UKOSEFU WA HAMU YA TENDO LA NDOA
low sex drive |
Ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa ni changamoto ambayo inawakumba watu wengi, wanaume kwa wanawake katika wakati flani wa maisha yao.
Ingawa visababishi vyake vinaweza kutofautiana baina ya mtu na mtu, Afya njema ya maisha ya tendo la ndoa hutegemea sana ulaji mzuri, ufanyaji kazi mzuri wa mishipa ya fahamu, kiwango sahihi cha vichochezi (hormones) pamoja na damu kuzunguka vizuri kwenye mishipa iliyopo maeneo ya pelvis (kwenye nyonga).
VISABABISHI VYA UKOSEFU WA HAMU YA TENDO LA NDOA KWA WANAWAKE
- Matatizo ya Uzazi: kama vile maumivu wakaji wa tendo,
- Baadhi ya magonjwa: kama vile saratani, kisukari, shinikizo la juu la damu (hypertension),
- Baadhi ya dawa: kama vile anti depressants husababisha ukosefu huu.
- Upasuaji: wa sehemu ya matiti au maeneno ya sehemu za siri.
- Uchovu: majukumu mengi ya kina mama huwafanya wachoke sana na hivyo kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa.
- Kukoma kwa hedhi (menopause): kipindi hiki estrogen hupungua sana na baadhi hupoteza hamu kabisa na kua na uke mkavu.
- Ujauzito au wakati wa kunyonyesha: hua na mabadiliko ya hormones zinazoweza kupelekea kupungua kwa hamu.
- Matatizo ya kisaikolojia: kama vile historia ya unyanyasaji wa kijinsia, kujiona kua na shepu mbaya, pamoja na msongo wa mawazo, au ugomvi usioisha kwenye mahusiano.
VISABABISHI VYA UKOSEFU WA HAMU YA TENDO LA NDOA KWA WANAUME.
- Kupungua kwa Testosterone: Hii ndio hormone inayojulikana kwa UWANAUME
- Baadhi ya Dawa: mfano dawa za presha huchangia kupungua kwa Hamu ya tendo.
- Msongo wa mawazo: hupelekea kushuka kwa testosterone.
- Magonjwa: kama vile Kisukari, Shinikizo la juu la damu (pressure), matatizo ya figo na ini.
- Uzito uliopitiliza: ni moja ya visababishi vya upungufu wa nguvu za kiume.
- Kutokupata usingizi wa kutosha: hupelekea kushuka kwa testosterone.
- Uzee: kadri umri unavyozidi kwenda, kiwango cha testosteron hupungua.
- Unywaji wa pombe kupita kiasi.
- Uvutaji wa Sigara na dawa za kulevya.
- Kukosa kujiamini (kisaikolojia).
NINI CHA KUFANYA?
- Punguza matumizi ya wanga uliokobolewa: penda sana kutumia wanga ambao haujakobolewa, chakula jamii ya kunde, matunda pamoja na mboga mboga. Tumia pia kiwango cha kutosha cha protini. Matunda jamii ya machungwa ni mazuri kwa ajili ya Vitamin C ili kuimarisha kuta za mishipa ya damu. Mboga za majani zina Riboflavin kwa ajili ya kuleta ute kwenye uke wa mwanamke.
- Tumia Zinc: Husaidia sana katika mambo ya afya ya uzazi, inahusika hata katika utengenezwaji wa shahawa. Inapatikana zaidi kwa viumbe vya baharini (seafood), nyama, kuku, maini, mayai, maziwa, maharage, pamoja na nafaka ambazo hazijakobolewa.
- Punguza matumizi ya pombe: ukitumia kupita kiasi, husababisha kusinyaa kwa korodani na upotevu wa nguvu za kiume.
- Tumia madini ya chuma: hupatikana kwenye nyama, samaki, mbegu (karanga), jamii ya kunde, nafaka ambazo hazijakobolewa, matunda na mboga za majani.
- Tumia kitunguu swaumu kama kiungo: unga chakula chako bila kukosekana kwa kitunguu swaumu mara kwa mara. kina allicin inayosaidia katika mzunguko wa damu katika viungo vya uzazi kwa wanawake na wanaume.
- Fanya mazoezi: ili uzalishe hormone ya endorphin, kua na uzito sahihi pamoja na kusaidia mzunguko wa damu.
- Usivute Sigara: Nicotine ni adui wa mishipa ya damu. husababisha kutengenezeka kwa plaque kwenye mishipa ya kwenye uume pamoja na kusinyaa.
kwa msaada zaidi juu ya Tiba ya ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa/ urijali au upungufu wa nguvu za kiume. Tuwasiliane. Bonyeza HAPA kwa whatsapp.
MAWASILIANO:
0753068572 (Mobile)
0621068072 (whatsapp)
Imeandikwa na SAMUEL MACHA
FIT BY WAYNE.
Comments
Post a Comment