Nyama Inayofuatwa na Nzi Au Isiyofuatwa na Nzi. Ununue Ipi?
karibia kila mtu ameshawahi au hua ananunua nyama Buchani au sehemu nyingine yoyote kwa ajili ya matumizi ya kula.
Lakini kuna sehemu au Bucha ambazo nyama hufuatwa na nzi japokua bucha ni safi tu. Utaona tu kua muuza bucha anafukuza nzi mara kwa mara.
Vilevile, kwenye bucha nyingi za kisasa pamoja na supermarkets, hua wananyama ambazo zinavutia sana machoni na ni safi, lakini hamna hata nzi mmoja anatua kwenye nyama hiyo, na hata akitua, basi hatathubutu kurudi tena. Je ni kwanini?
Je, ununue Nyama Ipi?
Kabla ya yote, USINUNUE NYAMA SUPERMARKET AU KWENYE BUCHA AMBAYO HAMNA NZI ANAYESOGEA.
Ni kwa nini?
Nyama hizi hutunzwa kwa kutumia Dutu (substance) hatarishi ijulikanayo kwa jina la Sodium Metabisulfite
Japokua taasisi nyingi duniani husema ya kwamba ni salama. Lakini jiulize... Je, ni salama kweli? kama wadudu kama nzi wanaikimbia, Je inafaa kwa matumizi ya mwanadamu?
Mara nyingi wanyama au wadudu hua wanauwezo wa kutambua kitu ambacho hakifai kwa matumizi, ndio maana hunusa kwanza, wakiona hakifai basi hawali.
Nyama inatakiwa itumike ikiwa fresh, Sio ambayo inaweza kukaa wiki nzima au zaidi bila kuharibika.
Hivyo ni bora ununue nyama katika bucha za kawaida ili kupata nyama fresh. Au ukiweza zaidi nunua sehemu ya machinjio ili kujihakikishia uhakika wa kupata nyama fresh.
Comments
Post a Comment