UNA MKAKATI GANI ILI KUIMARISHA AFYA YAKO?
kuna msemo hua napenda sana kuutumia, ya kwamba MJI WA ROMA HAUKUJENGWA KWA SIKU MOJA.
Hii inamaanisha ya kwamba, afya ya mtu ilivyo, ni matokeo ya alivyozoea kula kwa kipindi cha muda flani. Hamna mtu aliyenenepa kwa siku moja, wala aliyepungua kwa siku moja. ila vyote huhusisha mazoea ya namna flani ambayo ndio husababisha mtu kua na afya ya namna flani.
Mara nyingi watu hupenda sana kupungua ndani ya muda mfupi, tena bila kuweka juhudi katika kupungua, lakini wanasahau ya kwamba, hata unene walionao haukuja kwa muda mfupi. Bali umechukua muda flani wao kufikia unene huo waliokua nao.
Ili uweze kua na uzito sahihi (uzito sahihi hukufanya kuepukana na magonjwa mengi yasioambukizwa ambayo ni hatarishi), Ni lazima uanze kufanya baadhi ya vitu. lakini sio kufanya tu, inabidi viwe tabia yako ya kila siku. Na endapo vitu hivyo vikiwa tabia, basi ndani ya muda flani Afya yako itaimarika zaidi na zaidi.
TABIA 10 AMBAZO ZITAKUWEZESHA KUA NA UZITO SAHIHI/KUIMARIKA KWA AFYA.
- Kunywa maji mengi zaidi ya ulivyozoea. walau lita 2 kila siku. (jitahidi kuongeza zaidi ya ulivyozoea)
- Punguza matumizi ya wanga ambao umekobolewa, na uongeze matumizi ya wanga ambao haujakobolewa
- Punguza matumizi ya sukari pamoja na vitu vinavyotengenezwa na sukari. (sukari huongeza uzito zaidi kuliko hata mafuta)
- Fanya mazoezi walau mara 3 kwa wiki. (unaweza ukawa unatembea hata nusu saa tu kwa siku)
- Kula matunda na mboga za majani kila siku (hakikisha haukosi)
- Pata muda wa kulala walau kwa saa 8 kila siku.
- Jitahidi sana kutoa kipaombele kwa vyakula vyenye Protini pamoja na nyuzinyuzi.
- Tumia sahani ndogo unapopakua chakula (sahani ndogo itaiambia akili yako ya kwamba chakula ni kingi na utashiba haraka)
- Usikae muda mrefu sana sehemu moja bila kusogea kidogo na kujinyoosha.
- Ikitokea mara kadhaa umeenda nje ya ratiba yako nzuri ya kula, usijali, wewe kesho yake endelea na tabia yako ile ile ya kutengeneza afya yako.
Mara nyingi watu wamekua wakisema ya kwamba Diet ni gharama. lakini ukweli ni kwamba, magonjwa yatokanayo na mlo mbovu au mtindo mbovu wa maisha ni kubwa zaidi.
PROGRESS OVER PERFECTION, yawezekana usiweze kufanya mambo yote hayo kwa wakati mmoja. lakini kila siku jitahidi kua bora kuliko jana.
Nikutakie mwaka mwema wenye kuimarisha afya yako zaidi.
Imeandikwa na SAMUEL MACHA
FIT BY WAYNE.
Asante mwl mungu aendelee kukupa nguvu
ReplyDeleteAmen, na kwako pia
Delete