BAWASIRI NA JINSI YA KUKABILIANA NAYO NYUMBANI.
Bawasiri ni sehemu katika njia ya haja kubwa mwishoni
(rectum) au dalili ya tatizo lenyewe.
Mishipa ya fahamu ya Bawasiri (Haemorrhoidal Plexus): ni
mfumo wa mishipa ya fahamu, mishipa ya damu, tishu pamoja na misuli laini.
Haemorroidal Plexus ni kama sehemu laini ambayo husaidia
kudhibiti haja kubwa wakati wa haja kutokana na mgandamizo mkubwa unaokuepo
katika tumbo.
Plexus hii pia huhakikisha ya kwamba njia ya haja kubwa
(anus) hufunga vizuri wakati mtu amepumzika au ametulia
Kuna aina mbili za haemorroidal plexus.
I.
Internal
plexus
II.
External
plexus
External plexus (mishipa upande wa nje) zina mishipa wakati
internal plexus haina mishipa ya fahamu. Hivyo external plexus (mishipa ya nje)
hua na maumivu makali wakati ya ndani haina maumivu.
Mishipa hii (haemorroids) huleta dalili pale zinapotanuka,
kuvimba au kutokezea kwa nje ya njia ya haja kubwa.
Mtu anapokua katika sababu za hatari mara nyingi hupelekea
kuvimba kusiko kwa kawaida katika sehemu ya mishipa hiyo (plexus)
Na inapotokea mtu anapata haja kubwa, basi hupelekea kutokwa
na damu ambayo ni nyekundu ambayo haijakolea (bright red)
Plexus hizo zikitokea kwa nje, hupelekea choo kua na ute ute
ambao husababisha sehemu ya haja kubwa kuwasha mara kwa mara.
Kisababishi kikuu hakijulikani, ila kuna sababu za hatari
(risk factors) ambazo huongeza mgandamizo katika eneo la plexus.
SABABU ZA HATARI ZA BAWASIRI
I.
Kutumia
nguvu au kujikamua wakati wa haja kubwa
II.
Kukaa
chooni kwenye choo cha kukaa kwa muda mrefu (haswa watu ambao hua wanaenda na
simu za mkononi au kusoma vitabu wanapojisaidia)
III.
Mimba
IV.
Kufanya
ngono kinyume na maumbile
V.
Uzito
uliopitiliza au unene
VI.
Majeraha
katika uti wa mgongo
VII.
Lishe
isiyo na nyuzinyuzi
VIII.
Misuli
dhaifu ya njia ya haja kubwa
IX.
Historia
ya bawasiri katika familia.
ISHARA NA DALILI ZA BAWASIRI.
I.
Maumivu
wakati wa kukaa au wakati wa haja kubwa
II.
Kuwashwa
katika sehemu ya haja kubwa
III.
Kupata
damu katika choo au damu kuwepo katika toilet paper uliyoitumia.
IV.
Uvimbe
wenye maumivu katika sehemu ya njia ya haja kubwa.
Kutokwa damu wakati wa haja kubwa ni ishara kubwa Zaidi ya
bawasiri.
Bawasiri inaweza kutibiwa ukiwa nyumbani kwako, ingawa
inaweza isipone kabisa. Matibabu ya nyumbani yatakuondolea maumivu, uvimbe
pamoja na inflammation.
Bawasiri ambayo inajirudia mara kwa mara huenda ikahitaji
matibabu Zaidi hospitali pamoja na upasuaji.
Bawasiri inaweza kujirudia baada ya matibabu, hivyo ni rahisi
kudhibiti na kuzuia kuliko kuitibu na kupona.
JINSI YA KUJITIBU BAWASIRI NYUMBANI.
I.
Unaweza
kuloweka sehemu yako ya haja kubwa katika maji ya vuguvugu kwa dakika 15, hii
itakusaidia kukupa unafuu.
II.
Unaweza
kutumia vilainisha choo ambazo husaidia kupata choo kilaini.
III.
Sehemu
ya njia ya haja kubwa inapaswa kuwa safi mara zote
IV.
Unaweza
kutumia dawa za maumivu kama vile paracetamol (Panadol) ili kupunguza maumivu.
Endapo kutokwa na damu kunaendelea ama hakuna nafuu yoyote,
basi ni vyema kuonana na daktari kwa ajili ya matibabu Zaidi.
JINSI YA KUZUIA BAWASIRI.
I.
Kula
vyakula vyenye wingi wa nyuzi nyuzi kama vile wanga tata (complex carbohydrates)
na mboga za majani pamoja na mbogamboga
II.
Kunywa
maji ya kutosha kulingana na uzito wako. (kwa kawaida, katika kila kilo 20
huhitaji maji lita moja). Hivyo utaangalia katika uzito wako, ishirini zipo
ngapi.
III.
Usijikamue
au kulazimisha kupata haja. Nenda chooni pale unapohisi haja, kama huna haja,
epuka kukaa chooni.
IV.
Tumia
choo cha kuchuchumaa badala ya kukaa.
V.
Fanya
mazoezi walau mara 4 kwa wiki. Ni muhimu sana.
VI.
Punguza
uzito kama ni mnene.
FANYA MAMBO YAFUATAYO KAMA HUA UNAPAMBANA NA BAWASIRI
I.
Acha
kabisa kutumia choo cha kukaa na uanze kuchuchumaa.
II.
Usitumie
maziwa pamoja na ngano. (lactose iliyopo kwenye maziwa hupelekea inflammation
ya tumbo)
III.
Acha
kabisa matumizi ya sukari pamoja na asali (hii itasaidia Ini lako kua huru na
kutengeneza chumvi za bile (bile salts) pamoja na lehemu (cholesterol)
IV.
Usitumie
mafuta ya mbegu (vegetable oils and seed oils). Hua yanaleta inflammation
V.
Jifunze
kufunga kula mara kwa mara. (mfumo wa OMAD au One Meal a Day ni njia nzuri
Zaidi ili kuruhusu tumbo kua tupu na kujifanyia uponyaji)
VI. Epuka matumizi ya pombe. Huleta inflammation ya tumbo
hhhh
Comments
Post a Comment