MADHARA YA UNENE KWA WANAWAKE.
Wanawake hupata madhara
makubwa Zaidi kwa sababu ya unene ukilinganisha na wanaume. Ingawa ifahamike ya
kwamba, unene una madhara na athari kubwa wa mtu yoyote bila kujali ni wa
jinsia gani.
NI KWA NINI MWANAMKE ANA ATHIRIKA ZAIDI?
·
MATATIZO
YA UZAZI: wanawake wanene huwa wanakumbwa na changamoto nyingi
za uzazi kutokana na kuvurugika kwa homoni pamoja na mzunguko wa hedhi.
·
KUPUNGUA
KWA HAMU YA TENDO LA NDOA: mara nyingi huwalaumu wanaume
kwamba wana uume mdogo au wanamwaga mapema. Lakini uhalisia ni kwamba wanawake
wanene hua hawana hamu ya tendo la ndoa, ni ngumu kuamsha hisia zao za mahaba
ukilinganisha na wanawake wenye uzito sahihi.
·
MATATIZO
KATIKA KUJIFUNGUA: hua wanapoteza nguvu katika kusukuma
mtoto wakati wa kujifungua. Au pia hua na watoto wakubwa (macrosomia) kutokana
na athari za insulin kwa mtoto anaekua tumboni.
·
VISIRANI
NA HASIRA ZISIZOKUA NA SABABU: wanawake wanene hua na self-esteem
ndogo. (hali hafifu ya kujithamini). Hivyo wengi hua na visirani na hasira za
hapa na pale bila sababu za msingi.
·
HUZUNI:
mwanamke hujivunia uzuri wake na uzazi, mara nyingi anapokua mnene hujiona kama
thamani yake ya uzuri imeshuka na huhisi ya kwamba mume wake au mwanaume yoyote
hamuangalii kwa matamanio kama ilivyo kwa mwanamke mwembamba au mwenye uzito wa
kawaida..
·
MAGONJWA
YA AUTOIMMUNE: hua na hatari kubwa ya kupata magonjwa ya
auto immune kama vile lupus, shida za homoni (thyroid conditions) n.k
·
SYDNROME
X:
wanawake wanene wengi huishia kupata shida za kimetaboliki kama vile kisukari,
presha, saratani ya matiti n.k
Kama wewe ni mwanamke, na
kama una mke ambae ni mnene. Msaidie aweze kua na uzito sahihi. Mtie moyo, kua
nguvu yake anapokata tamaa, muaminishe ya kwamba inawezekana kuondokana na
unene. Ukiwa kama baba wa familia, wewe ndio kichwa kwa maana ya kiongozi. Anza
kuongoza familia yako katika ulaji unaofaa. Usitoe pesa kununua visivyofaa,
ukitaka familia ile vyakula vizuri, maana yake hakikisha vinavyokuwepo nyumbani
ni vyakula sahihi na sio products.
Na wewe kama mwanamke, ni
lazima ukubali ndani ya nafsi yako kuondokana na unene. Kaa mbali na wale
mashoga au mashosti ambao watakukatisha tamaa. Sio lazima utangaze kama unataka
kupungua, wewe fanya kimya kimya. Watu wataona tu matokeo yako. Na wewe
mwenyewe afya yako itaimarika.
Wanawake hua na athari
mbaya Zaidi za unene ukilinganisha na wanaume, ingawa madhara yatokanayo na
unene yanampata kila mwanadamu.
Na FIT BY WAYNE.
Comments
Post a Comment