Skip to main content

APPLE CIDER VINEGER KWENYE KUPUNGUZA UZITO.

 

Apple Cider Vineger

UKWELI KUHUSU APPLE CIDER VINEGER KUPUNGUZA UZITO.

Kwa miaka mingi, Apple cider vineger (siki ya tufaa) ilikua ikitumika kama dawa ya vitu vingi kama vile kupunguza kiwango cha sukari mwilini pamoja na kupunguza kiwango cha lehemu n.k

Japokua hamna tafiti za moja kwa moja zinazohusisha siki ya tufaa kupunguza uzito, watu watu kadhaa ambao wanasema imewasaidia kwa kiasi flani ukilinganisha na ambao hawakua wakitumia siki ya tufaa.

BAADHI YA FAIDA ZITOKANAZO NA KUTUMIA SIKI YA TUFAA.

  1. Husaidia kuweka sawa mmeng,enyo wa chakula
  2. Husaidia kushusha kiwango cha sukari kwa wenye kisukari
  3. Husaidia kupunguza lehemu mbaya (bad cholesterol)
  4. Husaidia kuondoa kiungulia
  5. Inasaidia kufanya detox
  6. Na faida nyingine nyingi
JINSI YA KUTUMIA SIKI YA TUFAA (APPLE CIDER VINEGER) KUPUNGUZA UZITO.

  • Andaa glass au kikombe kimoja cha maji ya kunywa.
  • weka vijiko viwili vya chakula vya maji ya limao/ndimu
  • weka vijiko viwili vya chakula vya Apple Cider Vineger
  • weka kijiko kimoja cha chakula cha asali mbichi.
MATUMIZI

changanya mchanganyiko huu kwenye glass au kikombe cha maji na kisha unywe usiku walau saa moja kabla ya kwenda kulala.

ANGALIZO

Hamna ushahidi mkubwa wa kisayansi unaosema kua hii ni njia ya kupungua uzito, lakini wapo watu ambao njia hii imewasaidia. Matokeo huweza kutofautiana baina ya mtu na mtu.

Njia nzuri zaidi ya kupunguza uzito ni kwa kuzingatia mlo sahihi kila siku na kua na mtindo wa maisha ambao unajenga afya yako zaidi.

Comments

Popular posts from this blog

DETOX YA SIKU 7. HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE

  HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE. Uzito Unaotakiwa kua nao Kulingana na Urefu Pamoja na Jinsia UREFU (CM) UREFU (FT & INCH) UZITO (KG)       MWANAUME MWANAMKE 147 4' 10" - 45-59 150 4' 11" - 45-60 152 5' 0" - 46-62 155 5' 1" 55-66 47-63 157 5' 2" 56-67 49-65 160 5' 3" 57-68 50-67 162 5' 4" 58-70 51-69 165 5' 5" 59-72 53-70 167 5' 6" 60-74 54-72 170 5' 7" 61-75 55-74 172 5' 8" 62-77 ...

FANYA HIVI KAMA UNASUMBULIWA NA CHUNUSI

  FANYA HIVI KAMA UNASUMBULIWA NA CHUNUSI. Chunusi ni vimbe zinazosababishwa na kuzibika kwa folikoli za nywele na mafuta ya ngozi (sebum), seli za ngozi zilizokufa, na protini zilizokufa. Kuziba huku kunavuta bakteria wa ngozi ambao husababisha uvimbe na kuongezeka kwa vimbe hizi. Sebum ni dutu yenye mafuta inayozalishwa na tezi za mafuta kwenye ngozi yako. Sebum inalinda ngozi, lakini unapozalishwa kupita kiasi, inaweza kuziba njia za ngozi, kufunga seli za ngozi zilizokufa, na kuvuta bakteria wa ngozi, hivyo kusababisha uvimbe na chunusi.   Uzalishaji wa sebum kupita kiasi unatokana na homoni za ngono zinazosambaa sana kwenye damu. Hii ndiyo sababu chunusi ni kawaida kwa vijana na watu wazima vijana. Protini inayojulikana kama Sex Hormone Binding Globulin (SHBG) inapunguza homoni za ngono zisizo na mpangilio.   SHBG inashikilia homoni hizi za ngono ili zisilete athari zisizohitajika kwenye seli na viungo kama ngozi. Homoni hizi za ngono ni estrogeni na testos...

BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI

 BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI.   💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊   BAWASIRI NI NINI?   Bawasiri (kikundu, future, puru au mjiko ) ni hali ya kutuna kwa mishipa ya damu katika mfereji wa sehemu ya haja kubwa (anus). Kuna aina mbili za Bawasiri;   1. Bawasiri za ndani ( internal haemorroids )   2. Bawasiri za nje ( external haemorroids )  Bawasiri za ndani hua na dalili ya kupata kinyesi kilichokua na damu,  bawasiri za nje hua na dalili ya maumivu makali wakati wa kujisaidia pamoja na kinyama kutoka kwa nje.  NINI VISABABISHI VYA BAWASIRI?   1️⃣Historia ya familia, mara nyingi baadhi ya familia hukumbwa na changamoto hii. Na hua watu wa familia hiyo husika wanakua na hili tatizo. 2️⃣Kupata choo kigumu mara kwa mara husababisha mtu kutumia nguvu nyingi (straining) ambayo husababisha bawasiri kutokea. 3️⃣Unene (uzito uliopitiliza) hua ni kisababishi cha bawasiri kwa sababu ya kuongezeka kwa Rectal Vein Pressure. 4️⃣Ku...