MADHARA 6 MAKUBWA YATOKANAYO NA KUNYWA SODA.
Soda hua ni kinywaji chenye sukari nyingi sana na kisicho na faida yoyote mwilini. (No nutritional value) ingawa watu wengi hupendelea kutumia katika nyakati tofauti.
Soda ni kinywaji chenye madhara mengi sana mwilini kuliko faida, na ni kinywaji ambacho ni vyema kukiepuka, ingawa watu wengi hupendelea hata kuwapa watoto watumie bila kujua ya kwamba wanahatarisha maisha yao ya sasa na baadae.
MADHARA YATOKANAYO NA KUNYWA SODA.
- Ugonjwa wa Kimetabiliki (metabilic Syndrome): Matumizi ya Soda moja kwa siku huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari kwa asilimia 67%
- Afya ya Ngozi kudhoofika: Soda hua na kemikali inayoitwa Flame-Retardant Brominated Vegetable Oil (BVO), ni kemikali inayodhoofisha afya ya ngozi pamoja na mfumo wa neva za fahamu.
- Huongeza Kasi ya Uzee: Soda ina Phosphate pamoja na Phosphoric acid ambazo hutumika kufanya soda zikae muda mrefu bila kuharibika. Ila husababisha kuongezeka kwa kasi ya uzee na kusinyaa kwa ngozi.
- Husababisha mishipa ya damu kukakamaa na kua migumu: kutokana na kuongezeka kwa mafuta ya Triglycerides kwa asilimia 30% pale unapokunywa soda moja kwa siku.
- Huharibu Ubongo: soda ina mchanganyiko wa rangi za chakula (food dye), sukari nyingi ambayo ni aspartame. Hizi hua ni sumu katika seli za ubongo.
- Unyeti wa meno (Tooth sensitivity) na Kuharibika kwa meno: soda zina Phosphoric acid pamoja na citric acid ambazo hubadilisha uwiano wa pH katika mdomo na kupelekea kuharibika kwa enamel ambayo inalinda jino.
Ni vyema kufanya maamuzi sahihi, hata kama wewe hujali afya yako, basi jitahidi usiwazoeshe watoto wako kunywa soda. Maji yanabaki kua kinywaji bora zaidi kuliko vyote.
Unapoenda ugenini, ukikaribishwa soda, hamna dhambi yoyote ukaomba maji. Sio lazima unywe soda unapokaribishwa, unaweza kuomba maji na ukafurahia afya yako.
Comments
Post a Comment