Skip to main content

Posts

Umuhimu Wa Kufunga Kula na Jinsi ya Kufunga Ipasavyo

  Kufunga Kula Kuna Faida Gani? Kufunga kula kulianza tangu enzi za kale. Hata wanadamu walioshi miaka mingi iliyopita walifunga kwa sababu mbali mbali. Hivi ni nani ambae alisema ya kwamba mwanadamu anatakiwa kula mara tatu kwa siku? Umeshawahi kujiuliza swali hilo? Je, kuna sababu za msingi zinazomfanya mwanadamu ale mara tatu kwa siku, na kuna faida gani endapo atakula pungufu ya hapo? Wagiriki wa kale waliamini ya kwamba kufunga huongeza uwezo wa utambuzi (cognitive ability). Wanafalsafa wengi waliamini ya kwamba kufunga kula ni moja wapo ya tiba katika mwili. Hippocrates ambae ni Baba wa Tiba (father of medicine) aliwaagiza wagonjwa wake wafunge kula ikiwa njia ya kwanza ya tiba kwao kabla ya kuwapa dawa yoyote ile. Hippocrates alisema " To eat when you are sick is to feed your illness" ikiwa na maana ya kwamba " kula chakula wakati ni mgonjwa ni sawa na kuulisha ugonjwa" Mwanafalsafa aitwaye Plutarch pia alisema " Instead of using medicine, better fast...

Kati ya Nyama Inayofuatwa na Nzi, Au Isiyofuatwa na Nzi, Ununue Ipi?

  Nyama Inayofuatwa na Nzi Au Isiyofuatwa na Nzi. Ununue Ipi? karibia kila mtu ameshawahi au hua ananunua nyama Buchani au sehemu nyingine yoyote kwa ajili ya matumizi ya kula. Lakini kuna sehemu au Bucha ambazo nyama hufuatwa na nzi japokua bucha ni safi tu. Utaona tu kua muuza bucha anafukuza nzi mara kwa mara. Vilevile, kwenye bucha nyingi za kisasa pamoja na supermarkets, hua wananyama ambazo zinavutia sana machoni na ni safi, lakini hamna hata nzi mmoja anatua kwenye nyama hiyo, na hata akitua, basi hatathubutu kurudi tena. Je ni kwanini? Je, ununue Nyama Ipi? Kabla ya yote, USINUNUE NYAMA SUPERMARKET AU KWENYE BUCHA AMBAYO HAMNA NZI ANAYESOGEA. Ni kwa nini? Nyama hizi hutunzwa kwa kutumia Dutu (substance) hatarishi ijulikanayo kwa jina la Sodium Metabisulfite  Japokua taasisi nyingi duniani husema ya kwamba ni salama. Lakini jiulize... Je, ni salama kweli? kama wadudu kama nzi wanaikimbia, Je inafaa kwa matumizi ya mwanadamu? Mara nyingi wanyama au wadudu hua wanauwezo w...

Faida 8 Za Kutumia Majani Ya Nanaa (Mint Leaves)

  Faida Za Kutumia Majani ya Nanaa (Mint leaves). Majani ya nanaa hutumika kwa sababu mbali mbali duniani, wengi wakiwa wanatumia kama kiungo katika mapishi, dawa za meno hutumia majani haya kwa ajili ya kuleta harufu nzuri kwenye kinywa na kuzuia ukuaji wa bakteria kwenye meno na sababu nyingine nyingi. Zifuatazo ni faida zinazopatikana kwa kutumia majani ya Nanaa (mint) ki afya. Faida za Kutumia Majani ya Nanaa (Mint) 1. Hutibu Matatizo ya Tumbo Mint husaidia kutibu matatizo mbalimbali ya tumbo pamoja na kusaidia mmeng`enyo wa chakula na hivyo kuondokana na shida ya kukosa choo au kupata choo kigumu. 2. Hupandisha Kinga ya Mwili Kutokana na kua na wingi wa madini ya Phosphorus, calcium pamoja na Vitamin A,C,D na E ambazo huongeza kinga ya mwili kwa kulinda seli za mwili kutoka kwenye uharibifu. 3. Huondoa Chunusi Kwenye Ngozi Kutokana na tabia yake ya kua anti-inflammatory pamoja na anti-bacterial, majani ya nanaa husaidia kulainisha ngozi na kuondoa chunusi. Pia yana salicylic a...

Madhara 7 Yanayowapata Wanawake Wanene

  Madhara 7 Yanayowapata Wanawake Wanene. Unene au uzito uliopitiliza una madhara kwa jinsia zote mbili, wanaume na wanawake, Ingawa kwa wanawake hupata madhara makubwa zaidi ukilinganisha na wanaume. Madhara Yanayowapata Wanawake Wanene. 1. Kushindwa Kubeba Ujauzito Wanawake wanene hupata changamoto nyingi zinazoathiri kizazi kama vile Polycistic Ovarian Syndrom ijulikanayo kama PCOS, Mji wa mimba kuzungungwa na mafuta au kuvurugika kwa hedhi inayosababishwa na kuvurugika kwa homoni. 2. Kupata Shida Wakati Wa Kujifungua Wengi hupata tabu katika kusukuma mtoto au mtoto kua mkubwa (macrosomia). Hii husababishwa na uchochezi wa insulini kwa kiumbe kinachokua tumboni mwa mama kutokana na ulaji mbovu wa mama kwa muda mrefu. 3. Neuroticism (kutokua sawa kisaikolojia) Mara nyingi hawa huwa na hasira za mara kwa mara, kujiona hawana thamani, kukosa kujiamini, kua na hisia hasi wakati mwingi, kua na ugomvi n.k. Hua wanajihisi kama vile kila mtu anawaona ni wabaya kutokana na miili yao iliv...

Vyakula 8 Vinavyosaidia Kusafisha Damu Kwa Asili

  Vyakula 8 Vinavyosaidia Kusafisha Damu Kwa Asili. Mara zote huwa tunavuta hewa, tunakula pamoja na kunywa kemikali za hatari na kuingiza katika miili yetu. Miili yetu hua inafanana sana na injini mfano magari. Gari ni lazima ulifanyie service kama vile kubadilisha oil n.k kila baada ya muda flani. Vivyo hivyo na miili yetu, ni lazima kujifunza kuisafisha na kuondoa taka mwili ambazo huingia kupitia njia mbali mbali kila siku. Katika mlo wako wa kila siku, kuna vyakula unaweza kuviongeza na vikasaidia sana kusafisha mwili wako kuanzia ndani. 1. Giligilani Majani ya giligilani Zina wingi wa vitakasa sumu ( antioxidants ) pamoja na Vitamin A, K pamoja na C, husaidia moyo, Figo pamoja na Ini kuondoa taka mwili ambazo hujishikiza humo. Mafuta yaliyomo kwenye giligilani ( volatile Oil ) husawazisha seli zinazosababisha saratani. Juisi ya giligilani husaidia sana afya ya macho pamoja na kuzuia uono hafifu wa macho kwa kuongeza mtiririko wa damu kwenye mishipa midogo midogo kwenye macho....

MADHARA 6 MAKUBWA YATOKANAYO NA KUNYWA SODA.

  MADHARA 6 MAKUBWA YATOKANAYO NA KUNYWA SODA. Soda hua ni kinywaji chenye sukari nyingi sana na kisicho na faida yoyote mwilini. (No nutritional value) ingawa watu wengi hupendelea kutumia katika nyakati tofauti. Soda ni kinywaji chenye madhara mengi sana mwilini kuliko faida, na ni kinywaji ambacho ni vyema kukiepuka, ingawa watu wengi hupendelea hata kuwapa watoto watumie bila kujua ya kwamba wanahatarisha maisha yao ya sasa na baadae. MADHARA YATOKANAYO NA KUNYWA SODA. Ugonjwa wa Kimetabiliki (metabilic Syndrome) : Matumizi ya Soda moja kwa siku huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari kwa asilimia 67% Afya ya Ngozi kudhoofika : Soda hua na kemikali inayoitwa Flame-Retardant Brominated Vegetable Oil (BVO ), ni kemikali inayodhoofisha afya ya ngozi pamoja na mfumo wa neva za fahamu.  Huongeza Kasi ya Uzee : Soda ina Phosphate pamoja na Phosphoric acid ambazo hutumika kufanya soda zikae muda mrefu bila kuharibika. Ila husababisha kuongezeka kwa kasi ya uzee na kusinya...

MKAKATI WA KUIMARISHA AFYA YAKO MWAKA 2022

  UNA MKAKATI GANI ILI KUIMARISHA AFYA YAKO? kuna msemo hua napenda sana kuutumia, ya kwamba  MJI WA ROMA HAUKUJENGWA KWA SIKU MOJA. Hii inamaanisha ya kwamba, afya ya mtu ilivyo, ni matokeo ya alivyozoea kula kwa kipindi cha muda flani. Hamna mtu aliyenenepa kwa siku moja, wala aliyepungua kwa siku moja. ila vyote huhusisha mazoea ya namna flani ambayo ndio husababisha mtu kua na afya ya namna flani. Mara nyingi watu hupenda sana kupungua ndani ya muda mfupi, tena bila kuweka juhudi katika kupungua, lakini wanasahau ya kwamba, hata unene walionao haukuja kwa muda mfupi. Bali umechukua muda flani wao kufikia unene huo waliokua nao. Ili uweze kua na uzito sahihi (uzito sahihi hukufanya kuepukana na magonjwa mengi yasioambukizwa ambayo ni hatarishi), Ni lazima uanze kufanya baadhi ya vitu. lakini sio kufanya tu, inabidi viwe tabia yako ya kila siku. Na endapo vitu hivyo vikiwa tabia, basi ndani ya muda flani Afya yako itaimarika zaidi na zaidi. TABIA 10 AMBAZO ZITAKUWEZESHA KUA ...