Skip to main content

UKWELI KUHUSU NJIA ZA UZAZI WA MPANGO

 

Njia za uzazi wa mpango

Ukweli Kuhusiana Na Njia za Uzazi wa Mpango.

Kuna aina 2 kuu za njia za uzazi wa mpango.

  1. 1.      Combined Oral Contraceptives (progesterone and oestrogen)
  2. 2.      Progesterone only contraceptives (POC)

Hua zinakuja katika hali tatu tofauti.

  1. 1.      Vidonge vya kumeza. (ikijumuisha na P2)
  2. 2.      Sindano ambazo mtu huchomwa kila baada ya miezi 3
  3. 3.      Long acting mfano Norplant or jadelle (vitanzi)

Njia hizi huzuia mbegu zisirutubishe yai katika mirija ya uzazi wakati wa ovulation. Hivyo hufanya kazi ya kuzuia ovulation kwa mwanamke.

Mwanamke anapomeza dawa hizi, hutuma taarifa hasi (negative feedback) kwenye hypothalamus (sehemu ya ubongo) ambapo hupunguza uzalishwaji wa follicle stimulating hormone (FSH) pamoja na Lutenizing Hormone (LH), ambapo hufanya au kuzuia ukuaji wa follicle.

Follicle ni kimfuko ambacho hua na yai ambalo halijakomaa. Isipotumika, basi yai hilo hupoteza uhai na mwanamke atakosa ovulation yake na kutokua na fertilization (kurutubishwa kwa yai).

Je, tatizo liko wapi?

1.      OVULATION ni sifa moja wapo kati ya sifa kuu za mwanamke yeyote yule. Ni wakati ambapo mwanamke hua mwanamke kweli. Kwa lugha nyingine tunasema, ni wakati ambao miungu yake ya uzazi hua hai. Na ndio maana hua na hamu ya kukutana na mwanaume kuliko wakati mwingine wowote.

Progesterone ni homoni ambayo humtuliza mwanamke. Kwa sababu ya kuchochea uzalishwaji wa serotonin na melatonin (homoni za usingizi)

Progesterone husaidia ufanyaji kazi wa homoni nyingine ambazo husaidia kuondoa inflammation kwenye mwili kutoka kwenye adrenal glands.

Progesterone husaidia mwili wa mwanamke kufyonza virutubisho  muhimu kama vile zinc, magnesium, iodine pamoja na calcium na kuweka sawa uwiano wa bacteria katika tumbo.

Sasa mwanamke anapomeza dawa hizi, huzuia uzalishwaji wa homoni ya progesterone. Kwa kawaida progesterone hutengenezwa na cholesterol. Ndio maana wanawake wanaomeza dawa za STATINS (zinazopunguza cholesterol) au wanaokula lishe yenye upungufu wa shahamu (fats) hua wana kiwango kidogo cha progesterone.

NI NINI HUTOKEA PALE AMBAPO MWANAMKE ANAKOSA PROGESTERONE?

  •         I.            Hupata inflammation mara kwa mara. Kama vile kuumwa kwa matiti, kuumwa tumbo wakati wa hedhi pamoja na kupata maginjwa mbali mbali.
  •       II.            Hubadilika mood mara kwa mara na kua na kisirani, hasira kali au kukosa usingizi kutokana na mvurugiko wa serotonin na melatonin
  •     III.            Kushindwa kubeba ujauzito, anaweza kuchelewa sana au kupata tatizo la mimba kuharibika mara kwa mara kwa sababu hamna progesterone ya kutosha kushikilia mimba vizuri.
  •     IV.            Matatizo ya tumbo ya mara kwa mara kama vile kujaa gesi, kuvimbiwa, kukosa choo na vidonda vya tumbo.
  •       V.            Kuongezeka uzito kutokana na uharibifu wa satiety hormone inayoitwa Ghrelin.
  •     VI.            Maji kutokutoka ndani ya mwili.
  •   VII.            Mifupa dhaifu
  • VIII.            Kupoteza hamu ya tendo la ndoa

Na mengine mengi.

Kupata hedhi ni kinyume cha ovulation katika mzunguko wa mwanamke. Ndio maana mwanamke anaweza akawa na hasira, kisirani au kua na mood swings kwa sababu ya homoni ya oestrogen.

Mwanamke yoyote hapasiw kutumia njia za uzazi wa mpango ambazo ni hormonal.

Na SAMUEL MACHA

Mwanzilishi wa FIT BY WAYNE.

Comments

Popular posts from this blog

DETOX YA SIKU 7. HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE

  HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE. Uzito Unaotakiwa kua nao Kulingana na Urefu Pamoja na Jinsia UREFU (CM) UREFU (FT & INCH) UZITO (KG)       MWANAUME MWANAMKE 147 4' 10" - 45-59 150 4' 11" - 45-60 152 5' 0" - 46-62 155 5' 1" 55-66 47-63 157 5' 2" 56-67 49-65 160 5' 3" 57-68 50-67 162 5' 4" 58-70 51-69 165 5' 5" 59-72 53-70 167 5' 6" 60-74 54-72 170 5' 7" 61-75 55-74 172 5' 8" 62-77 ...

BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI

 BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI.   ๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š   BAWASIRI NI NINI?   Bawasiri (kikundu, future, puru au mjiko ) ni hali ya kutuna kwa mishipa ya damu katika mfereji wa sehemu ya haja kubwa (anus). Kuna aina mbili za Bawasiri;   1. Bawasiri za ndani ( internal haemorroids )   2. Bawasiri za nje ( external haemorroids )  Bawasiri za ndani hua na dalili ya kupata kinyesi kilichokua na damu,  bawasiri za nje hua na dalili ya maumivu makali wakati wa kujisaidia pamoja na kinyama kutoka kwa nje.  NINI VISABABISHI VYA BAWASIRI?   1๏ธโƒฃHistoria ya familia, mara nyingi baadhi ya familia hukumbwa na changamoto hii. Na hua watu wa familia hiyo husika wanakua na hili tatizo. 2๏ธโƒฃKupata choo kigumu mara kwa mara husababisha mtu kutumia nguvu nyingi (straining) ambayo husababisha bawasiri kutokea. 3๏ธโƒฃUnene (uzito uliopitiliza) hua ni kisababishi cha bawasiri kwa sababu ya kuongezeka kwa Rectal Vein Pressure. 4๏ธโƒฃKu...

CALORIE ZA VYAKULA VYA TANZANIA

 CALORIES ZA VYAKULA TANZANIA   NINI MAANA YA CALORIE?    Calorie ni kiasi cha nishati kinachohitajika ili kuongeza joto la gramu moja ya maji (ยฐC). Kwa lugha nyepesi, calorie katika chakula hutoa nishati (energy) kwa njia ya joto ili miili yetu iweze kufanya kazi. Hii ni kwa sababu miili yetu huhifadhi na kuchoma calorie kama mafuta.  UHUSIANO WA CALORIE NA UZITO WA MWILI.  Kwa kawaida, kila chakula kina kiwango chake cha calorie. Hivyo unapokula chakula, unaingiza mwilini calorie kadhaa, na mwili wako pia unatumia calorie katika kuweka uhai. Lakini unapokula chakula, unaingiza calorie mwilini. Na mwili wako pia unatumia calorie kama nishati. Hivyo unapokula calorie nyingi kuliko mwili unavyoweza kutumia, zinahifadhiwa kama mafuta na utaongezeka uzito. Unapotumia calorie nyingi kuliko unavyoingiza mwilini, unapungua uzito. Na ukitumia kiasi sawa na unachoingiza, basi unabaki na uzito ule ule.   MWANADAMU ANAHITAJI WASTANI WA CALORIE NGAPI? ...