus (mishipa upande wa nje) zina mishipa wakati internal plexus haina mishipa ya fahamu. Hivyo external plexus (mishipa ya nje) hua na maumivu makal...

UKWELI KUHUSU NJIA ZA UZAZI WA MPANGO

  Njia za uzazi wa mpango Ukweli Kuhusiana Na Njia za Uzazi wa Mpango. Kuna aina 2 kuu za njia za uzazi wa mpango. 1.       Combined Oral Contraceptives (progesterone and oestrogen) 2.        Progesterone only contraceptives (POC) Hua zinakuja katika hali tatu tofauti. 1.       Vidonge vya kumeza. (ikijumuisha na P2) 2.       Sindano ambazo mtu huchomwa kila baada ya miezi 3 3.        Long acting mfano Norplant or jadelle (vitanzi) Njia hizi huzuia mbegu zisirutubishe yai katika mirija ya uzazi wakati wa ovulation. Hivyo hufanya kazi ya kuzuia ovulation kwa mwanamke. Mwanamke anapomeza dawa hizi, hutuma taarifa hasi (negative feedback) kwenye hypothalamus (sehemu ya ubongo) ambapo hupunguza uzalishwaji wa follicle stimulating hormone (FSH) pamoja na Lutenizing Hormone (LH), ambapo hufanya au kuzuia ukuaji wa follicle. Follicle ni k...

Mbinu za Kukusaidia Kua Mwanaume Rijali na Kuondokana na Upungufu wa Nguvu za Kiume

  Mbinu Zinazosaidia Kua Mwanaume Rijali na Kuondoa Upungufu Wa Nguvu Za Kiume. Upungufu wa nguvu za kiume (Erectile Dysfunction) ni hali ya kukosa uwezo wa kudumisha kusimama kwa uume wakati wa kufanya ngono. Hali hii huleta fedheha ambayo huteteresha mahusiano yaliyo mengi, husababishwa na matukio au hali ambazo huvuruga utimamu wa misuli, vhichochezi (hormones), mishipa ya fahamu pamoja na mishipa ya damu katika uume. Visababishi Vya Upungufu Wa Nguvu Za Kiume. Sababu za Kisaikolojia Sababu za kimetaboliki Sababu za mfumo wa neva za fahamu pamoja na mifupa ya misuli. 1. Sababu za Kisaikolojia Sonona/ msongo wa mawazo Unywaji wa pombe na sigara: (hudhoofisha mfumo wa neva, ubongo pamoja na mishipa ya damu kadiri mtumiaji anavyotumia) Wasiwasi Hali ya hatia Kujiona huna thamani (low self esteem) Picha ama video za ngono na punyeto: Hizi ndio mbaya zaidi kwani huleta ganzi katika sehemu zihusikazo na ladha za kimahaba katika ubongo. 2. Sababu Za Kimetaboliki Ugonjwa wa kisukari Shi...

Nini Cha Kufanya Endapo Unaugua (Au mtoto kuugua) Mafundofundo Mara Kwa Mara

Mafundofundo Tonsillitis, Tonsils, Mafundofundo, Matezi. Tonsillitis ni inflammation ya Tonsils pale ambapo mwili hushambuliwa na bacteria au virusi. Tonsilitis ni tishu 2 zenye umbo la mviringo zinazopatikana nyuma ya koromeo pande mbili za ulimi. Tonsils ni mstari wa mbele katika kinga ya mwili. Hizi huzuia vimelea hatarishi kabla havijafika katika mfumo wa mwili. Tonsils zinapokamata vimelea, na zenyewe hupata inflammation na kupelekea hali ijulikanayo kama Tonsillitis ambapo huvimba na kua na mamumivu pale unapokua unameza kitu. Mara nyingi watu haswa watoto hupata Tonsillitis na kwenda hospitali kutibiwa kwa antibiotics. Ila kuna ambazo zinajirudia mara kwa mara hata kama zikitibiwa kwa dawa. Mara nying8 katika hali ya kujirudia mara kwa mara, wengi hushauriwa kufanya upasuaji mdogo ujulikanao kama Tonsilectomy ili kuziondoa. Ikiwa Tonsils ndio mstari wa mbele wa kinga, ni kwa nini ziondolewe? Nini Kifanyike Endapo Tonsillitis Inajirudia Mara kwa Mara. Epuka kabisa sukari na vitu ...