Obesity ama unene, uzito uliopitiliza ni ugonjwa unaohusisha mwili kua na mafuta mengi kuliko kiwango kinachotakiwa.
Hali hii sio kwamba inakupa mwonekano mbaya tu, bali ni hali inayoongeza hatari ya magonjwa kama vile magonjwa ya moyo, kisukari, shinikizo la juu la damu pamoja na aina kadhaa za saratani.
UTAJUAJE KAMA UZITO WAKO UMEZIDI? (OBESITY)
Wataalam walikuja na kitu kinachoitwa BODY MASS INDEX, (BMI). na wakaonyesha ya jinsi unavyoweza kujua kama una uzito sahihi kulingana na Urefu pamoja na uzito ulio nao.
FORMULAR YA BMI
BMI hutafutwa kwa kutumia uzito wako kwa kg pamoja na urefu wako kwa mita. hivyo kama una urefu mfano wa cm 170, basi utabadilisha ziende kua meter. ambapo cm 170 ni sawa na 1.7m
Hivyo BMI ni sawa na uzito wako kwa kg gawanya kwa mraba wa urefu kwa meter.
BMI = kg/m2
lakini ni rahisi zaidi kujua BMI yako kwa kutumia mtandao. utaenda sehemu ya Google na uandike BMI CALCULATOR. itakupeleka sehemu husika ya kupata BMI yako. Au bonyeza BMI CALCULATOR
au unaweza kupakua application kutoka playstore au appstore inayoitwa BMI calculator na kisha ukaitumia kupata BMI yako kwa urahisi.
chati ya BMI |
BMI | Hali ya Uzito |
---|---|
Pungufu ya 18.5 | uzito wa chini (Underweight) |
18.5-24.9 | Uzito wa kawaida (Normal) |
25.0-29.9 | Uzito uliopitiliza (Overweight) |
Zaidi ya 30.0 | Unene (Obesity) |
- Ulaji mbovu wa chakula: unapokula calorie nyingi kuliko mwili unavyochoma, hii husababisha kuongezeka kwa uzito, kitambi pamoja na nyama zembe.
- kutokushughulisha mwili: hii husababisha mwili kukusanya calorie nyingi bila kuzichoma, na matokeo yake kuhifadhiwa kama mafuta.
- Ujauzito: kwa baadhi ya wanawake ujauzito huwasababishia kuongezeka uzito.
- Kutokupata usingizi wa kutosha: hii hupelekea mabadiliko ya hormones kwenye mwili wako na kupelekea kunenepa.
- Msongo wa mawazo: pia husababisha mabadiliko ya hormones, hivyo kuongezeka uzito.
- Kutokuishi muda mrefu kwa ujumla (mortality): tafiti zinaonyesha ya kwamba, watu wenye uzito mkubwa huishi muda mfupi zaidi ukilinganisha na watu wenye uzito sahihi.
- Shinikizo la juu la damu (High blood pressure)
- Kiwango kikubwa cha lehemu mbaya (LDL Cholesterol)
- Kisukari
- Ugonjwa wa moyo
- Kiharusi (stroke)
- Mawe kwenye kibofu cha mkojo
- Matatizo ya mifupa na viungio (joints and bone problems)
- Kukoroma wakati wa kulala na kushindwa kuhema vizuri wakati wa kulala.
- Saratani za aina mbali mbali
- Maumivu ya mwili na kupata shida kufanya movements za kawaida.
- Na matatizo mengine mengi ambayo utaona yakiondoka pale ambapo mwili wako utakua na uzito wa kawaida.
- Punguza kiwango cha calorie: ukiweza kuongezea na mazoezi walau nusu saa kwa siku, hii itakusaidia kupunguza kilo 0.5 hadi 0.9 katika kila wiki.
- Usiache kupata Breakfast: tafiti zinaonyesha ya kwamba, watu waliokua wakipata breakfast walikua na uzito wa kilo 2.7 pungufu kuliko waliokua wanaruka breakfast kwa wanaume, na pungufu ya kilo 4 kwa wanawake.
- Tumia vyakula vyenye nyuzi nyuzi zaidi: hii ni kuacha kutumia vyakula vya wanga uliokobolewa na kutumia vyakula vya wanga ambao haujakobolewa.
- Tumia mboga mboga zaidi: unapopakua chakula chako, jaza zaidi mboga mboga na matunda kuliko wanga.
- Tumia vyakula vya protini katika kila mlo: sio lazima iwe protini ya wanyama ili kupunguza gharama, unaweza hata kutumia protini zitokanazo na mimea. kama vile maharage, mbaazi, kunde, njegere n.k
- Shughulisha mwili zaidi: hapa ni kuhakikisha unaweza kutembea zaidi badala ya kutumia usafiri au kitu kinachokusaidia kusogea, unaweza ukawa unatumia ngazi badala ya lift, ukienda kazini gari lako paki mbali kidogo ili uweze kutembea, tembea tu kwa dk 15 asubuhi na 15 jioni. au ukatembea kwa dk 30 kwa wakati mmoja, penda kufanya vitu mwenyewe badala ya kutuma wasaidizi n.k
- Fanya mazoezi walau mara 3 kwa wiki.
🙏🙏🙏🙏🙏🙏
ReplyDeleteAsante kwa ushauri wako...
ReplyDeleteMungu akubariki
ReplyDeleteMasomo mazuri.
ReplyDelete