Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2020

BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI

 BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI.   💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊   BAWASIRI NI NINI?   Bawasiri (kikundu, future, puru au mjiko ) ni hali ya kutuna kwa mishipa ya damu katika mfereji wa sehemu ya haja kubwa (anus). Kuna aina mbili za Bawasiri;   1. Bawasiri za ndani ( internal haemorroids )   2. Bawasiri za nje ( external haemorroids )  Bawasiri za ndani hua na dalili ya kupata kinyesi kilichokua na damu,  bawasiri za nje hua na dalili ya maumivu makali wakati wa kujisaidia pamoja na kinyama kutoka kwa nje.  NINI VISABABISHI VYA BAWASIRI?   1️⃣Historia ya familia, mara nyingi baadhi ya familia hukumbwa na changamoto hii. Na hua watu wa familia hiyo husika wanakua na hili tatizo. 2️⃣Kupata choo kigumu mara kwa mara husababisha mtu kutumia nguvu nyingi (straining) ambayo husababisha bawasiri kutokea. 3️⃣Unene (uzito uliopitiliza) hua ni kisababishi cha bawasiri kwa sababu ya kuongezeka kwa Rectal Vein Pressure. 4️⃣Kukaa sehemu moja kwa muda mrefu au kutokufanya mazoezi. (sed

KWA NINI MZANI SIO NJIA BORA ZAIDI KUJUA KAMA UNAPUNGUA.

JE, MZANI AU KUJUA KILO NI SAHIHI KUJUA KAMA UNAPUNGUA? Mara nyingi hutokea watu kukata tamaa wakati wapo kwenye safari yao ya kupungua kwa sababu ya kuangalia kilo zao kwenye mzani. Unakuta ameanza Diet mwezi uliopita, lakini akiangalia kilo zake kwenye mzani haoni mabadiliko makubwa... Hapa nina solution mbili kama huyu mtu ni wewe 1. Usitumie mzani kwanza 2. Fahau jinsi ya kutumia mzani vizuri. KWA NINI NIMESEMA USITUMIE MZANI KWANZA? Kwa sababu mzani unakupa sehemu ndogo tu ya taarifa unazotakiwa kuzipata, yaani inakwambia uzito wako wa mwili kwa ujumla.  Lakini mzani huo huo hautakupa taarifa kuhusu kiwango cha mafuta (FAT),  kiwango cha maji yaliopo mwilini, uzito wa mifupa, uzito wa misuli N.K hivi vyote nilivyovitaja vinachangia uzito kwenye mwili wako. sasa lengo letu ni kupunguza mafuta, lakini sio kupunguza misuli au kitu kingine. Ni vyema kufahamu ya kwamba, kilo utakazopima kwenye mzani hazikupi taarifa ya kwamba umepungua mafuta kwa kiasi gani.  Angalia picha ya hawa watu

UHUSIANO WA KUNDI LA DAMU NA UZITO

  UHUSIANO WA KUNDI LA DAMU NA UZITO . Kuna msemo unasema, ONE MAN ' S FOOD IS ANOTHER ONE ' S POISON . Ukiwa na maana ya kwamba, chakula kinachomnufaisha mtu mmoja, kwa mwingine ni hasara. Dr. Peter J D ' Adamo alifanya utafiti na kugundua ya kwamba kuna uhusiano mkubwa kati ya afya ya mtu pamoja na kundi la damu la mtu husika. Ndio akaja na msemo unaosema ya kwamba ONE MAN ' S FOOD IS ANOTHER MAN ' S POISON . Kwenye tafiti yake, aligundua ya kwamba afya ya mtu huimarika Zaidi endapo atakula kulingana na kundi lake la damu. Hata kwenye swala la UZITO. Mtu wa kundi flani la damu anaweza kunenepa kwa kula vyakula vya aina flani, ambavyi vyakula hivyo hivyo akila mtu mwingine, basi atapungua. Katika somo hili, tutaangalia uhusiano wa uzito wa mtu pamoja na kundi la damu. BLOOD GROUP O VYAKULA VINAVYOWAONGEZEA UZITO BLOOD GROUP O ·          Ngano na gluteni yake : kundi hili wakitumia ngano yenye gluten huingilia uzalishwaji wa insulin na hivyo kupeleke

VYAKULA VINAVYOTUNZA AFYA YA NGOZI (ANTI-AGING FOODS)

  VYAKULA VINAVYOHITAJIKA KATIKA AFYA YA NGOZI. (ANT-AGING FOODS) Bila shaka unafaham ya kwamba kuna watu ambao wamekua na makunyanzi na kuonekana wakubwa (wazee) kuliko umri wao halisi. Lakini pia kuna ambao ngozi zao hulegea baada ya kupungua na kuonekana kusinyaa pamoja na makunyanzi. Collagen nip rotini muhimu sana katika kuipa ngoz afya, na ndiyo inayohusika na kufanya ngozi iwe na hali ya kuvutika (elasticity) Lishe inahusika sana kwa kiasi kikubwa kufanya ngozi yako iwe vizuri na isiwe na makunyanzi au kuonekana yam zee kuliko umri wako. VYAKULA MUHIMU KWA AFYA YA NGOZI . ·          KITUNGUU SWAUMU : kina kiwango kikubwa cha sulfur inayosaidia kuzalisha kiwango cha collagen. Hivyo jitahidi kutumia kitunguu swaumu kama moja ya viungo vyako muhimu. ·          MAHARAGE : protini itokanayo na maharage husaidia kuongeza kiwango cha collagen, bakuli moja la maharage lina wastani wa gram 15 za protini ambazo zikifanyiwa mmeng ' enyo wa chakula, amino acids zinatumika

MSIMU WA SIKUKUU NITUMIE DIET GANI?

  NITUMIE DIET GANI MSIMU WA SIKUKUU? ❔❓❔❓ kama umekua ukitumia diet ya aina flani kwa ajili ya kupungua uzito (na kueka afya nzuri kwa ujumla), basi utakua umeshajiuliza swali la namna hii.  Huu ndio ule msimu ambao kila kona unayopita wamepika chakula ambacho wewe ukitumia ni kinyume na Diet ambayo unaitumia katika kupungua uzito. ONDOA SHAKA... FANYA YAFUATAYO : Kabla ya yote, ni vyema ukafahamu ya kwamba ROME WAS NOT BUILT IN ONE DAY . Yaani Mji wa Roma haukujengwa ndani ya siku moja. bali ni mkusanyiko wa siku nyingi za ujenzi ndipo mji ukakamilika. hivyo, hata kwa mtu ambae ana uzito mkubwa leo hii. sio kwamba aliongezeka ndani ya siku moja. Bali ni mkusanyiko wa siku nyingi ambazo hakua anakula vizuri au kua na mtindo mzuri wa maisha. POINT YANGU NI IPI HASWA ❓❔ kula kawaida siku ya siku kuu au msimu wa siku kuu hakutakufanya uharibu Diet yako ambayo umekua ukiendelea nayo. Hivyo bado unaweza kujumuika na ndugu jamaa na marafiki na mkala, kunywa na kufurahi pamoja. ZINGATIA MAMB

Hormonal Imbalance, Visababishi na Tiba yake

  Hormonal Imbalance HORMONAL IMBALANCE    Hormonal imbalance ama kwa Kiswahili ni mvurugiko wa kichochezi (hormone). Mara nyingi huwakumba wanawake Zaidi, ingawa hata wanaume wanaweza kua na tatizo hili. na kusababisha kiwango kidogo sana au kikubwa sana cha hormone au kichochezi chochote kutokukaa sawa.  NINI HUSABABISHA HORMONAL IMBALANCE  1️⃣Ulaji Mbovu wa chakula 2️⃣Unene (uzito uliopitiliza) 3️⃣Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango.  4️⃣Stress na msongo wa mawazo 5️⃣kisukari 6️⃣Hyperglycemia (uzalishwaji wa kuzidi wa glucagon) 7️⃣Hypoglycemia (insulin kuzalishwa nyingi kuliko glucose kwenye damu) 8️⃣Saratani pamoja na vimbe kwenye via vya kizazi.  DALILI ZA HORMONAL IMBALANCE  1️⃣Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa 2️⃣Kutokushika mimba (infertility) 3️⃣Kutokua na uwezo wa kusimamisha uume 4️⃣Mbegu za uzazi kuwa chache (low sperm count) 5️⃣Uke kua mkavu (vaginal dryness) 6️⃣Kubadilika badilika kwa mzunguko wa hedhi au maumivu makali 7️⃣Kutokupata usingizi vizuri 8️⃣Kuongezeka uzito