SHINIKIZO LA JUU LA DAMU/HIGH BLOOD PRESSURE
Shinikizo la juu la damu(hypertension) |
NINI MAANA YA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU?
kwa kawaida, inasemekana mtu ana shinikizo la juu la damu kama pressure yake kwenye vipimo ni kuanzia 140/90 mmhg au zaidi.
Na hua inasemekana kua pressure imezidi sana kama pressure yake kwenye vipimo ni zaidi kuanzia 180/120 mmhg au zaidi.
Kwa kawaida mtu anaweza asionyenye dalili za kua na pressure mwanzoni, ila ikiendelea kwa muda flani bila kufanya juhudi za kuishusha, basi atapata magonjwa ya moyo na ndipo ataanza kuonyesha dalili za kua na pressure.
Na kama dalili zikitokea, basi hua ni kusumbuliwa na maumivu ya kichwa mara kwa mara, kukosa pumzi, kutokwa na damu puani.
NINI HUSABABISHA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU?
kuna baadhi ya magonjwa au sababu za kiafya zinazoweza kusababisha shinikizo la juu la damu, kama vile magonjwa ya figo, utumiaji wa dawa hatarishi, matatizo ya adrenal gland, matatizo ya thyroid n.k.
lakini sababu kuu hua ni zile za hatari ya ugonjwa huu, yaani risk factors.
Athari za High blood pressure |
ATHARI ZA SHINIKIZO LA DAMU
- Magonjwa ya moyo: kama vile stroke, heart attack, heart failure (kufeli kwa moyo)
- Matatizo ya nguvu za kiume
- Matatizo ya figo au kufeli kwa figo
- Matatizo ya macho na kutokuona vizuri
SABABU ZA HATARI (RISK FACTORS) ZA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU.
- Umri: mara nyingi kuanzia umri wa miaka 64 kwa wanume na 65 kwa wanawake, hua ndio matatizo ya pressure hujitokeza.
- Historia ya familia: mara nyingi familia zenye matatizo ya pressure hupelekea na vizazi vyao kua na hayo matatizo. (ni vizuri kujikinga mapema)
- Unene au uzito uliopitiliza: kadri ambavyo uzito wako ni mkubwa, ndivyo ambavyo damu nyingi huhitajika kwa nguvu ili kupeleka oksijeni na chakula kwenye tishu zako za mwili. Hivyo kupelekea shinikizo la juu la damu.
- Kutokushughulisha mwili: Hii hupelekea kua na heart rate kubwa ambayo hupelekea kua na shinikizo la juu la damu, pia kutokushughulisha mwili hupelekea kua na uzito mkubwa.
- Matumizi ya chumvi nyingi (sodium): Hii hupelekea mwili wako ku retain maji ndani yake, na hivyo kupelekea shinikizo la juu la damu.
- Matumizi makubwa ya pombe:Pombe inapozidi kiwango hua na kawaida ya kuharibu figo, pia na moyo.
- Msongo wa mawazo (stress): unapokua na stress, hufanya msukumo wa damu kupanda. Hivyo unapokua na stress mara kwa mara, hupelekea kua na hatari ya shinikizo la juu la damu.
JINSI YA KUONDOKANA NA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU
Ikumbukwe ya kwamba, kama tayari una huu ugonjwa, basi ni vyema kwenda hospitali na kuanza matibabu. ili kama kuna tatizo jingine lolote basi uweze kutibiwa.
Nitakavyovielezea hapa, kama mtu yupo kwenye dalili za awali, basi anaweza kupona kabisa na kuondokana na tatizo hilo, lakini kama ni hali iliyofika mbali, haimaanishi uache kutumia dawa, ila tu ni kwamba ukifwata maelekezo haya, inaweza kutokea ukapata nafuu kiasi kwamba ukawa huhitaji tena dawa za hospitali.
- Tumia nafaka ambazo hazijakobolewa: hizi zina virutubisho pamoja na fiber za kutosha.
- Tumia matunda na mboga za majani kwa wingi: Hakikisha kila siku au katika kila mlo hukosi mboga za majani pamoja na matunda. mfano karoti, mboga zenye majani, viazi vitamu, n.k
- Punguza matumizi ya nyama na samaki (iwe gram 170 kwa siku): na ikitokea unakula, basi usitumie zenye mafuta.
- Punguza matumizi ya mafuta kwenye chakula
- Punguza matumizi ya sukari na vitu vya sukari
- Punguza matumizi ya chumvi: pia epukana sana na vyakula vya kiwandani (processed foods) kwa sababu hua vinatengenezwa kwa chumvi nyingi (sodium)
- Pata madini ya potassium ya kutosha: kwa sababu madini haya husaidia kubalance kiwango cha maji na chumvi mwilini. hupatikana kwenye vyakula kama vile matunda na mboga mboga hususani ndizi mbivu, maziwa na jamii ya kunde.
- Punguza matumizi ya pombe na caffein (acha kama ukiweza)
PIA ZINGATIA YAFUATAYO
- Fanya mazoezi: husaidia kupunguza pressure kwa kufanya moyo ufanye kazi kwa ufanisi zaidi, pia itakusaidia kupunguza uzito.
- Punguza uzito kama ni mnene: kupungua kwa uzito kutafanya kushuka kwa shinikizo la damu.
- Acha kuvuta sigara: nicotine husababisha kuongezeka kwa shinikizo la juu la damu.
- Jitahidi kuepukana na msongo wa mawazo: stress husababisha kuzalishwa kwa adrenal hormones ambazo hupelekea kuongezeka kwa shinikizo la damu.
- Usitumie dawa bila ushauri wa wataalam: kuna baadhi ya dawa husababisha shinikizo la damu kupanda.
VYAKULA VYENYE MANUFAA
- mboga za majani
- maziwa ya low fat
- jamii ya kunde
- matunda haswa haswa ndizi mbivu
- nafaka ambazo hazijakobolewa
- karoti
- viazi vitamu
VYAKULA VYA KUTUMIA KWA KIASI
- Vyakula vyenye mafuta
- pombe
- caffein
VYAKULA VYA KUEPUKA/VYENYE MADHARA
- chumvi pamoja na vyakula vya kiwandani (processed foods)
Comments
Post a Comment