Skip to main content

NINI MKAKATI WAKO WA KUA NA UZITO SAHIHI/AFYA BORA MWAKA 2021?

 

UNA MKAKATI GANI ILI KUA NA UZITO SAHIHI 2021?

kuna msemo hua napenda sana kuutumia, ya kwamba MJI WA ROMA HAUKUJENGWA KWA SIKU MOJA.

Hii inamaanisha ya kwamba, afya ya mtu ilivyo, ni matokeo ya alivyozoea kula kwa kipindi cha muda flani. Hamna mtu aliyenenepa kwa siku moja, wala aliyepungua kwa siku moja. ila vyote huhusisha mazoea ya namna flani ambayo ndio husababisha mtu kua na afya ya namna flani.

Mara nyingi watu hupenda sana kupungua ndani ya muda mfupi, tena bila kuweka juhudi katika kupungua, lakini wanasahau ya kwamba, hata unene walionao haukuja kwa muda mfupi. Bali umechukua muda flani wao kufikia unene huo waliokua nao.

Ili uweze kua na uzito sahihi (uzito sahihi hukufanya kuepukana na magonjwa mengi yasioambukizwa ambayo ni hatarishi), Ni lazima uanze kufanya baadhi ya vitu. lakini sio kufanya tu, inabidi viwe tabia yako ya kila siku. Na endapo vitu hivyo vikiwa tabia, basi ndani ya muda flani Afya yako itaimarika zaidi na zaidi.

TABIA 10 AMBAZO ZITAKUWEZESHA KUA NA UZITO SAHIHI/KUIMARIKA KWA AFYA.

  1. Kunywa maji mengi zaidi ya ulivyozoea. walau lita 2 kila siku. (jitahidi kuongeza zaidi ya ulivyozoea)
  2. Punguza matumizi ya wanga ambao umekobolewa, na uongeze matumizi ya wanga ambao haujakobolewa 
  3. Punguza matumizi ya sukari pamoja na vitu vinavyotengenezwa na sukari. (sukari huongeza uzito zaidi kuliko hata mafuta)
  4. Fanya mazoezi walau mara 3 kwa wiki. (unaweza ukawa unatembea hata nusu saa tu kwa siku)
  5. Kula matunda na mboga za majani kila siku (hakikisha haukosi)
  6. Pata muda wa kulala walau kwa saa 8 kila siku.
  7. Jitahidi sana kutoa kipaombele kwa vyakula vyenye Protini pamoja na nyuzinyuzi.
  8. Tumia sahani ndogo unapopakua chakula (sahani ndogo itaiambia akili yako ya kwamba chakula ni kingi na utashiba haraka)
  9. Usikae muda mrefu sana sehemu moja bila kusogea kidogo na kujinyoosha.
  10. Ikitokea mara kadhaa umeenda nje ya ratiba yako nzuri ya kula, usijali, wewe kesho yake endelea na tabia yako ile ile ya kutengeneza afya yako.
Nipende tu kusema ya kwamba, MWILI WAKO NDIO SEHEMU PEKEE AMBAYO UNAISHI, NI VIZURI KUWEKA AFYA YAKO VIZURI.

Mara nyingi watu wamekua wakisema ya kwamba Diet ni gharama. lakini ukweli ni kwamba, magonjwa yatokanayo na mlo mbovu au mtindo mbovu wa maisha ni kubwa zaidi.

PROGRESS OVER PERFECTION, yawezekana usiweze kufanya mambo yote hayo kwa wakati mmoja. lakini kila siku jitahidi kua bora kuliko jana.

Nikutakie mwaka mwema wenye kuimarisha afya yako zaidi.

Imeandikwa na SAMUEL MACHA

FIT BY WAYNE.

Kwa msaada zaidi juu ya kua na uzito sahihi,

whatsapp BOFYA HAPA

Mobile 0753068572







Comments

Popular posts from this blog

DETOX YA SIKU 7. HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE

  HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE. Uzito Unaotakiwa kua nao Kulingana na Urefu Pamoja na Jinsia UREFU (CM) UREFU (FT & INCH) UZITO (KG)       MWANAUME MWANAMKE 147 4' 10" - 45-59 150 4' 11" - 45-60 152 5' 0" - 46-62 155 5' 1" 55-66 47-63 157 5' 2" 56-67 49-65 160 5' 3" 57-68 50-67 162 5' 4" 58-70 51-69 165 5' 5" 59-72 53-70 167 5' 6" 60-74 54-72 170 5' 7" 61-75 55-74 172 5' 8" 62-77 ...

BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI

 BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI.   ๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š   BAWASIRI NI NINI?   Bawasiri (kikundu, future, puru au mjiko ) ni hali ya kutuna kwa mishipa ya damu katika mfereji wa sehemu ya haja kubwa (anus). Kuna aina mbili za Bawasiri;   1. Bawasiri za ndani ( internal haemorroids )   2. Bawasiri za nje ( external haemorroids )  Bawasiri za ndani hua na dalili ya kupata kinyesi kilichokua na damu,  bawasiri za nje hua na dalili ya maumivu makali wakati wa kujisaidia pamoja na kinyama kutoka kwa nje.  NINI VISABABISHI VYA BAWASIRI?   1๏ธโƒฃHistoria ya familia, mara nyingi baadhi ya familia hukumbwa na changamoto hii. Na hua watu wa familia hiyo husika wanakua na hili tatizo. 2๏ธโƒฃKupata choo kigumu mara kwa mara husababisha mtu kutumia nguvu nyingi (straining) ambayo husababisha bawasiri kutokea. 3๏ธโƒฃUnene (uzito uliopitiliza) hua ni kisababishi cha bawasiri kwa sababu ya kuongezeka kwa Rectal Vein Pressure. 4๏ธโƒฃKu...

CALORIE ZA VYAKULA VYA TANZANIA

 CALORIES ZA VYAKULA TANZANIA   NINI MAANA YA CALORIE?    Calorie ni kiasi cha nishati kinachohitajika ili kuongeza joto la gramu moja ya maji (ยฐC). Kwa lugha nyepesi, calorie katika chakula hutoa nishati (energy) kwa njia ya joto ili miili yetu iweze kufanya kazi. Hii ni kwa sababu miili yetu huhifadhi na kuchoma calorie kama mafuta.  UHUSIANO WA CALORIE NA UZITO WA MWILI.  Kwa kawaida, kila chakula kina kiwango chake cha calorie. Hivyo unapokula chakula, unaingiza mwilini calorie kadhaa, na mwili wako pia unatumia calorie katika kuweka uhai. Lakini unapokula chakula, unaingiza calorie mwilini. Na mwili wako pia unatumia calorie kama nishati. Hivyo unapokula calorie nyingi kuliko mwili unavyoweza kutumia, zinahifadhiwa kama mafuta na utaongezeka uzito. Unapotumia calorie nyingi kuliko unavyoingiza mwilini, unapungua uzito. Na ukitumia kiasi sawa na unachoingiza, basi unabaki na uzito ule ule.   MWANADAMU ANAHITAJI WASTANI WA CALORIE NGAPI? ...