Mafundofundo |
Tonsillitis, Tonsils, Mafundofundo, Matezi.
Tonsillitis ni inflammation ya Tonsils pale ambapo mwili hushambuliwa na bacteria au virusi.
Tonsilitis ni tishu 2 zenye umbo la mviringo zinazopatikana nyuma ya koromeo pande mbili za ulimi.
Tonsils ni mstari wa mbele katika kinga ya mwili. Hizi huzuia vimelea hatarishi kabla havijafika katika mfumo wa mwili.
Tonsils zinapokamata vimelea, na zenyewe hupata inflammation na kupelekea hali ijulikanayo kama Tonsillitis ambapo huvimba na kua na mamumivu pale unapokua unameza kitu.
Mara nyingi watu haswa watoto hupata Tonsillitis na kwenda hospitali kutibiwa kwa antibiotics. Ila kuna ambazo zinajirudia mara kwa mara hata kama zikitibiwa kwa dawa.
Mara nying8 katika hali ya kujirudia mara kwa mara, wengi hushauriwa kufanya upasuaji mdogo ujulikanao kama Tonsilectomy ili kuziondoa.
Ikiwa Tonsils ndio mstari wa mbele wa kinga, ni kwa nini ziondolewe?
Nini Kifanyike Endapo Tonsillitis Inajirudia Mara kwa Mara.
- Epuka kabisa sukari na vitu vya sukari katika lishe yako na lishe ya mtoto.
- Epuka wanga na nafaka zilizokobolewa katika lishe yako na ya mtoto.
- Epuka kupikia mafuta ya mbegu (vegetable oils), badala yake tumia mafuta ya nazi au ya wanyama kama vile siagi, samli, tallow (mafuta ya ng`ombe), mafuta ya zeituni, mafuta ya parachichi, mafuta ya zeituni, Lard (mafuta ya nguruwe), Suti (mafuta ya kondoo), na mafuta mengineyo ya wanyama.
- Tembea au mtembeze mtoto juani mara kwa mara. haswa jua la asubuhi
- Tumia vyakula vyenye wingi wa madini ya Zinc kama vile nyama, kuku, mbegu kama korosho, karanga, mlozi n.k, maharage, vyakula vya baharini kama vile chaza, pweza, ngisi n.k
vyakula vyenye Zinc |
Comments
Post a Comment