UKOSEFU WA HAMU YA TENDO LA NDOA low sex drive Ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa ni changamoto ambayo inawakumba watu wengi, wanaume kwa wanawake katika wakati flani wa maisha yao. Ingawa visababishi vyake vinaweza kutofautiana baina ya mtu na mtu, Afya njema ya maisha ya tendo la ndoa hutegemea sana ulaji mzuri, ufanyaji kazi mzuri wa mishipa ya fahamu, kiwango sahihi cha vichochezi (hormones) pamoja na damu kuzunguka vizuri kwenye mishipa iliyopo maeneo ya pelvis (kwenye nyonga). VISABABISHI VYA UKOSEFU WA HAMU YA TENDO LA NDOA KWA WANAWAKE Matatizo ya Uzazi: kama vile maumivu wakaji wa tendo, Baadhi ya magonjwa: kama vile saratani, kisukari, shinikizo la juu la damu (hypertension), Baadhi ya dawa: kama vile anti depressants husababisha ukosefu huu. Upasuaji: wa sehemu ya matiti au maeneno ya sehemu za siri. Uchovu: majukumu mengi ya kina mama huwafanya wachoke sana na hivyo kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa. Kukoma kwa hedhi (menopause): kipindi hiki estrogen hupungua sana
Blog hii ni kwa ajili ya kukusaidia kutatua changamoto za ki afya ambazo zinaweza kutatulika kwa kubadilisha jinsi ya kula na mtindo wa maisha